DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Watu wanalaumu vitu kabla hawajauliza sababu.
Mara nyingi system admins kwenye taasisi nyeti au walipo watumiaji wengi wenye uelewa mdogo au uelewa mkubwa sana wa vifaa na mifumo ya ICT wana disable CD drive na USB ports kwa sababu za kiusalama wa mfumo(System).
Wanatoa access level kutokana na group flani Kama ilivyo muelezea mdau mmoja huko juu.

Mimi naona wangelaumu gharama kubwa za kuingiza hizo taarifa hapo ningewaelewa.
Yeah na hiyo ufanywa kwa usalama wa Server 👏👏👏👏
 
Waziri wa Afya ninaandika hili kwa uchungu mkubwa na majuto ya kujitawala, mimi ninaumwa nilikwenda hosipitali ya mkoa nikafanya X-Ray na Ct-Scan, kisha nikapewa rufaa kwenda Muhimbili.

Nimeenda Muhimbili tarehe 9/11/2023 nikiwa na CD ya Ct-Scan ili daktari aicheze kuona tatizo langu, daktari hawezi kuicheza mpaka niipeleke ICT eti waikopi waiweke kwenye mfumo wa Muhimbili!

Na ili waikopi ninatakiwa nilipe sh 86,000/=? Bila hivyo nikae na CD yangu nikafilie mbali, sina hela hiyo na pia sioni uhalali wa malipo hayo kwani hiyo CD ukiweka kwenye kompyuta inafunguka haihitaji uchawi wowote ule.

Mhe. Waziri walionipa CD hiyo ni hospitali ya Serikali na niligharamia hiyo Ct- Scan kwa ajili ya madaktari wajue tatizo langu na si kwa ajili yangu binafsi ya kutengeneza Bongo muvi, hiyo CD kwangu mimi ni nyangarakasha kwani sina utaalamu wa kuisoma na nimeingia hasara ya kufanya Ct- Scan.

Kwaheri kuonana ni majaliwa.
Na ili waikopi ninatakiwa nilipe sh 86,000/=? Bila hivyo nikae na CD yangu nikafilie mbali, sina hela hiyo na pia sioni uhalali wa malipo hayo kwani hiyo CD ukiweka kwenye kompyuta inafunguka haihitaji uchawi wowote ule.[emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole ndugu yetu.Hiyo ndio Tz.Mabazazi,madhalimu na walafi wapo kila mahali.Na kwa kweli mlilie Muumbaji tu.Hao wengine hawawezi kukusaidia
 
Kitengo cha ICT naona wana watu wendawazimu.

Kufanya Uploading ya data za kwenye CD kuziingiza kwenye mfumo ni kuijaza DATABASE bila sababu ya msingi. Kwanini Daktari asiwe na files zake yeye mwenyewe bila kuwa redirected na watu wengine? Kingine faragha ya Mgonjwa ipo wapi hapo? Maana IT anaona kila kitu.

Kwa upande wa pili, kwanini hizo Hospital za rufaa zisiwe na portal ya kutuma hizo data moja kwa moja kwa daktari wa Muhimbili? Dunia inatoka ktk physical devices hasa hzi storage devices kama vile CD.

Inatakiwa Ubunifu wa hali ya juu ktk hii ishu mifumo isomane.
Kwa nchi yangu Tanzania bado sana. Viongozi wanajali matumbo yao kwanza. Madaktari hawezi kubali hilo litokee kwani itapunguzia njia haramu ya kupata pesa kwa wagonjwa.

Tanzania ni nchi ya kitapeli kila mtu tapeli. Inaumiza sana.
 
Acha hizo, vipimo nilivitaka mimi na nilifanya vipimo 4 vikiwemo X-ray na CT- Scan na vyote nililipia bila tatizo pamoja na gharama za matibabu, kinachonikwaza ni hiyo shs 86,000/= ya kuiingiza DVD ya CT Scan kwenye mfumo wa Muhimbili badala ya dakitari kuisoma kwenye kompyuta yake na kunitibu.
Hebu nieleweshe wapi nimeshindwa kulipia.
mkuu kuna mtu kakuuliza unayo report ya hyo ct scan kutoka kwa mtaalamu aliyefanya hyo ct scan kutoka hospital A? mbali na hyo cd, maana radiologist ndo mwenye utaalamu mkubwa wa kutafsiri hzo picha mkuu wangu.
 
Tatizo siyo kutibiwa tatizo kwanini dakitari asiisome hiyo CD na kisha anitibu bila ya kutaka picha yangu iingizwe kwenye seva za Muhimbili, ili iweje.
sasa mkuu taarifa zako si zinatakiwa ziwe kwenye database for future reference mkuu, cd si inaweza haribika au kupotea mkuu, halafu si wanasema kila kitu kinatakiwa kiwe kwenye mfumo boss.
 
Ripoti imeambatanishwa na DVD, aliyeisoma ni mtaalamu wa hispitali ya serikali.
Mimi bado sijapata mtu akithibitisha uhalali wa hiyo gharama ys shs. 86,000/= kwa ajili ya DVD kuingizwa kwenye mfumo wa Muhimbili, ili iweje!
Ndugu heshim taratibu za hospital uliopo,
 
Wewe ni mgonjwa ujiwezi wala hujui kama kuna vifungashio vingine vinatakiwa viambatanishwe unapofanyiwa transfer...au umesahau wengine wanafanyiwa transfer wakiwa hawajiwezi na wanaoshughulikia wanakuwa hawana uelewa wowote wa hizo nyaraka, je huko Mhimbili hawana uwezo wa kuwasiliana na Hospitali iliyotoa transfer ili missing documents zitumwe? Mbona taasisi zingine wanafanya mawasiliano?
Yaani kwa akili yako timamu unadiriki kumlaumu mgonjwa kuwa amesahau nyaraka ya hospitali kwenda hospitali nyingine!!! Badala ya kutoa lawama kuwa amesahau kutumia dawa kwa wakati.

Acha kutetea upumbavu
Da. Watanzania tuna matatizo makubwa. Hili unalosema hata Ulaya hawezi kufanya hivyo. Yaani hospital ijivike jukumu la kuwasiliana na ulikotoka ili wapate records zako? Ni hivi: tatizo letu kubwa ni kuwa wananchi wengi hawajui tatizo letu hasa ni nini! Tatizo ni uongozi wa CCM uliofeli kwa namna zote uliofanya wananchi wawe maskini wa kutupwa na kutokujiweza kiuchumi. Kama tunataka mabadiliko basi tuiondoe CCM na siyo kulalamika kusiko na maana.
 
sasa mkuu taarifa zako si zinatakiwa ziwe kwenye database for future reference mkuu, cd si inaweza haribika au kupotea mkuu, halafu si wanasema kila kitu kinatakiwa kiwe kwenye mfumo boss.
Sihitaji future reference ninahitaji tiba ya sasa hivi kwanza, nimeingia gharama za vipimo vinne vikiwemo X Ray na CT Scan si kwa ajili ya hospitali iweke kumbukumbu yangu bali ni kwa ajili ya tiba ya sasa na si kwa mwaka keshokutwa.
 
Da. Watanzania tuna matatizo makubwa. Hili unalosema hata Ulaya hawezi kufanya hivyo. Yaani hospital ijivike jukumu la kuwasiliana na ulikotoka ili wapate records zako? Ni hivi: tatizo letu kubwa ni kuwa wananchi wengi hawajui tatizo letu hasa ni nini! Tatizo ni uongozi wa CCM uliofeli kwa namna zote uliofanya wananchi wawe maskini wa kutupwa na kutokujiweza kiuchumi. Kama tunataka mabadiliko basi tuiondoe CCM na siyo kulalamika kusiko na maana.
Unajua maana ya synchronization? Yaani taarifa zote za mgonjwa zinakuwa online line in confidential form. Kama ikihitajika zinapatikana, mbona taarifa za NIDA zipo kwenye mfumo zinasomwa na mamlaka zingine kama Uhamiaji?
 
Mkuu kuna kitu kimoja unakisahau sana (Samahani kusema hivyo)
Kumbuka Taarifa zako zote za ugonjwa pamoja Na CT-Scan ulopiga zipo Huko Hospitali ya mkoa ulikotoka..

Muhimbili ni hospitali Ya Rufaa Haiwezi kurelly Kwenye Report uliyokuja nayo kutoka Hopitali nyingine hii hairuhusiwi katika Refferal system guildlines..

Kusoma report uliyokuja nayo atasoma Ili kujua Anaanzia wapi kuangalia na nini hasa afanye zaidi ili.kugundua tatizo lako..
Hawezi kuchukua Moja kwa moja Report iliyoandikwa na hospitali Nyingine na yeye akaifanyia kazi bila kufanya na yeye uchunguzi wa vipimo vilivyofanywa ikiwa atarely only kwwnye report ya uchunguzi uliyokuja nayo bila kuangalia CD uliyoleta...

Unfikiri kama Yule Daktari wa Ulikotoka alikosea Kuku-Diagnose na yeye akachkua report yko kama ilivyo Ingekuwepo maana ya Wewe kupewa Rufaa

Umuhimu wa kuingizwa Taarifa zako Kwenye Mfumo wa kimatibabu (HMIS)
Kuingiza Taarifa zako katika mfumo wa kimatibabu ni muhimu sio lazima uwe maarufu kwa sababu kwanza...

  • Inafanya Taarifa zako ziwe more accesible na jopo jingine la madaktari kama Taarifa zako zitabidi zitatuliwe na Wataalamu wa juu zaid kama mabingwa zaidi...hakutakuwa na haja tena ya kwenda kitengo kingine wakuulize maswali ambayo tayari wanayoma kwenye mfumo au kufanya vipimo ambavyo tayari vimeshafnywa
  • kutafanya iwe vyepesi kurejea Taarifa zako za kimatibabu pale ambapo Utapata tatizo jingine na ili wajue jinsi ya kukusaidia ensapo tatizo jipya linaweza kuwa ni chanzo kutoka tatizo la zamani
  • mambo ya legas cases pia
  • ziko nyingi sana ila ni muhimu taarufa kutunzwa kwa ajili ya marejeo ya baadae
NB: kumbukumbu za Hospitali hawaingizwi maarufu tu ni kwa sababu ya Taarifa za kimatibabu kwa ajili na kwa ajili ya ofisi...

Nakupa scenario chukulia Umetibiwa Muhimbiri miaka Mitatu ilopita lets say Kisukari na ukawa unatumia Dawa aina fulani ambazo ulipewa umetumia dawa kwa muda mrefu na una Mzio (Allgy ) na dawa fulani ukitumia unazidiwa..
BAada ya miak miwili umepelekwa ukiwa umepata ajali n hujitambui unafikiri zile Taarifa zilizowekwa hazitakufaa kuchagua aina ya matibabu Utakayopewa?
Binafsi nadhani umetoa maelezo ya kutosha kabisa ya kimfumo, mpo sawa kabisa kwa kufanya hivyo. Hapo utata unakuja kwenye gharama, uploading file lwenye systems za MNH kwa 86,000 mbona ni pesa nyingi sana mkuu? Otherwise maelezo yako mimi nakubaliana nayo.
 
Sihitaji future reference ninahitaji tiba ya sasa hivi kwanza, nimeingia gharama za vipimo vinne vikiwemo X Ray na CT Scan si kwa ajili ya hospitali iweke kumbukumbu yangu bali ni kwa ajili ya tiba ya sasa na si kwa mwaka keshokutwa.
Mkuu,
Future reference kwa taasisi kubwa kama MNH ni muhimu, lazima rekodi zako zihifadhiwe kwa ajili ya matumizi ya baadae, nimekuwa na wagonjwa kadhaa wamepitia MNH, muhimu sana kuweka rekodi.

Nisichoelewa, scan uliyofanya hospitali ya mkoa iligharimu kiasi gani? Na kingine ambacho nashindwa kuuelewa uongozi wa hospitali, gharama ya kufanya uploading ya hilo file, kwa nini iwe kubwa kiasi hicho?

Binafsi naamini ni lazima files ziwe uploaded ili kuweza kufanya follow up na kuweka data zako kwenye mifumo yao.
 
Unajua maana ya synchronization? Yaani taarifa zote za mgonjwa zinakuwa online line in confidential form. Kama ikihitajika zinapatikana, mbona taarifa za NIDA zipo kwenye mfumo zinasomwa na mamlaka zingine kama Uhamiaji?
Umesoma nilichoandika? Wachana na hiyo ya NIDA, mimi nimeishi kwenye nchi zenye application ya synchronization in real life. Unakwenda kumwona Dr akishaandika vipimo na dawa taarifa zako unazikuta tayari kule unakokwenda kufanya vipimo au pharmacy yoyote mjini. Ukienda hospital nyingine, nako dr anakuomba idhini kama utakubali a-retrieve data zako kutoka hospital uliyotibiwa mwanzo. Back to the topic: Rudi usome kwa ufahamu nilichoandika ili uelewe!
 
Bahati mbaya mlalamikaji hajaongea ukweli either kwa makusudi au hakumuelewa daktari. Issue kama hiyo iliwahi kunitokea . Maelezo niliyopewa ni kua mgonjwa wangu amekuja na CD yenye picha za CT scan kutoka hospitali nyingine,bila kua na report yake. Kusoma picha za CT scan ni taaluma inayosomewa,si Kila daktari atakua na uwezo wa kusoma hizo picha na kuona tatizo. usipokuja na report, unaweza shauriwa ufuate system ya muhimbili ambapo wanatoa hiyo huduma ya kuzisoma hizo picha na pia hiyo report itakua posted Kwenye system. Nilielekezwa na nikaelewa ni kwa nia njema ili daktari aweze kujua shida ya mgonjwa na mgonjwa apate matibabu sahihi. Shida tu ni gharama zinaongezeka,but alternative inaweza kumgharimu mgonjwa maisha yake.
 
Waziri wa Afya ninaandika hili kwa uchungu mkubwa na majuto ya kujitawala, mimi ninaumwa nilikwenda hosipitali ya mkoa nikafanya X-Ray na Ct-Scan, kisha nikapewa rufaa kwenda Muhimbili.

Nimeenda Muhimbili tarehe 9/11/2023 nikiwa na CD ya Ct-Scan ili daktari aicheze kuona tatizo langu, daktari hawezi kuicheza mpaka niipeleke ICT eti waikopi waiweke kwenye mfumo wa Muhimbili!

Na ili waikopi ninatakiwa nilipe sh 86,000/=? Bila hivyo nikae na CD yangu nikafilie mbali, sina hela hiyo na pia sioni uhalali wa malipo hayo kwani hiyo CD ukiweka kwenye kompyuta inafunguka haihitaji uchawi wowote ule.

Mhe. Waziri walionipa CD hiyo ni hospitali ya Serikali na niligharamia hiyo Ct- Scan kwa ajili ya madaktari wajue tatizo langu na si kwa ajili yangu binafsi ya kutengeneza Bongo muvi, hiyo CD kwangu mimi ni nyangarakasha kwani sina utaalamu wa kuisoma na nimeingia hasara ya kufanya Ct- Scan.

Kwaheri kuonana ni majaliwa.
Pole sana Mkuu, njoo inbox
 
Sihitaji future reference ninahitaji tiba ya sasa hivi kwanza, nimeingia gharama za vipimo vinne vikiwemo X Ray na CT Scan si kwa ajili ya hospitali iweke kumbukumbu yangu bali ni kwa ajili ya tiba ya sasa na si kwa mwaka keshokutwa.
sawa mkuu we endelea kukomaa nao watakutibu tu hawana namna.
 
Back
Top Bottom