Hongera sana Bwana Makirita. Hii ni habari njema sana. Nimekuwa pia mwanachama mwaminifu wa UTT na faida yake naendelea kuiona. Asante kwa kuendelea kutuelimisha kupitia experience yako pia. Naomba ushauri mmoja.
Nami pia nipo kwenye safari ya kuusaka utajiri na uhuru wa kifedha. Nina uwezo wa kusave 4,200,000 kila mwezi kwenye mfuko wa UTT na nimekuwa nikifanya hivyo. Nataka nifikie uhuru wa kifedha haraka iwezekanavyo ndani ya miaka 7 mpaka 8 ijayo. Unanishauri nijikite katika uwekezaji upi hasa ili niweze kufikia malengo yangu kwa haraka zaidi?
NB: Sina muda wa kusimamia biashara kabisa
Hongera sana mkuu kwa kuwa mwekezaji, hasa kupitia UTT ambayo ni fursa nzuri sana kwa hapa nchini kwetu.
Kuhusu kufikia uhuru wa kifedha ndani ya huo muda na kwa kiasi unachowekeza, inategemea zaidi matumizi yako ya kila mwezi.
Hiyo ni kwa sababu UHURU WA KIFEDHA ni pale uwekezaji wako unapoweza kukuingizia fedha ya kuendesha maisha yako bila ya kulazimika kufanya kazi moja kwa moja.
Huwa nina miongozo mbalimbali ya kukokotoa kiasi cha kuwekeza na muda ili mtu kufikia uhuru wa kifedha, kama utahitaji tutawasiliana tufanyie kazi.
Ila kwa jibu la haraka na ambalo kila mtu anaweza kufanyia kazi ni kuchukua wastani wa matumizi yako ya mwezi na kuzidisha mara 100. Kisha kuwa na uwekezaji wenye hiyo thamani, kwenye UTT au BONDS.
Kwa mfano kama matumizi yako ya mwezi ni TSH 5,000,000/= (milioni 5) unahitaji kuwa na uwekezaji wenye thamani ya Tsh 500,000,000/= (milioni 500).
Ukiweza kuwa na uwekezaji huo kwenye Mfuko wa UMOJA, UKWASI au BOND wa UTT au ukawa na bonds za serikali kwa thamani hiyo, au mchanganyiko wa aina hiyo, utafikia uhuru wa kifedha.
Hivyo anza na matumizi yako ya mwezi kwa kipindi hicho utakachokuwa umestaafu na zidisha mara 100 kisha kokotoa itakuchukua muda gani.
MUHIMU; Hii niliyotoa ni rough calculation, kama unataka ukokotozi sahihi na wa kina zaidi, tuwasiliane kwa wasap 0678 977 007. Karibu sana.