Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,133
- 12,361
Yaani hela yako iongezeke asilimia 15 kwa muda wa miaka 25?bond za BOT zinalipa mpaka 15% for 25 years, nafikiri ni easy money kwa kiasi fulani
Huu ni uwekezaji au ni uwekezwaji?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani hela yako iongezeke asilimia 15 kwa muda wa miaka 25?bond za BOT zinalipa mpaka 15% for 25 years, nafikiri ni easy money kwa kiasi fulani
Nimeshangaa sana. Miaka 25?Why easy money,Ukae na hela yangu for 25 years unipe 15%. ?
Inflation ni 4.6 to 6 kwa mwaka. Mnaakili nyie?
Kongole sana na Mungu akubariki.Rafiki yangu mpendwa,
Nimekuwa napenda utajiri tangu nikiwa mtoto mdogo.
Nakumbuka niliwahi kumwambia mama yangu kwamba kwenye maisha yangu lazima nitakuwa tajiri. Alicheka na kuniambia ni utoto tu unanisumbua.
Nikiwa shuleni nilifuata vizuri ile kanuni maarufu ya NENDA SHULE, SOMA KWA BIDII, FAULU, UTAPATA KAZI NA KUWA NA MAISHA MAZURI.
Lakini katika kufuata hiyo kanuni, tangu naanza darasa la kwanza mpaka nafika chuo kikuu, sikuwahi kufundishwa chochote kuhusu usimamizi wa fedha binafsi.
Baada ya kutoka kwenye mfumo wa elimu na kuingia mtaani, ndiyo niliona ombwe kubwa lililopo kwenye eneo la USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI (PERSONAL FINANCE MANAGEMENT).
![]()
Hilo lilinisukuma mimi binafsi kuanza kujifunza peke yangu kuhusu eneo hilo la fedha binafsi. Nilisome vitabu vingi vya fedha, utajiri na uhuru wa kifedha. Vitabu hivyo vilinifungua sana ufahamu wangu kwenye eneo la fedha.
Vitabu vitatu vilivyonifungua sana ni THINK AND GROW RICH, THE RICHEST MAN IN BABYLON na RICH DAD POOR DAD. Mwaka 2012 niliamua rasmi kwamba nitaweka kwenye matendo yale yote ninayojifunza kwenye vitabu hivyo.
Tangu mwaka 2013 nimekuwa najifunza na kufanya uwekezaji kwa vitendo, kitu ambacho kimekuwa kinanipa manufaa makubwa.
Kwa sababu nimekuwa naandika na kufundisha, nimekuwa pia nikiandikia na kufundisha eneo la fedha binafsi. Pamoja na fursa nyingi za uwekezaji na kujenga utajiri zinazopatikana Tanzania, bado watu wengi hawanufaiki nazo.
Hilo ndiyo limekuwa linanisukuma kushirikisha maarifa haya ya fedha na utajiri kwa watu wengi zaidi. Pamoja na kufanya hilo kwa nia kubwa, bado watu wengi wamekuwa siyo waelewa, wakiwa hawaamini kama yale ninayofundisha yanaweza kufanya kazi kwao.
Benki Kuu Ya Tanzania (BOT) wakiwa kama watu wenye dhamana ya usimamizi wa fedha hapa Tanzania, wameona ombwe kubwa lililopo kwenye uelewa wa fedha kwa wananchi.
Kumekuwa na harakati za serikali kuingiza somo la usimamizi wa fedha binafsi kwenye mtaala wa elimu. Maboresho ya mtaala wa sasa yanaleta elimu ya fedha kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.
Pamoja na hatua hizo, ilionekana wazi kuna kundi kubwa la watu ambao hawapo kwenye mfumo wa elimu. Kundi hilo linahitaji kupata elimu sahihi ya fedha ili kuwa na maisha bora.
Na hapo ndipo BOT ilipokuja na programu ya mafunzo kwa watoaji wa elimu ya fedha na kuwaidhinisha ili wakatoe elimu ya fedha kwa umma. BOT wameweza kuandaa na kuendesha mafunzo hayo ya watoa elimu ya fedha na kuwatunuku vyeti vya CERTIFIED FINANCIAL EDUCATORS.
![]()
Ninayo furaha kukujulisha kwamba mimi Kocha wako, Amani Emanuel Makirita ni mmoja wa kundi la kwanza kabisa kupate elimu hii. Hivyo sasa nimethibitishwa kuwa mtoaji wa elimu ya fedha.
Rafiki, nimekuwa nafundisha na kufanya hayo kwa vitendo kwa miaka zaidi ya 10 sasa. Kupata uthibitisho huu inanipa mimi fursa ya kuendelea kufanya kwa upana zaidi na kuaminika na wengi.
Hivyo nikukaribishe tuendelee kushirikishana elimu hii na kufanyia kazi ili kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha.
Kwa sasa elimu ya fedha ninayotoa inasimamia maeneo matano muhimu;
1. Kuwa na njia halali ya kuingiza kipato cha uhakika.
2. Kudhibiti matumizi yasizidi kipato.
3. Kuondoka kwenye madeni binafsi.
4. Kuwa na akiba kwa ajili ya dharura na mipango ya maendeleo.
5. Kufanya uwekezaji kwa ajili ya uhuru wa baadaye.
![]()
Pia nafundisha na kusimamia njia kuu mbili za kujenga utajiri.
Ya kwanza ni njia ya MWENDO POLE, hii inahusisha kuwekeza asilimia 10 ya kipato kwa muda mrefu. Njia hii inachukua miaka 20 mpaka 30 kujenga utajiri.
Njia ya pili ni ya MWENDO KASI, hii inahusisha kuwekeza asilimia 50 ya kipato kwa muda mfupi. Njia hii inachukua miaka 10 mpaka 15 kujenga utajiri.
Katika kuhakikisha unapata elimu hii na kunufaika, nina programu kuu mbili;
Moja ni NGUVU YA BUKU, hii ni programu ya bure kabisa ambapo unapata mafunzo na usimamizi wa kujenga utajiri.
Mbili ni UHURU WA KIFEDHA, hii ni programu ya kulipia ambapo unasimamiwa kufikia uhuru wa kifedha kama ulivyopanga.
Kupata mafunzo na huduma hizi, tuwasiliane kwa namba 0678 977 007.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua hayo kwa kina na hatua za kuchukua ili uweze kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha. Karibu ujifunze na kuchukua hatua.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
www.amkamtanzania.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.
Id nyingi zimekuja kumsapoti mleta uzi. Ni kitu kimoja kua na nadharia na ni kitu kingine nadharia kua practically doable.
Hapana 😂, ni kila mwaka inaongezeka 15% na kuna zaidi ya hapo ndio maana nilimwambia jamaa atoe somo la bond specific za BOT maana ndio zinawahusuYaani hela yako iongezeke asilimia 15 kwa muda wa miaka 25?
Huu ni uwekezaji au ni uwekezwaji?
😄Binafsi nimempongeza Kwa kutunukiwa cheti, hata kwenye maisha tunawapiongeza wanaohitimu wakati tunajua wana kazi kubwa ya kwenda kuitumia hiyo Elimu kwenye maisha Yao, hiyo ni kipengere tofauti kabisa.
Anaweza akapata hiki cheti na bado asiweze kutekeleza adhimio lake.
Kupata lesseni ya udereva jambo moja, kuwa dereva mzuri jambo lingine.
Hua naliona tatizo kidogo kwenye baadhi ya majibu yake, vinginevyo anajitahidi na yuko na bidii.
Shida nyingine ni kuamini kile anachokiamini yeye ndio suluhu ya kumfaa Kila mtu. Ukitofautiana na nadharia zake, inatokea mikwaruzano.
Kuna wapemba, wakinga na wachaga hautawaona kwenye semina yoyote ya personal finance lakini wanapesa chafu.
Hili ni eneo pana,Hongera. Kwa sasa kwenye soko ni benki gani inatoa mikopo kwa riba nzuri?
Tunapiga kote kote mkuu.Ulimwengu wa sasa hasa huku kwetu Tanzania watu hawapendi kusoma vitabu.
Wewe jikite kwenye mitandao ya kijamii, unaandaa mada na kuifundisha na kutupia short videos mtandaoni. Hiyo ndio njia rahisi ya kuwapata walengwa wako.
Hakikisha uko mitandao yote, mitandao ya kulipia hakikisha unalipia ili kuwafikia wengi zaidi.
Kwa sababu nimekiwekea juhudi, nimelipa ada, nimesoma na kufaulu mtihani.Sasa mbona umeshangilia kukipata kama unalijua hilo?
Mkuu,Hongera Ila ngoja mie niongee kinyume na emotions zako. Why usiwe tajiri kwanza ndio watu wakaja kwako kutaka uwape maarifa Mana uelewe vitendo ni gharama mno kuliko maneno.
Kila mtu anaweza akaongea na akafundisha Ila sio kutenda.
Actions are strong than words hata wanao wafundishe kwa kufanya ama ku behave unavyotaka wao waji behave.
Binadamu tunaelewa kwa kuona kuliko kwa kusikia.
Ndio yake kishimba anasema wewe unakuja na Cheti chako na tai yako Halafu unataka usimamie hela zangu kweli.
Yaani Cheti tu na tai u trade na hela zake. Aliongea kuhusu benki waliyotaka kufungua wao wametoa pesa nyingi zaidi ya 500M jumla 2bn benki ifunguliwe Ila Sasa eti bot wakasema kuwa mtu asiye na Cheti cha masuala ya pesa ama iyo elimu asiwepo katika bodi ya wakurugenzi.
Kupata pesa ni kitendo, hela ziishi kwako ama zisiondoke kwako ni tabia yako na hela kuzidi kuzaliana ni suala la maarifa na ujuzi.
Sasa hapo kwenye tabia ni kazi mno kufundisha mtu tabia. Ni sawa useme utamfundisha mzinzi qache uzinzi, Malaya aachane umalaya,
Mwizi aache wizi, mvivu awe na nguvu ama bidii za kazi,mlevi ama mvuta sigara aachane na hizo tabia.
Kuongea ni rahisi mno na unayoyaongea sio kuwa sio ukweli unakuta ni ukweli Ila utendaji ni ishu nyingine hata wewe unayeyaongea huwezi yafanya.
Samahani kwa kwenda kinyume na wewe Ila nakupongeza kumiliki Cheti cha CFA.
Ila jitahidi na ninakuombea uwe like abood watu watakuwa wanaelewa mno masomo yako hata Yule wa Kijijini atakuelewa.
Sasa unaandika kitabu namna ya kumiliki pesa Halafu unakiuza badala ya ugawe bure Mana tayari umeshatumia hizo mbinu kumiliki hela.
Kuna jamaa alienda kuomba hela akachape kitabu chake how to make money akaenda kuomba hela bana si akaambiwa akasome hicho kitabu apate hela akakichape.
Talk is cheap but actions are fuckin expensive.
Elimu inabidi ijikite katika vitendo na sio theory tu.
Mana ya elimu ni actions Ila ni kazi mno kufanya kazi. Kuna engineer hajui ratio ya materials kutoa 37MPA
Mkuu,Kwa kusoma reply zako unaonekana mtu mwenye kiburi fulani
Siwezi kucoach ugoro mkuu,Yaani anajiita coach akijibiwa asivyopenda anasema huo ni ugoro! Kwa style hiyo atamcoach mtu kweli😃
Mkuu,80% ya utajiri watu hurithi,20 creativity & self made.
Kwaio tufanyeje ili tuwe matajiri mkuu?S
Sawa sawa lakini kazi ipo ndugu kuwa tajiri au kupatq elimu juu ya jinsi ya matumizi ya pesa haitoshi hata kiduchu hata kuwa na uwezo wa kununua anyway safari njema
Asante mkuu,Umeshavisoma vingapi vikashindwa kukusaidia?
Warren Buffett ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani, lakini kama isingelikuwa tabia yake ya kujisomea vitabu kwa wingi, labda angekuwa anausikia tu utajiri kwenye TV.
Never underestimate the power of books.