Habari
Mfumo wa Kinga wa mwili unahusika na kupambana na vijidudu vya magonjwa kwa njia nyingi, mojawapo ni kuzuia visienee zaidi ya sehemu vilipoingilia. Kwa hiyo kuna matezi maalumu ambayo yanahusika na kuvikamata vijidudu vya magonjwa visipite zaidi ya eneo fulani na kuenea mwili mzima.
Unapoumia mguuni, vijidudu vinaingia hapo kwenye kidonda na vinaanza kuenea kwenda sehemu zingine za mwili, mfumo wa Kinga unavinasa kwenye matezi yaliyoko kwenye nyonga.
Matibabu sio kutibu tezi,Bali kutibu kidonda kwa dawa za kuua vijidudu. Ukienda hospitali utapewa dawa sahihi .