4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 11,613
- 13,543
Wakuu JF, amani ya Bwana ikawe juu yenu kila mmoja kwa imani yake.
Rejea mada tajwa hapo juu.
Mnajua, Mh. Lissu bado yupo mahabusu kwa kesi ya kubumba na wapiga doria kwenye mitandao ya kijamii.
Na ikumbukwe, juzi alitoa wasilisho lake mbele ya Mahakama ya Kisutu kabla ya tarajio la kesi yake kwenda Mahakama Kuu.
Kwenye wasilisho lake, amedokeza mashahidi watatu kati ya mashahidi wake alionao, ambao ni:
Kwa muktadha huu, mpaka sasa kesi ya Mh. Lissu imekuwa na mvuto kuliko hata uchaguzi usemwao upo, ila Mungu wangu ananiambia haupo.
Tafadhali, vyombo vya ulinzi, wazalendo, walindeni mashahidi wa Mh. Lissu kwa wivu mkubwa. Sio muda mrefu watatakiwa kufika Mahakama Kuu na kusimama kizimbani pale, na ni lazima wajibu maswali ya mshtakiwa.
Mungu mwema siku zote.
Thanks.

- Rais wa Jamhuri ya Muungano (ssh),
- Makamu wake,
- Waziri Mkuu.