Uchaguzi 2020 Hai: Freeman Mbowe azindua kampeni kwa kishindo, apokelewa na Mabango, shangwe za Mwamba tuvushe zarindima

Uchaguzi 2020 Hai: Freeman Mbowe azindua kampeni kwa kishindo, apokelewa na Mabango, shangwe za Mwamba tuvushe zarindima

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo Hai Freeman Mbowe , amezindua rasmi kampeni za ubunge na kupokelewa na umati wa wananchi wenye mabango.

Mbowe ambaye kampeni nzima hufanya mikutano mitatu tu ya kuomba kura kutokana na kuaminiwa na wananchi , ambao mara zote humtaka apumzike asubiri kuchaguliwa tu, hata hivyo mikutano hiyo michache ndio humfanya achukue Halmashauri.

FB_IMG_1600893793271.jpg
FB_IMG_1600893783213.jpg
FB_IMG_1600893773647.jpg
 
Cha kufurahisha, mabango yote ukiyachunguza yameandikwa na mtu mmoja.

Mwandiko huwa haujifichi!

Mbowe aache usanii!

Kinachochekesha zaidi, picha zilizopigwa niza pasipoti ili ionekane kuna umati mkubwa!

Tanzania kuna vituko!
 
Mtaumia sana roho zenu za kichawi baada ya mpuuzi wenu mnayemtumia kudhibitiwa na wananchi , na kubwa linakuja , tusilaumiane .

Liwalo na liwe !
Unaleta thread halafu unaanza kujenga hoja zilizo nje ya thread!

Inashangaza kiongozi wa chama kikuu cha upinzani anayegombea ''ubunge'' anaandika mabango na kuyagawa kwa watu ili ionyeshe kuwa wanampa ujumbe wakati ujumbe ameuandika mwenyewe!

Tanzania kuna vituko!
 
Cha kufurahisha, mabango yote ukiyachunguza yameandikwa na mtu mmoja.

Mwandiko huwa haujifichi...
Umeniwahi mkuu maana nilitaka kuuliza kama hao walioshika mabango Wana uwezo wa kuyaandika hayo yanayoonekana kuandikwa, inaonekana kabisa uwezo huo hawana.

Makamanda wanapitia kipindi kigumu Sana ila wanajifariji kwa kujifanya hawaoni yanayowatokea.
 
Umeniwahi mkuu maana nilitaka kuuliza kama hao walioshika mabango Wana uwezo wa kuyaandika hayo yanayoonekana kuandikwa, inaonekana kabisa uwezo huo hawana.

Makamanda wanapitia kipindi kigumu Sana ila wanajifariji kwa kujifanya hawaoni yanayowatokea.
Inashangaza kamanda mkuu anatengeneza mazingira ili aonekane anahitajika wakati anajidanganya yeye mwenyewe!

Hizi sarakasi zake zitaisha baada ya Uchaguzi Mkuu!
 
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo Hai Freeman Mbowe , amezindua rasmi kampeni za ubunge na kupokelewa na umati wa wananchi wenye mabango..
Ajenda ya kwanza aidai damu au mwili wa Ben kwa Wana Moshi popote aendapo
 
Awaulize watu wa Moshi Ben Saanane amepelekwa wapi na awamu ya tano?
 
23 September 2020
Hai, Kilimanjaro
Tanzania

MBOWE Aunguruma JIMBONI kwake HAI, Atangaza VIPAUMBELE vyake, Asema LISSU Atashinda kwa KISHINDO




Mwenyekiti wa CHADEMA kamanda Freeman Mbowe amewahakihishia ushindi wa CHADEMA na huku Rais wa Jamhuri ya Muungano akiwa Tundu Lissu baada ya kupigiwa kura nyingi tarehe 28 Oktiba 2020

Serikali ikishaapishwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 ni Kurudisha umoja wa kitaifa kwa kuleta maridhiano. Hivyo wanaCCM wasiwe na hofu.

Katiba Mpya kama Tume ya Warioba ilivyopendekezwa. Uhuru , Haki na Maendeleo ya Watu.
 
Yaani Chadema hii hii ambayo haina hata jengo la Ofisi kwa miaka 20 ndio wafanye yote hayo kwa muda wa siku 100??

Msitudanganye makamanda.
 
Sherehe za Rais mtarajiwa akiwa katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita Tanzania



Historia ya Mkoa wa Geita

Mkoa wa Geita ulianzishwa rasmi kwa Tangazo la Serikali namba 72 la tarehe 02 Machi, 2012, na kuzinduliwa tarehe 08, Novemba, 2013 na Mheshimiwa DKT Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkoa huu ulitokana na sehemu ya Mikoa ya Mwanza, Kagera na Shinyanga ambapo upande wa Magharibi na Kusini unapakana na Mkoa wa Kagera, upande wa Kusini na Kusini Mashariki unapakana na Mkoa wa Shinyanga na Mwanza kwa upande wa Kaskazini unapakana na Ziwa Victoria.

Umbile la Mkoa na Maeneo ya Utawala

Mkoa huu una eneo au ukubwa wa kilometa za mraba 21,879 (Geita 6,375 km2, Bukombe 6,798 km2, Chato 3,572 km2, Mbogwe 3,684 km2, na Nyang`hwale 1,450 km2), kati ya hizo kilomita za mraba 19,933 niza nchi kavu na kilomita za mraba1,946 ni za maji.

Mkoa una Wilaya tano (5), Majimbo saba (7) ya Uchaguzi, Halmashauri sita (6), Mji mdogo 1, Tarafa23, Kata 122, Vijiji 474, Vitongoji 2,219 na Mitaa 65. Wilaya hizo ni Geita, Nyang‟hwale,Chato, Bukombe na Mbogwe.

Mkoa una jumuisha Halmashauri ya Mji Geita, Halmashauriza Wilaya za Geita, Nyang’hwale, Chato, Bukombe na Mbogwe. Kuanzishwa kwa Mkoa huu kumesaidia kuharakisha upelekaji wa huduma za kijamii, kiuchumi na maendeleo kwa wananchi.

Idadi ya Watu

Kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Mkoa una wakazi wapatao 1,739,530 ambapo wanaume ni 861,055 na wanawake ni 878,475.

Idadi ya Watu Kiwilaya kwa Mwaka 2012

WilayaJumla ya WakaziMEKEWastani watu kwa Kaya Uwiano wa jinsia
Geita807,619400,475407,1445.998
Bukombe224,542110,857113,6855.998
Chato365,127181,365183,7596.099
Mbogwe193,92265,08398,8396.496
Nyang`hwale148,32073,27275,0486.898
Jumla1,739,530861,055878,4756.198
Chanzo: NBS, 2012

Hali yaHewa


Mkoa unapata mvua za kutosha kuanzia milimita 900 hadi 1200 na joto la wastani la nyuzi 22 hadi 30 kwa mwaka. Aidha, Mkoa umekuwa ukipata mvua za vuli katika kipindi cha kuanzia Septemba hadi Desemba na mvua za masika kuanzia mwishoni mwa mwezi Februari hadi Mei. Pia, kipindi cha kiangazi huanza mwanzoni mwa mwezi Juni hadi Septemba kila mwaka na unyevu wa kati ya asilimia 35 na 60.

Shughuli Za Kiuchumi na Pato la Mkoa

Wakazi wa Mkoa wa Geita wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji wa mifugo mbalimbali na nyuki, uvuvi, uchimbaji madini pamoja na biashara ndogo ndogo. Aidha, Sekta ya kilimo ina changia takribani asilimia 70 ya pato la Mkoa wa kati shughuli nyingine za kiuchumi zinachangia asilimia 30. Kwa mujibu wa takwimu kutoka NBS mwaka 2013 zinaonesha kuwa mchango wa Mkoa wa Geita katika pato la taifa umefikia shilingi bilioni 1,584 wakati Pato la mwananchi ni Shilingi 910,824.

Source : History | Geita Region
 
Mungu Tunaomba unabii huu ukapate kutokea.
Haki huinua Taifa.

Tumechoshwa na...
Udikteta.
Mauaji ya watanzania.
Kupotezwa kwa Watu.
Kutekana nknk.

Mungu utuepishie hiki kikombe.
 
Back
Top Bottom