Haji Manara afungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa Miaka 2. Atakiwa pia kulipa faini Tsh milioni 20

Haji Manara afungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa Miaka 2. Atakiwa pia kulipa faini Tsh milioni 20

Angalau apunguze na kizabazabina! Atangaze utalii na makampuni ambako hakutakuwa na matusi
 
naangalia kwa jicho lingine kwamba mpira ni kazi yake kama zilivyo kazi nyingine
 
Huyu jamaa ana backup kubwa sna nyuma yake..hii ni danganya toto kama hamuamin muda ni mwalimu mzuri...vipi akibaki kama shabiki wa yanga??
 
Kwa mashabiki wa Yanga wenye akili, hili jambo tumelipokea kwa furaha mno ila kwa mashabiki wa GSM yanga ni taarifa mbaya kwao. Manara nilikuwa alipokuwa Simba nilimuona hana weledi na hata kuja kwake Yanga kulinichukiza mno
Sure,akawe anamuhudumia kahawa GSM huko........ pamoja na kuisaidia timu Kuna vitu vya kijinga sana anavifanya mojawapo ni kumrudisha Morrison na kumleta Manara
 
Msemaji wa Yanga, Haji Manara amefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 2 na kupigwa faini ya Tsh milioni 20

Manara amekumbwa na adhabu hiyo kutokana na sakata lake na Mwenyekiti wa TFF
View attachment 2298517
====

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfungia Msemaji Klabu ya Yanga, Haji Manara kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 2 na kupigwa faini ya Tsh. milioni 20

Amekutwa na hati kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF, Wallace Karia kwenye fainali ya ASFC kati ya Yanga na Coastal Jijini Arusha
View attachment 2298509
Wanamaanisha nini kusema asijiusishe na mpira. Huwezi mzuia mtu kuzungumzia mpira na kutoa maoni yake kuhusu mpira popote pale duniani. Hiyo ni inbon right.
 
Asipoangalia anaweza kupotea kwenye game mazima ,maana miaka miwili ikiisha atakuja na kiki ipi na generation inabadilika
Pengine asingeweza kufungiwa ila kwa nilivyowasikia mawakili wake siku ile nikajua hawa lazima wamchomeshe

Walikuwa wana hoja ya kijinga ambayo ilikuwa inawageuzia kibao bodi ya ligi kuwa wao ndio wafungiwe

Kwa situation hiyo tu nikajua hiyo ni wrong move na dalili za mtu kupona ni zero

Sasa miaka 2 hiyo labda kama atakuja kuipigia magoti bodi imsamehe kama alivyofanya mwakalebela
 
Tayari habari iko kila mahali juu ya maamuzi ya kamati ya maadili ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kumfungia msemaji wa Yanga kujihusisha na soka ndani/nje ya nchi pamoja na FAINI YA SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI 20

Nataka wanamichezo tujadili kidogo hapa, hii MILIONI 20 inakwenda kwa nani, na inakwenda kufanya nini?

Inakwenda kwa anayedaiwa kutukanwa Rais wa TFF, Bwana Wallace Karia au inakwenda pale TFF

Au hii ni sehemu ya kitega uchumi cha TFF?
Manara.jpeg
 
Wanayanga tuungane tumlipie Manara hii faini aliyotozwa na TFF!
Manara amekuwa mtu mwenye mapenzi mema na timu yetu ametutetea sana, na hata hiki kifungo alichopata ni kwa sababu ya mapenzi yake mema na Club yetu!
Hivyo tupitishe bakuli ndani ya siku chache million 20 tunapata, inalipwa!
Wengine nadhani wana wazo la kukata rufaa, sishauri rufaa kwa sababu ni bora apumzike tu ili akitoka kwenye kifungo awe na adabu pia!
Ila wanayanga tumsuport kwa kumlipia faini kama kumuonyesha fadhila, na pia tuwaombe wanasimba waliokuwa wakimpenda watusaidie katika hili!
Nawasilisha!
Hukumu Ni kifungo na faini kwapamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom