Jana wakati wa mchezo Kati ya Yanga na Prisons, Haji Manara alifanya kitendo kisicho cha kingwana na udhalilishaji kwa jeshi la Magereza kwa kuwaita askari ni wafungwa.
Manara ambae alikuwa anahojiwa na waandishi wa habari huku akiwa amepark gari lake njiani na kuziba njia hiyo magari mengine yasipite, alipotakiwa kulitoa gari lake ili gari la Magereza lipite alimtukana askari huyo na kumuita ni mfungwa hivyo askari wote wa magereza ni wafungwa.
Kitendo hiki kilikuwa cha kidhalilishaji haswa kwani wote tunatambua kuwa kuna utofauti mkubwa Kati ya askari magereza na wafungwa, askari ni muajiriwa wa serikali ambae analinda na kurekebisha wafungwa wakati mfungwa ni mtu aliyepatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu na mahakama.
Jeshi la Magereza linatakiwa kumchukulia hatua Haji ili iwe fundisho kwa watu wengine, kama jeshi litaruhusu udhalilishaji wa namna hii na wakakaa kimya basi ipo siku tutashuhudia udhalilishaji zaidi ukifanywa kwa askari.
Mbona hatuoni askari wa jeshi la polisi, Jwtz wakidhalilishwa Kwanini iwe kwa magereza.
Huyu mtu anapaswa kukamatwa ikiwezekana apelekwe gerezani akaone utofauti wa askari magereza na mfungwa.
View: https://youtu.be/F93mZI980ZU?si=sShG-Fz-jyypfYKV