Haji Manara ni nani hapa Tanzania hadi kuwadhalilisha Askari Magereza na wafungwa bila kuchukuliwa hatua?

Haji Manara ni nani hapa Tanzania hadi kuwadhalilisha Askari Magereza na wafungwa bila kuchukuliwa hatua?

Jana wakati wa mchezo Kati ya Yanga na Prisons, Haji Manara alifanya kitendo kisicho cha kingwana na udhalilishaji kwa jeshi la Magereza kwa kuwaita askari ni wafungwa.

Manara ambae alikuwa anahojiwa na waandishi wa habari huku akiwa amepark gari lake njiani na kuziba njia hiyo magari mengine yasipite, alipotakiwa kulitoa gari lake ili gari la Magereza lipite alimtukana askari huyo na kumuita ni mfungwa hivyo askari wote wa magereza ni wafungwa.

Kitendo hiki kilikuwa cha kidhalilishaji haswa kwani wote tunatambua kuwa kuna utofauti mkubwa Kati ya askari magereza na wafungwa, askari ni muajiriwa wa serikali ambae analinda na kurekebisha wafungwa wakati mfungwa ni mtu aliyepatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu na mahakama.

Jeshi la Magereza linatakiwa kumchukulia hatua Haji ili iwe fundisho kwa watu wengine, kama jeshi litaruhusu udhalilishaji wa namna hii na wakakaa kimya basi ipo siku tutashuhudia udhalilishaji zaidi ukifanywa kwa askari.

Mbona hatuoni askari wa jeshi la polisi, Jwtz wakidhalilishwa Kwanini iwe kwa magereza.

Huyu mtu anapaswa kukamatwa ikiwezekana apelekwe gerezani akaone utofauti wa askari magereza na mfungwa.

View: https://youtu.be/F93mZI980ZU?si=sShG-Fz-jyypfYKV


Haji yupo sahihi
 
Wafungwa wenzio......ni kweli prison kafungwa nne jana kuna tusi gani hapo!?
 
Ila Manara kanihuzunisha sana nategemea muda wowote aje alie lie kuomba msamaha,

Ametumia maneno makali sana kudharirisha jeshi la magereza,

Kuna siku nilisema hapa kama hukuwahi kukaa jela huwezi kuwaheshimu askari magereza ila ukija kukaa wiki tu hata siku ukitoka ukiwaona mtaani utakimbia uvunje mguu,

Nb, Haji asipoangaliwa ipo siku atakuja kuropoka makubwa kila mtu akashika mdomo, nategemea magereza watoe tamko kwa udharirishaji ule ,ikumbukwe huwezi kuwa mfungwa mpaka uhukumiwe nje ya hapo ni mahabusu tu sasa,

Yeye anamuambia askari magereza aende kwa wafungwa wenzie?
Haji manara alishafungwa jela Kwa ubadhilifu wa fedha za ccm mkoa wa Dar es salaam na alivaa uniform kabisa amshukuru Jakaya ndie alimtoa Kwa msamaha
 
Huyu haji manara mdomo wake ni mchafu anajikuta ana mamlaka ya kumtusi na kumdhalilisha yeyote kama kesi ilikuwa na magereza wafungwa wamefuata nini anasahau naye kesho anaweza kuwa mfungwa.

Na hao kituo cha sheria za haki za binadamu hatusikii wakikemea kitu wafungwa wapo kutumikia makosa yao sasa kama haji kakoromewa na magereza ya nini awadhalilishe na wafungwa

Mtu huyu hastahili huruma kwa ule ulemavu wake achukuliwe hatua tu!

Haji Manara ni nani katika nchi hii!
Huyo ni kada wa yanga
 
Hana adabu,kwa sababu anajuana na viongozi ndy anajiona yuko juu
Ila ngoja siku aingie kwenye 18 zao atawajuaaa vzr

Ova
Uoga jamaa hana ndio maana tunamshangaa Sisi watanzania kwa uoga tumezidi kila mtu mwajiriwa wa serikali anaogopeka kama nini! ukute Askari kuna kitu hajakitenda ipasavyo manara kamkasirikia vizuri tu
 
Back
Top Bottom