Haji Manara ni nani hapa Tanzania hadi kuwadhalilisha Askari Magereza na wafungwa bila kuchukuliwa hatua?

Huyo ni zeruzeru, hatuna neno albino kwenye kiswahili.
Ni utata wa lugha yetu ya Kiswahili.
Ni sawa na blind ina maana ya kipofu, lakini kumwita mhusika kwa jina hilo ni unyanyapaa. Anatakiwa aitwe "asiyeona"
Ukitumia kanuni hiyo hiyo ukamwita kiziwi kwa jina la "asiyesikia" hawataki kabisa, wanataka kuitwa kiziwi kwa sababu ukiita "asiyesikia" ina tafsiri kwamba ni mtu ambaye haambiliki yaani kama msumbufu au mtukutu.
 
Acha ujuha, Magereza haina uwezo wa kumchukulia hata raia wa kawaida kwa kitendo kama hicho, hata hivyo Manara ni chawa wa serikali tegemea atajitokeza muda wowote kutubu na kuomba msamaha kwa magereza na serikali.
Kwa hiyo hata wewe huna uwezo wa kumchukulia hatua mtu anayekukebehi/kudhalilisha?
 
Si alimaanisha kua wamefungwa na yanga??
 
Kwa hiyo hata wewe huna uwezo wa kumchukulia hatua mtu anayekukebehi/kudhalilisha?
Sina na pia hakuna raia anayeruhusiwa kumchukulia hatua mtu yeyote, ukiona umedhalilishwa nenda kashitaki police au fungua kesi binafsi ya madai mahakamani.
 
Sina na pia hakuna raia anayeruhusiwa kumchukulia hatua mtu yeyote, ukiona umedhalilishwa nenda kashitaki police au fungua kesi binafsi ya madai mahakamani.
Kumbe shida ipo kwenye lugha.Hicho kitendo cha kumfungulia mtu mashtaka(wewe umeeleza kushtaki police)ndiyo kumchukulia hatua sasa.
 
Embu toka zako uko, mpira haupo hivi wewe. Ilimradi hajatamka tusi, basi hakuna shida kabisa. Mfungwa si ni looser kwa kiswahili?
 
Kumbe shida ipo kwenye lugha.Hicho kitendo cha kumfungulia mtu mashtaka(wewe umeeleza kushtaki police)ndiyo kumchukulia hatua sasa.
Kumshitaki mtu sio kumchukulia hatua, anaweza akakushinda mahakamani halafu wewe uliyeshitaki ukatakiwa ulipie gharama pia..
 
Kumshitaki mtu sio kumchukulia hatua, anaweza akakushinda mahakamani halafu wewe uliyeshitaki ukatakiwa ulipie gharama pia..
Kwa fikra zangu,kabla hatujaendelea kueleza kuhusu kuchukua hatua,turudi kujifunza maana ya kumchukulia mtu hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…