NIMEONA Mzee wetu, Mh. Dkt Kikwete alitokea kupendwa sana na kuaminiwa na watanzania baada ya kutamka ameleta chuma cha pua (Dkt Magufuli) na yeye kukiri watu walimdharau akiwa Rais. Dkt Kikwete alizidi kupata umaarufu ktk utawala wa Dkt Magufuli kwa hekima zake za kutokujisemesha mbovu au kuwa mkimya na kukubaliana na kazi ya Dkt Magufuli. Chuki dhidi ya Dkt Kikwete ilianzia pale alipokiri kuwa eti mafisadi wakishughulikiwa basi nchi haitatawalika (hata IGP Said Mwema alikiri hilo). Basi watu wakasema Dkt Kikwete anakumbatia wezi. Na ktk kipindi chake cha urais ndiyo tulishuhudia ukiukwaji wa haki za binaadamu (ulimboka mpaka leo sijui yupoje unaweza kukuta ni kilema, Daudi Mwangosi aliuawa mchana kweupe, bomu arusha, wizi wa epa, richmond, wafanyakazi hewa, etc). Dkt Magufuli aliposhika hatamu alifanya kazi kurekebisha na ktk kurekebisha huko Dkt Kikwete alisifia pia na watanzania wakaona ana hekima. Ila waliomharibia na wapambe wake akina Makamba, Nape, Rais Samia etc. Wao badala ya kuonesha hudhuni ya msiba walianza na kuonesha kufurahia kifo cha Dkt Magufuli. Kushangilia huku kwa wapambe wake ndiko kumeunganisha doti kuwa Dkt Kikwete anahusika na kifo cha Dkt Magufuli ili aendelee kutawala kupitia Rais Samia. Sharti hawa akina Nape wangejua wanavyoropoka na kufurahia kifo cha Dkt Magufuli wanazidi kumharibia Dkt Kikwete ambaye ni kipenzi cha wote wangenyamaza. Dkt Kikwete ana hekima sana tena sana, ni muadilifu mno, ila ana zungukwa na watu wenye upeo mdogo wa kuchambua mambo na wasiokuwa wavumilivu.