Hakika UKIMWI ni ugonjwa wa maskini. Magic Johnson kaishi nao miaka 32

Hakika UKIMWI ni ugonjwa wa maskini. Magic Johnson kaishi nao miaka 32

Huyu mcheza kikapu maarufu ambaye hivi juzi ametangazwa kuwa bilionea ameishi na ngoma kw miaka 32. Aligundulika na UKIMWI mwaka 1991. Akatangaza hadharani kuwa kaukwaa. Hadi leo mwaka wa 32, akiwa na miaka 64 bado anadunda nao. Tajiri hafi kwa ngoma.

View attachment 2800302
Tatizo NI kukimbilia kuanza kutumia Arv's badala ya kukimbilia kuanza kutumia vyakula vya kuimarisha Kinga,hasahasa vyakula vya vitamin C.
 
Eazy E na Freddy Mercury walikuwa maskini?
Eazy E na Freddie Mercury walikuwa wamejikatia tamaa, wana aibu kutengwa, wameharibika kisaikolojia na matibabu labda hawakuzingatia. Na huwezi jua waliupata lini kabla hawajagunduliwa maana Johnson alitangazwa akiwa na afya tele.

Kuwa na hela pekee haitoshi. Discipline ya afya, lishe, saikolojia kujikubali, genes zako na mengine. Ila kuwa na hela kunachangia pakubwa kumsogeza muathirika.
 
Kwan unadhani zamani sana wala miaka ya 2005 huko ulikuwa kuna sehemu ukiporavkama mbeya yan mwenye ngoma unamjua tu ilikuwa ikikunasa hakuna rangi utaacha kuona, huu ukimwi sikuiz umepungua makali sana aisee yan mgonjwa wa ukimwi anashinda bar wakati kipindi kile mgonjwa wa ukimwi anashinda toi yan mavi hayakai aisee hayakai kabisa yani

Kweli kabisa, siku hizi ukimwi imeisha nguvu ndio maana watu wanadharau. Zamani mtu akiugua kwa ukimwi ilikuwa aibu maana kila mmoja anakuona unavyohangaika na kukondeana. Ilikuwa aibu Sana, na Ukimwi uliogoowa Sana sema ndio hivyo ngono haiepukiki kwa wanadamu.
 
Siyo kuhisi,doctor wake alishautonya umma kuwa jamaa hana cha ngoma wala nini,alikuwa tu anawatimua mabinti wakware waliokuwa wakimsumbua,kuna binti aliwahi kushuka jukwaani na kuvua chupi na kumfuta nayo jasho jamaa alipokuwa anatoka uwanjani kucheza,walimuwinda vilivyo
vizuri kama ni hivyo.. ila njia aliyotumia nadhani kama sio nzuri sana, unajua UKIMWI bhana🤔🤔
 
Eazy E na Freddie Mercury walikuwa wamejikatia tamaa, wana aibu kutengwa, wameharibika kisaikolojia na matibabu labda hawakuzingatia. Na huwezi jua waliupata lini kabla hawajagunduliwa maana Johnson alitangazwa akiwa na afya tele.

Kuwa na hela pekee haitoshi. Discipline ya afya, lishe, saikolojia kujikubali, genes zako na mengine. Ila kuwa na hela kunachangia pakubwa kumsogeza muathirika.

Kweli kabisa. Saikolojia ni muhimu Sana kwenye UKIMWI. Ukiishinda saikolojia kwenye Ngoma mengine utayaweza. Wengi walianza kuwaza kuwa watakufa, wataiacha watoto etc wanapotea.
 
Wenzetu utajiri hawaangalii cash tu. Unaweza ambiwa una dola milioni nane na ukawa hauna pesa ya kula. Hapo wanathaminisha nyumba, boti, mikataba yako nk.

Yani uwe na bilioni mbili na ushee za Mali na ukose pesa ya kula? Hapana. Shida ya Eazy E alikuwa mtumia madawa na ndipo alipoupatia Ngoma kwenye kudungana mashindano. Hivyo alikuwa Teja.
 
Back
Top Bottom