MGOGOHALISI
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 4,555
- 6,773
Mtu wa kupuuzwa ndio unamwandikia makala ndefu hivi kwa id ya uongo?😂😂😂😂😂. Mjibuni polepole kwa kutulia la sivyo atawafumua huo mshono. Sasa hivi ni CCM vs CCM.Ukimsikiliza Polepole utagundua hakuna cha maana sana anachokipigania, malalamiko yake mengi ni kama yanatokana na kuekwa mbali na meza kuu au kutomkubali tu Mwenyekiti wa chama chake. Hayo malalamiko ya ubatili wa utaratibu wa kumpata mgombea ndani ya chama chake ni kivuli cha kujificha na porojo tu.
Amejikanganya mno katika mahojiano yake na Jenerali Ulimwengu, majibu na ufafanuzi wake kwa masuala muhimu yamejaa hadaa sana. Mfano anasema mwenyekiti wa chama chao ana nguvu kuliko rais! Jenerali Ulimwengu amejaribu kumuelewesha kwamba dola ndio ina nguvu kuliko CCM na tatizo linaloipata CCM analolilamikia na ambalo limekuwa tatizo kwa muda wote ni rais wa nchi ambaye ni mkuu wa dola kuwa mwenyekiti wa CCM pia lakini yeye Polepole anabisha na vihoja vya kitoto ilihali kila mtu anajua hivyo ndivyo ilivyo.
Kitu kingine Polepole analalamikia watu kutekwa kunapotokana na uongozi dhaifu na wahuni! Ama kweli Nyani haoni...
Polepole anaamini kwamba chama chake CCM kimekuwa kinafanya vizuri sana wakati wote eti ndio maana kimekuwa "kinapata ridhaa" ya raia kutawala na kumfanya rais wa nchi kuwa mwenyekiti wa chama chao wakati wote na anaomba iendelee kuwa hivyo!
Jenerali Ulimwengu amemuuliza mambo gani hayaendi vizuri yanayomfanya kusema uongozi wa sasa hauko vizuri wakati barabara, madaraja, mabwawa ya umeme, treni, vituo vya afya n.k vinajengwa, Polepole anasema hayo ni mambo yanayoweza kufanyika hata nchi ikiwa katika "autopilot" kwamba kinachokosekana sasa ni uongozi wa kiutumishi unaojali watu! Mimi namuunga mkono katika hili lakini hivi ni kweli Polepole leo ndio amelifahamu hili wakati awamu iliyopita alikuwa akijuvuna na ujenzi wa flyovers na mavietee wapinzani walipokuwa wanaukosa utawala?!