Hakuna cha maana anachokipigania Polepole, hana muelekeo, apuuzwe tu na wapenda mabadiliko halisi

Hakuna cha maana anachokipigania Polepole, hana muelekeo, apuuzwe tu na wapenda mabadiliko halisi

Lakini Katiba ya chama na ya Nchi ilikiukwa kwenye uteuzi wa Samia na hilo ndilo analolipigania achilia mbali mauaji na kupotezwa kwa wapinzani,, kwa akili zako haya si a maana?
 
Jamaa yuko vizuri na Kwa hakika anaongea kama Nyerere. Kwani wewe unayaweza?
Kukosekana wa kumtingisha Mh Rais ndiyo tatizo lenyewe! Ndiyo CHADEMA wakatamani kuwepo reforms!

Rais siyo Mungu!!!! Ni mwanadamu kama wewe! Anakwenda chooni kama wewe!!! Na haja yake inanuka kama yako!!!! Anakosea kama mwanadamu mwingine yeyote!! Na akikosea lazima awepo wa kumkosoa! Na kama ana akili hapaswi kuteka na kuua wakosoaji wake bali atumie ukosoaji kujirekebisha na kuongoza sasa kwa hekima!!

Jinsi ulivyoongea ni kama ng'ombe nyingine ya mama! Hebu jaribu kuwaza nje ya box basi! Maendeleo yetu yataletwa na mimi na wewe! Kama mimi na wewe tukiwaza kama ng'ombe anayesubiriwa kukamuliwa watanzania wanyonge wanaotutegemea hawatoboi!!
 
Ukimsikiliza Polepole utagundua hakuna cha maana sana anachokipigania, malalamiko yake mengi ni kama yanatokana na kuwekwa mbali na meza kuu au kutomkubali tu Mwenyekiti wa chama chake. Hayo malalamiko ya ubatili wa utaratibu wa kumpata mgombea ndani ya chama chake ni kivuli cha kujificha na porojo tu.

Amejikanganya mno katika mahojiano yake na Jenerali Ulimwengu, majibu na ufafanuzi wake kwa masuala muhimu yamejaa hadaa sana. Mfano anasema mwenyekiti wa chama chao ana nguvu kuliko rais! Jenerali Ulimwengu amejaribu kumuelewesha kwamba dola ndio ina nguvu kuliko CCM na tatizo linaloipata CCM analolilamikia na ambalo limekuwa tatizo kwa muda wote ni rais wa nchi ambaye ni mkuu wa dola kuwa mwenyekiti wa CCM pia lakini yeye Polepole anabisha na vihoja vya kitoto ilihali kila mtu anajua hivyo ndivyo ilivyo.

Kitu kingine Polepole analalamikia watu kutekwa kunapotokana na uongozi dhaifu na wahuni! Ama kweli Nyani haoni...

Polepole anaamini kwamba chama chake CCM kimekuwa kinafanya vizuri sana wakati wote eti ndio maana kimekuwa "kinapata ridhaa" ya raia kutawala na kumfanya rais wa nchi kuwa mwenyekiti wa chama chao wakati wote na anaomba iendelee kuwa hivyo!

Jenerali Ulimwengu amemuuliza mambo gani hayaendi vizuri yanayomfanya kusema uongozi wa sasa hauko vizuri wakati barabara, madaraja, mabwawa ya umeme, treni, vituo vya afya n.k vinajengwa, Polepole anasema hayo ni mambo yanayoweza kufanyika hata nchi ikiwa katika "autopilot" kwamba kinachokosekana sasa ni uongozi wa kiutumishi unaojali watu! Mimi namuunga mkono katika hili lakini hivi ni kweli Polepole leo ndio amelifahamu hili wakati awamu iliyopita alikuwa akijuvuna na ujenzi wa flyovers na mavietee wapinzani walipokuwa wanaukosa utawala?!
Hivi ndivyo akili ya mwafrika mjinga Huwa. Ni vyema tukupuuze wewe mjinga kuliko polepope sauti ya watanzania
 
Iwapo Polepole ni shujaa au mzalendo hilo linaweza kuwa jambo la kujadiliwa, lakini jambo lisilo na shaka ni kwamba hoja zake ni za msingi, zenye uzito na mtazamo wa kiuadilifu. Kama kuna anayepinga aliyoyasema, basi na ayakanushe hadharani kwa hoja makini, si kwa mihemko. Ni muhimu kusikiliza kwa umakini speech ya Polepole, amezungumzia masuala yanayohusu Chama chake, CCM, na Serikali inayoundwa na Chama hicho. Jaribuni kubaki katika muktadha wa mjadala wake. Mengine mnayojaribu kuyahusisha ni sawa na kutafuta machungwa chini ya mwembe, hayapo.
mwenendo wa serikali na chama chake ndo wanakiuka utaratibu nma kuharibu chaguzi za nchi - sasa kama wamefika mahala wanaharibu hadi chaguzi zao za ndani , wanatakiwa kujivunia sana jambo hilo

yeye mwenyewe kwenye anayoyalalamikia mwisho anasema "muheshimiwa SSH amefanya kazi nzuri na inaishia hapa 2025" --- kwanini anasema amefanya kazi nzuri?


yeye mwenyewe polepole hoja zake ni za muhemko na kitapeli, na kama awamu miaka hii minne imeyumba - lawama inabidi iende kwenye chama chao kwa ujumla kwa kugoma kuchapa kazi na raisi mpya aliyeapishwa 2021 - maukwaani walikua wanapongeza lakini wakitoka hapo kazi wanalipua makusudi
 
Kitu kingine Polepole analalamikia watu kutekwa kunapotokana na uongozi dhaifu na wahuni! Ama kweli Nyani haoni...
Huyu jamaa Ccm kwake inatangulia kuliko Tanzania.

Haya yote awamu ya 5 aliyakalia kimya.
 
Ukimsikiliza Polepole utagundua hakuna cha maana sana anachokipigania, malalamiko yake mengi ni kama yanatokana na kuwekwa mbali na meza kuu au kutomkubali tu Mwenyekiti wa chama chake. Hayo malalamiko ya ubatili wa utaratibu wa kumpata mgombea ndani ya chama chake ni kivuli cha kujificha na porojo tu.

Amejikanganya mno katika mahojiano yake na Jenerali Ulimwengu, majibu na ufafanuzi wake kwa masuala muhimu yamejaa hadaa sana. Mfano anasema mwenyekiti wa chama chao ana nguvu kuliko rais! Jenerali Ulimwengu amejaribu kumuelewesha kwamba dola ndio ina nguvu kuliko CCM na tatizo linaloipata CCM analolilamikia na ambalo limekuwa tatizo kwa muda wote ni rais wa nchi ambaye ni mkuu wa dola kuwa mwenyekiti wa CCM pia lakini yeye Polepole anabisha na vihoja vya kitoto ilihali kila mtu anajua hivyo ndivyo ilivyo.

Kitu kingine Polepole analalamikia watu kutekwa kunapotokana na uongozi dhaifu na wahuni! Ama kweli Nyani haoni...

Polepole anaamini kwamba chama chake CCM kimekuwa kinafanya vizuri sana wakati wote eti ndio maana kimekuwa "kinapata ridhaa" ya raia kutawala na kumfanya rais wa nchi kuwa mwenyekiti wa chama chao wakati wote na anaomba iendelee kuwa hivyo!

Jenerali Ulimwengu amemuuliza mambo gani hayaendi vizuri yanayomfanya kusema uongozi wa sasa hauko vizuri wakati barabara, madaraja, mabwawa ya umeme, treni, vituo vya afya n.k vinajengwa, Polepole anasema hayo ni mambo yanayoweza kufanyika hata nchi ikiwa katika "autopilot" kwamba kinachokosekana sasa ni uongozi wa kiutumishi unaojali watu! Mimi namuunga mkono katika hili lakini hivi ni kweli Polepole leo ndio amelifahamu hili wakati awamu iliyopita alikuwa akijuvuna na ujenzi wa flyovers na mavietee wapinzani walipokuwa wanaukosa utawala?!
Pumbavu
 
sio tu nataka.

Nakwambia hivi Samia tunamzika mwaka huu,
Kachagua kulukutabu.

Na Tuaenda Kupata kiongozi Mwanaume anayemjua Mungu wa Kweli.

Screenshot hii Kiranga Mwisho wa Mwaka majibu utayapata.
SSH ni raisi ajaye mkuu 😁 --- urais na mambo ya kumjua Mungu wa kweli wapi na wapi mkuu
 
Yoda,

Nitaanza kwa kurejea mahojiano ya Nyerere.

Kuna mahojiano fulani aliyafanya Mwalimu Nyerere na muandishi mmoja wa India anaitwa Saeed Naqvi. Katika mahojiano hayo, kuna swali Saeed Naqvi alimuuliza Nyerere kuhusu uhusiano wake na Nehru (kiongozi wa India), na mambo ambayo Nyerere alipata kujifunza kwa Nehru. I am paraphrasing (link ipo chini kabisa).

Nyerere alisema kuwa, hakupata kujuana sana na Nehru, lakini walikutana wakaongea wakati Nyerere anadai uhuru. Akasema kitu kimoja Nehru alichomuusia Nyerere ni kumwambia "take what you can". Yani Nehru alimwambia Nyerere Wakoloni waki ku offer kitu, hata kama si kikubwa sana, hata kama si kile ulichokitaka, hata kama huwapendi, hata kama kina mapungufu, ilimradi hicho kitu kina advance cause yako, kichukue.

Kwa nini nimerejea ushauri huu wa Nehru kwa Nyerere?

Wapinzani, wanaharakati na wapenda mabadiliko Tanzania wana wakati mgumu sasa. Wanadai uhuru kama alivyodai Nyerere. Angalau wanasema hivyo.

Kwa upande mmoja, hawaupendi uongozi wa Samia na mapungufu yake, wanataka katiba mpya, wanataka mabadiliko. Lakini, kwa upande wa pili, kuna watu wanatokea ndani ya CCM na kuupinga uongozi huu, watu hawa wana makandokando mengi. Kina Gwajima na Polepole hao. Inakuwa vigumu kuwaunga mkono. Wapinzani wanaona kama wakikubali hoja zao fulani, watawapa credit wakati kiukweli hawastahili credit, hawa ni matapeli wa kisiasa tu.

Nimeona Godbkess Lema anamshambulia sana Polepole.

Mimi narejea ushauri wa Nehru kwa Nyerere. Take what you can.

Kuna namna ya kukubaliana na baadhi ya hoja za Polepole na Gwajima, katika hoja fulani, bila ya kumfanya Polepole au Gwajima kuwa hero, kuwa mtume, kuwa shujaa.

Tatizo letu tuna "all or nothing" mindset. Yani tunataka ukimkubali mtu umkubali kwa kila kitu. Halafu hatujui kutenganisha mtu na hoja. Inawezekana nikakubaliana na Polepole kwenye hoja kwamba uteuzi wa Samia una dosari, lakini nisikubaliane naye kwenye hoja kwamba mtu akishakuwa PM, VP na Speaker hafai kuwa rais.

Kuna namna ya kukubaliana na Polepole kwenye hoja kwamba Samia kapitishwa kuwa mgombea kwa ambush na namna ya aibu, bila kujidanganya kwamba Polepole hana ulterior motives zilizo nje ya siasa za principle tu. Angekuwa na siasa za principle angekaa kimya wakati swahiba wake Magufuli anavunja katiba na kuteka watu?

Many a time we focus on the personalities instead of the points.

Let's focus on the points. Kuna points za Polepole zinaweza kusaidia movement ya kudai mabadiliko Tanzania. Take what you can.

Waingereza wanasema even a broken clock can be right twice a day.

Polepole is a charlatan, a Machiavellian politician jockeying for position in the name of principle.

But that does not mean he is useless. That does not mean some of what he says cannot be true and is not useful in furthering activism against the current regime.

Let's argue the points, not the personalities.

Interview ya Nyerere na Saeed Naqvi naiweka hapa kwa marejeo.


View: https://youtu.be/PVdxiBidCoU?si=NKbKbOfTrjJ_D_0V

Very well said!! I will come back to listen and watch the interview of the late, Hon Nyerere and Mr Saeed.
Thank you!
 
Soma vizuri comments, huku kukurupuka kwako ndio ishara mbaya ya kurithishwa ujinga na upumbavu na hao unao wanadi wahedi

Matusi ya nini ndugu? Bila shaka yote uliyoandika yanakuhusu wewe zaidi.

Pambana na hali yako ndugu. Kwamba umtupu tololo hiyo siyo kosa langu!

Looh!
 
Kukosekana wa kumtingisha Mh Rais ndiyo tatizo lenyewe! Ndiyo CHADEMA wakatamani kuwepo reforms!

Rais siyo Mungu!!!! Ni mwanadamu kama wewe! Anakwenda chooni kama wewe!!! Na haja yake inanuka kama yako!!!! Anakosea kama mwanadamu mwingine yeyote!! Na akikosea lazima awepo wa kumkosoa! Na kama ana akili hapaswi kuteka na kuua wakosoaji wake bali atumie ukosoaji kujirekebisha na kuongoza sasa kwa hekima!!

Jinsi ulivyoongea ni kama ng'ombe nyingine ya mama! Hebu jaribu kuwaza nje ya box basi! Maendeleo yetu yataletwa na mimi na wewe! Kama mimi na wewe tukiwaza kama ng'ombe anayesubiriwa kukamuliwa watanzania wanyonge wanaotutegemea hawatoboi!!

Hebu rejea kusoma nilichoandika kumjibu aliyekuwa akimpiga dongo Polepole ambaye hatimaye kukubaliana nami kuwa Polepole yuko vizuri?

Kwani umekurupushwa kutokea chooni ndugu?

ndolelejiUduhe hebu angalia hii ng'ombe Nyerere akisema: "kama huyu, ameokotwa wapi?"

Kwamba umerukia ghafla trenu Kwa mbele hujiui inatoka au inakwenda wapi?

Kiherehere chako na mimba yako kulikoni kutuletea sisi tusiohusika nayo?

Kagombane na mumeo tafadhali wengine hatuhusiki!

Looh!

Bure kabisa!
 
Back
Top Bottom