Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Hakuna anayekataa kuhusu practice na ndio maana vipaji hukuzwa na kuendelezwa. Kuwa na kipaji haina maana huhitaji kufanyia mazoezi au kufanya juhudi.
Hakuna anayekataa practice lakini mimi nakataa kipaji.

#hakuna kipaji.
 
Umechelewa kujua Mkuu, binafsi naamini katika kujaribu/ kufanya mara nyingi hence unakua expert
Kuna inborn talent ambayo unaweza kuwa nayo mwingine asiwe nayo. Kuna kitu unaweza kujaribu kila siku na usoweze, usifanikiwe, ila mwenzako akiamka asubuhi tu anafanya tena bila kutumia nguvu.

Binadamu tuna karama tofauti, talent tofauti. Huwezi kuwa nazo zote, na ili ujue wapi unafit lazima ufanye. Ila sio kila utakachofanya utaweza coz hujaumbwa kuweza kila kitu.
 
Ukipenda kitu hasa tangu utatoni then ukapractice kwa kutumia akili unatisha balaa.
 
Nadharia ya kipaji imekuwepo duniani zaidi ya miaka elfu 10 iliopita, kwahiyo kuna vizazi vingi Tu vimepita na hiyo concept viliikubali.
Kama Tu from nowhere unaanza kubishia uwepo wa nadharia kongwe Kama hiyo, tena ya wazungu basi ujue wewe kipaji chako ni ubishi. Na ilikuchukua miaka mingi kujifunza kuchora Kwa sababu hukuwa na kipaji hicho.
Mwenye kipaji anafanya Jambo linaloonekana gumu na wengine Kwa urahisi na ustadi mkubwa.
Najua utanibishia Kwa sababu hicho ndio kipaji chako.
Thank me for opening your eyes into the talent that God had bestowed in you!!
 
Siku zote hata mnapofanya jambo lolote matokeo (performance) hayawezi kufanana. Kwani darasani kwenu wewe Kila siku ulikuwa unashika nafasi ya mwisho? Kama ulikuwa unapanda na kushuka kwa nini?

Kungekuwa na kipaji basi mtu fulani angekuwa anamaintain position fulani kwa wakati wote pale anapokutana na wasio na kipaji.

Messi ambaye watu wanadai kuwa na kipaji alishakosa penalties dhidi ya magolikipa ambao ambao mnadai kuwa hawana kipaji kama chake.

#hakuna mtu anayezaliwa akiwa na uwezo wa kifunya jambo fulani hapa duniani
 
Unaweza kuta watu wawili wote wanapenda kuwa wanasayansi na mmoja hata akijitahidi Vipi anafeli masomo ya sayansi ila masomo mengine anafanya vizuri wakati huohuo mwingine hakunjui msuli kivilee na bado anafaulu masomo ya sayansi na masomo mengine ufaulu wake ni mdogo.
Utasema nini kinamwezesha huyu asietia jitahada lakini bado anafaulu na Yule anaetoa jitihada na bado zinadunda?
 
Unaweza ukapenda kitu lakini approach unayotumia kuiendea kitu/jambo husika inaweza kukuangusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…