Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Kwahiyo wewe unaamini kama Messi angekuwa ana interest na kufanya mchezo Gymnast au riadha au kuogelea au kulenga shabaha nk nk kwa namna alivyo kwenye soka basi angekuwa na uwezo wa hali ya juu kwenye michezo hiyo kama alionao kwenye soka kwasababu unaamini ni JUHUDI tu imemfikisha hapo?

Kwamba Michael Jackson angezingatia kwa bidii na kuwa Boxer angekuwa na uwezo wa juu kama alivyofanya kwenye muziki?

Kama majibu hapo juu ndio basi utakua SAHIHI
Kama majibu ni hapana basi kila mtu anauwezo wake wa ndani(kipaji) amezaliwa hivyo...... kinachotafutwa ni trigger tu

Mimi naamini kipaji kinadhihirika pale mtu anapo kuja kufanya jambo sahihi kulinga na mazingira yanayo favor uwezo wake wa juu(kipaji)

Unaweza ukawa ni mchoraji mzuri lakini kumbe (ulivyozaliwa)body morphology and other factors zingeweza kukufanya uje kuwa mcheza tenesi mwenye uwezo mkubwa sana lakini mazingira hayakukupa nafasi ya kuujua wala kuucheza mchezo huo

Sioni tatizo la tafsiri
Mwili wako pia unaweza kukusapoti kufanya kitu fulani kwa mfano mtu mwenye misuli anaweza kuwa boxer, mtu mrefu anaweza kuwa mchezaji wa basketball. Wakati mwingine umbile linasaidia ukilitumia vizuri lakini matumizo mazuri ya akili kwenye Kila kitu ndo msingi.

Je, Messi angekuwa na ulemavu wa miguu angekuwa mchezaji wa mpira wa daraja la juu?
 
Mkuu kila mtu duniani anakipaji

Ili kipaji kijidhihirishe ni lazima ufanye hilo jambo ambalo unakipaji nacho.... Usipolifanya itabaki HUNA KIPAJI

Sio kama Messi alizaliwa anajua kucheza mpira...... alijifunza na kuupenda mchezo wenyewe na luckily enough ilikua ndio kipaji chake

Kuna zaidi ya mambo milioni moja mtu anaweza kuwa na kipaji nayo...... issue ni kwamba huwezi jua kipaji chako kipo wapi katika hayo labda mazingira yaku favor kuujua hilo jambo

Kwasababu inawezekana wewe hapo unakipaji kikubwa sana cha jambo fulani lakini Bongo unapoishi hilo jambo halipo
Ukiulizwa unakipaji gani utajua?

Same to Messi, angekua Gaza angekua anaona Soka ni haramu
Mkuu unajichanganya sana.

Mtu kama ana vipaji zaidi ya milioni Moja basi hiyo inamaanisha mtu yeyote anaweza kufanya Kila kitu akiamua.

Wewe una vipaji vingapi hapo ulipo.
 
Mwili wako pia unaweza kukusapoti kufanya kitu fulani kwa mfano mtu mwenye misuli anaweza kuwa boxer, mtu mrefu anaweza kuwa mchezaji wa basketball. Wakati mwingine umbile linasaidia ukilitumia vizuri lakini matumizo mazuri ya akili kwenye Kila kitu ndo msingi.

Je, Messi angekuwa na ulemavu wa miguu angekuwa mchezaji wa mpira wa daraja la juu?
Ndio maana nikasema kipaji ili kijidhihirishe ni lazima mazingira yote yanayo favor kipaji chako yawe sawa

Kama Messi angekuwa kilema maana yake mazingira yasingeweza tena ku favor kipaji chake ..... Pengine angekuwa mtu anayedhani hana kipaji chochote
 
Mkuu hebu define neno kipaji kwanza.
 
Mkuu hebu define neno kipaji kwanza.
Mkuu nime define hapa 👇👇👇
Mkuu kwako wewe unatafsiri kipaji ni nini?

Kimsingi hakuna mtu anayezaliwa na kipaji moja kwa moja...... kila mtu anaweza kujifunza jambo na akaweza kulifanya kwa uzuri tu.
Kipaji ni pale namna mtu anavyoweza kuwa na uwezo wa kulifanya hilo jambo baada ya kulijua kulifanya

Mara nyingi watu wenye vipaji huwa wanajipambanua kwa upekee na ubora wao wa kufanya jambo husika

Kuna mambo mengi yana weza kufanya kipaji kikajidhirisha
Wapo ambao maumbo yao, au viungo vyao, au hormoni zao, mazingira/eneo unaloishi au hata JUHUDI zao zinaweza kuwa favor vipaji vyao

Kiufupi kabisa KIPAJI ni uwezo wa KIPEKEE wa ziada wa kufanya jambo dhidi ya wengine

Hayo maswali ulio uliza...... yes kuna watu wana(upekee wa ziada kufanya)

Kuhusu Messi na Bolt..... wangeweza kuwa na kazi zingine tu kama mamilioni ya Wabrazil na wajamaica wengine wanafanya nje ya Riadha na soka

Mwisho Walokole kukariri Bibilia sio VIPAJI mkuu
 
Kimsingi hakuna mtu anayezaliwa na kipaji
Hili ndo jibu sahihi.

Sasa tumekubaliana kuwa hakuna mtu anayezaliwa na uwezo wa jambo lolote, tunazaliwa sawa lakini tofauti zetu huanza tukishaanza maisha ya hapo duniani.

Pamoja sana.
 
Hili ndo jibu sahihi.

Sasa tumekubaliana kuwa hakuna mtu anayezaliwa na uwezo wa jambo lolote, tunazaliwa sawa lakini tofauti zetu huanza tukishaanza maisha ya hapo duniani.

Pamoja sana.
😂😂😂😂
Hapo mbona hujakamilisha sentensi yangu na umeliacha neno “moja kwa moja” 😂😂😂
 
Mkuu unajichanganya sana.

Mtu kama ana vipaji zaidi ya milioni Moja basi hiyo inamaanisha mtu yeyote anaweza kufanya Kila kitu akiamua.

Wewe una vipaji vingapi hapo ulipo.
Mkuu read between the lines

Namaanisha hapa duniani kuna aina ya vipaji zaidi ya milioni moja
Na katika hivyo vipaji milioni moja mtu anaweza kuwa na kipaji kimojawapo..... issue ni atakutana vipi na kipaji chake?

Ndio nikasema kuna factors nyingi zinaweza kufanya kipaji chako kisijulikane au factors zika ku favor kipaji kikajidhihirisha
 
Mada nzuri sana.

Mtoa mada unawazungumziaje wale watu wanaovumbua vitu ndani ya ujuzi walionao? Mfano...umesema wachezaji wa mpira wamejua kucheza mpira kwa kuwa walikuta mpira ushagunduliwa lkn katika hao wachezaji walivumbua namna ya kufunga magoli kama hatrick n.k jee hao utasema wana kipaji ama vp mana kuna vitu hawajaigiliza bali wamevumbua wao wenyewe
Niliwahi kusoma kwenye gazeti zamani sn kuna mchoraji yeye anachora picha zisizoonekana, yaani hadi utumie
microscope...ni kitu cha kushangaza right! Sasa mtu kama huyu hiki alichonacho sio kipaji kweli? Mana kweli kuchora kakukuta lkn kwa alichokuwa anafanya yeye kakivumbua mwenyewe
Angalia kwa upande wa walimu, unakuta kuna walimu wa somo moja na wapo kwenye field kwa muda unaofanana lkn unakuta mwalimu mmoja anaeleweka sn na wanafunzi kuliko mwengine, jee huyu hatuwezi kusema ana kipaji!?
secretarybird
 
Attachments

  • Screenshot_20241125_172417_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20241125_172417_WhatsApp.jpg
    147.8 KB · Views: 19
Mada nzuri sana.

Mtoa mada unawazungumziaje wale watu wanaovumbua vitu ndani ya ujuzi walionao? Mfano...umesema wachezaji wa mpira wamejua kucheza mpira kwa kuwa walikuta mpira ushagunduliwa lkn katika hao wachezaji walivumbua namna ya kufunga magoli kama hatrick n.k jee hao utasema wana kipaji ama vp mana kuna vitu hawajaigiliza bali wamevumbua wao wenyewe
Niliwahi kusoma kwenye gazeti zamani sn kuna mchoraji yeye anachora picha zisizoonekana, yaani hadi utumie
microscope...ni kitu cha kushangaza right! Sasa mtu kama huyu hiki alichonacho sio kipaji kweli? Mana kweli kuchora kakukuta lkn kwa alichokuwa anafanya yeye kakivumbua mwenyewe
Angalia kwa upande wa walimu, unakuta kuna walimu wa somo moja na wapo kwenye field kwa muda unaofanana lkn unakuta mwalimu mmoja anaeleweka sn na wanafunzi kuliko mwengine, jee huyu hatuwezi kusema ana kipaji!?
secretarybird
Kwanza Asante kwa kuniwekea picha ilyochorwa ya Mama Samia😃.

Kwanza kabisa hoja yangu imejikita katika kukosoa hii maana ya neno kipaji (yaani kuita kipaji something inborn).

Naamini kuwa watoto wote wanapozaliwa wanakuwa na uwezo sawa lakini mazingira wanayokulia, malezi, interests, maumbile/body structure kwa mfano Urefu, ufupi, unene, uwembamba na factors zinginezo ndizo zinamfanya mtu mmoja kuwa na uwezo/kuwa na ufanisi katika ufanyaji wa jambo fulani kuliko mtu mwingine.

Kwa mfano umbo fupi la mesi linamruhusu kupiga chenga za haraka haraka kuliko Ronaldo. Pia ukipenda kitu (ukiwa interested na kitu fulani) akili yako itaanza kukifikiria kile kitu karibia Kila wakati jambo ambalo linafanya uanze kufikiria namna bora zaidi ya kufanya kile kitu, kwa mfano baada ya mtu kuokoka na kuanza kuwa na matamanio ya kuanzisha kanisa anaweza akakariri mistara ya bibilia hata akaiweka bibila yote kichwani na huyo huyo mtu alishindwa kukariri definition ya Biology au formula za hesabu akafeli kwa sababu hana interest nazo.

Angel Nylon kama umeshawahi kukutana na mwanfunzi kipofu utakubaliana na mimi kuwa mwanfunzi kipofu ana uwezo mkubwa sana wa kukariri yale yanayofundishwa na mwalimu wake pia mwanfunzi kipofu anaweza akakariri sauti yako hata ukiongea naye mara Moja halafu ukaja kuongea naye tena baada ya miezi kadhaa anaweza kukutambua, na hii siyo kipaji bali ni uwezo alioibua kama alternative baada ya kukosaa uwezo wa kuona, huu ni uwezo ambao Kila mtu anao ila shida ni kwamba tuna alternatives ndiyo maana tunaona kama vile hatunao.

Halafu pia napingana na ile kauli inayosema some teachers are born and some are made. Mara nyingi mwalimu ambaye anaweza kufanya vizuri zaidi ni yule anayekuwa anaipenda kazi hiyo tangu zamani toka moyoni mwake yaani ni yule ambaye akilala anauota ualimu kiasi kwamba ana imagine kama anafundisha hata akiwa usingizi, akiwa anatembea na akiwa popote pale na ndo maana anaweza akajiundia teaching approaches nzuri za kufundishwa, sasa huyu watu wanamwita teacher by born lakini kiuhalisia hakuzaliwa na ualimu bali several factors zilimshawishi kupenda kazi hiyo.

Pia kuna huyu mwalimu ambaye aliuvamia ualimu baada ya kukosaa kusoma kozi azipendazo, sasa huyu anaweza kuwa na contents lakini kuzi-deliver inakuwa shida maana kazi yenyewe haipendi ndo maana unakuta mwalimu mwenye masters anafelisha lakini mwalimu mwenye diploma anafaulisha wanafunzi.

Sasa Angel Nylon nakuuliza kwa nini huyu mwalimu mwenye diploma (mwenye elimu ndogo) anafaulisha wanafunzi kuliko huyu mwenye masters (aliyefaulu sana). Yaani kwa nini huyu mwalimu anayefaulisha wanafunzi hana elimu kumzidi huyu anayefelisha, kama ana kipaji cha ualimu si angekuwa na ufaulu mkubwa.

Ni hayo!
 
Habari ya muda Great Thinkers!!

Wakuu nimegundua kuwa hakuna kitu kinachoitwa kipaji (talent) katika Dunia hii.

Wazungu hupenda kutumia dhana au neno kipaji wakimaanisha mtu kuzaliwa akiwa tayari ana uwezo wa kufanya kitu fulani kwa mfano kucheza mpira, kuimba, kukimbia. Wamefanya na wanafanya hivi ili tujikatie tamaa ya kufanya mambo makubwa kama gunduzi za kisayansi na mengine mengi.

Binafsi nilishawahi kujaribu kukatishwa tamaa na jamaa mmoja, hii ni mara baada ya kuona mimi najaribu kuchora. Jamaa aliniambia wewe wala usihangaike maana huna kipaji cha kuchora,maneno haya yalininipa hasira ya kupambana zaidai ndiyo maana leo hii mimi ni miongoni mwa wachoraji wakubwa hapa Tanzania (hii ni mara baada ya kugundua kuwa hukuna kipaji duniani)

Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa tayari na uwezo wa kufanya jambo fulani (kipaji), watu wote wanazaliwa sawa lakini namna ya kufikiria ndiyo humfanya moja afanye jambo fulani kwa urahisi kuliko mwingine.

Hebu jiulize haya maswali na uyatafakari kwa kina.

-Je, kama mpira wa miguu usingegunduliwa Messi angekuwa na kipaji cha nini?
-Kusingekuwa na mchezo wa riadha Usain Bolt angekuwa na kipaji gani.
-Je, Kuna kipaji cha kujamiiana?
-Kuna kipaji cha kula?
-Kuna kipaji cha kunywa pombe?
-kwa nini walokole wana uwezo wa kukariri mistari ya bibilia na kuichambua lakini wanashindwa kukariri quotations kutoka kwenye vitabu vya fasihi wakati yote ni maandishi?

Cc Monetary doctor Poor Brain uzuri_hatujuani.

Bye bye 👋.
Kabla hujajiuliza hayo maswali ya kijinga ungeanza kujiuliza kwanini uwezo wa kufikiria unatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine
 
Kabla hujajiuliza hayo maswali ya kijinga ungeanza kujiuliza kwanini uwezo wa kufikiria unatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine
Jitihada na uzembe.

Changamoto zikikukumba uanshughilisha akili yako.
 
Unachora Rada Kama wezi au unachora Nini ?

Unazungumziaje Jambo ambalo wewe unatumia miaka kumi kulielewa na miaka Saba kulimudu huku Kuna mwenzio anatumia wiki.
Kwa kukazia comment yako tena anaenda extra miles katika ufanisi kwa maana ya kwamba may be alifundishwa moja mpaka mbili yeye akaweza kugundua tatu mpaka kumi hicho siyo kipaji?
 
Back
Top Bottom