Ramesses II
JF-Expert Member
- Sep 29, 2013
- 4,217
- 5,907
Vipaji vinaweza kuwepo. lakini msisahau pia kuna wakati mazingira yanaweza kuidanganya jamii kuwa fulani ana kipaji na fulani hana. Kumbe fursa ya mazingira tu yamemfanya mwingine kuonekana ana kipaji na mwingine hana. Mfano mzuri kwa Tanzania kidogo ni ngumu sana kujua vipaji vya watoto. Kuna shule zinaitwa za vipaji maalum lakini kimsingi ni shule za wachache wenye vipaji maalum na walio wengine waliopata fursa ya mazingira mazuri na wao wakaonekana wana vipaji maalum kumbe hawana. Ndo maana utaona vijana wanaenda shule form one kwa kigezo cha ufaulu wa marks lakini kidacho cha nne ufaulu huo wanapitwa na waliokuwa shule za kawaida.
Lakini pia hizi shule zetu zinazoitwa za vijapi hazijaweza kutusaidia kama Taifa kuwa hata na Ubunifu ili kuikwamua nchi. Hapa kuna mawili, ni ama tunaowapeleka kule siyo watu sahihi au sisi wenyewe kama nchi hatujatoa fursa ya kimazingira kuweza kutambua vipaji vya vijana wetu hawa au hatujaweka mazingira wezeshi hivi vipaji kuonekana na kuwa msaada kwa nchi.