secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 23,984
- 51,055
- Thread starter
- #241
Havipo.Vipaji vipo
Havipo.Vipaji vipo
itabidi acheze soka la magongo kwa hali yake.Aise we unanifurahisha sana.
Haya tukigundua kuwa ana kipaji cha mpira tutamsaidiaje ili aendeleze kipaji chake maana mnasema kipaji kukivumbuliwa kinaweza kuendelezwa kirahisi.
Changia madaNiambie.
Mkuu ukifikiria kwa kina utakubakiana na mimi kuwa hakina kitu kinachoitwa kipaji katika Dunia.itabidi acheze soka la magongo kwa hali yake.
Mkuu hii comment yako nitaihifadhi kabisa ili niitumie kuwaelewesha vijana kama akina NomadixUna hoja usikilizwe na pia kueleweka inahitaji mtu atafakari kwa kina.
1.Ili mtu aweze kufanya kitu vizuri zaidi sharti hicho kitu kimvutie.
Ndio maana kuna ule msemo usemao ukitaka kufanikiwa penda unachofanya,hiyo hutoa uwezo wa kuwekeza mawazo yako hapo na resources zote hivyo itaonekana ni kipaji chako mwisho wa siku.
2.Kwahiyo mtoto anapozaliwa akianza kukua hujikuta amependa jambo fulani ambalo akili yako hu concentrate upande huo na analifanya vyema,ila kwa mwingine analipenda lakiniakili yake inashindwa ku focus vzr.
3.Baada ya kupenda jambo hilo ili uzidi kuwa mzuri lazima uliendeleze,tunasikia vipaji huendelezwa ili ujenge uzoefu mwingi na kumaster hilo jambo
TAKEAWAY
Ili kutengeneza kipaji vitu hivi ni muhimu
1.Penda unachofanya/kutoka moyoni.
2.Focus kiakili na kiroho.
3.Practice mara nyingi.
Zingatia: Post#221Mkuu ukifikiria kwa kina utakubakiana na mimi kuwa hakina kitu kinachoitwa kipaji katika Dunia.
Hakuna anaye zaliwa anajua.Kwa mfano ukizaliwa kwenye jamii isiyojua chochote kuhusu mchezo wa mpira wa miguu (hawajui kama Kuna mchezo huo) na mtoto mwenye kipaji cha mpira akazaliwa katika jamii hiyo, je naye atakuwa anaufikiria mpira ilihali hajawahi kuuona wala kuusikia?
Cc Infropreneur
Kipaji ni ule uwezo wa kuelewa au kufanya jambo/kitu fulani kwa wepesi na ufanisi zaidi kuliko wengine.Mimi nimeelezea maisha ya masomo nilisoma na Zawadi Mdoe. Huyu jamaa alikuwa haandiki notes akimsikiliza mwalimu imetoka. Baba na mama yake walikuwa maprofesa SUA,alikuwa top 3 form four na form six. Kwa sasa ni Profesor Norway. Hii inaonesha mfumo wa elimu ni mbovu maana sio kila mtu ana kipaji cha elimu. Huku ujerumani kuna wanaosoma masomo ya utafiti() na kuna amabao wanasoma masomo ya vitendo(Beruf Schule). Na wanawatenga kabisa
Wewe utaendelea kubisha mimi naamini na nimeshuhudia kila mtu anazaliwa na kipaji. Na inabidi ujaribu kila kitu kujua kipaji chako. Ndio maana kila mtu ana urahisi wa kufanya jambo A na ugumu wa kufanya jambo B. Kipaji ni pale mtu anapokuwa na urahisi wa kufanya au kutekeleza fani fulani. Kuna kazi hata ukaze vipi kama hauna kipaji hauwezi kutoboa. Kazi kama Architect mwenye kipaji anakuwa juu kuliko wewe. Na ndio maana huku Ulaya watoto wanaruhusiwa kujaribu kila kitu ili wajue kipaji chao mapema.
Mkuu umeongea facts,na hicho ndicho nimeelezea huko juu,lkn bird 🐦 mi sijaelewa anataka majibu gani,naona kakamaa na msimamo wake!!!,HIvi vitu vinachanganya lakin twende taratibu kidogo.
Kitendo cha kujiongeza kwenye jambo fulani na ukawa mwepesi kuki master hiyo ni talent, kwa maana huo ni uwezo wako wa asili ambao upo nao kwenye jambo hilo.
Pia kumbuka kila mtu ana jambo lake ambalo ni mwepesi na hodari wa ku-catch(talent).
Tukija kwenye Skill/Ujuzi, Hali hii inakuja baada ya desire kutamalaki, yaani unajikuta unapenda jambo fulani hivyo itapelekea kulifanya mara kwa mara na mwishowe kubobea kabisa katika jambo hilo,
Skill haijalishi kama una kipaji au hauna isipokuwa mtu mwenye talent/kipaji na akawa na skill/ujuzi anakuwa ahead ya wewe mwenye skill/ujuzi peke yake.
Labda tupate mfano kidogo.
Darasani wanafunzi wote wanasoma kwa bidii, Lakin watatokea wanafunzi wachache ambao hao wanakuwa moto, yaani ni vipanga balaa na ingawa wanafunzi wote wanafundishwa na mwalimu mmoja.
Hapo pia kuna wanafunzi wengine ambao nao wanafosi kusoma kila siku yaani wanajikuta wanapenda kusoma ila ndo hivyo kitabu kinawakataa, sasa hawa wakiendelea kukaza, yaani kusoma na kusoma zaidi ndo wanakuwa nao hodari darasani.
Hapa tunapata wanafunzi wa aina mbili, mmoja hatumii nguvu kubwa kusoma ila ni kipanga, na mwengine anatumia nguvu kubwa kusoma ila nae ni kipanga vile vile.
Mfano no 2.
Katika hao vipanga darasani kuna wengine ndo vilaza kabisa yaani washajikatia tamaa na masomo yenyewe.
Ila upande wa pili wa shilingi hao jamaa wanapiga mpira balaa yaani shule nzima hakuna, hao hata wasipofanya mazoezi ndani ya week nzima ikija mechi wanakiwasha ile ile.
Kwa kifupi mzunguko unabaki kuwa ni hivyo hivyo kwa watu wote.
Kuna ambao wanelewa kwa haraka mambo ya elimu . Na kuna ambao wanaelewa haraka kwenye ufundi. Na kuna ambao wanaelewa haraka kwenye sanaa na michezo. Hapo ndipo unakuja kujua maana ya kipaji.Kipaji ni ule uwezo wa kuelewa au kufanya jambo/kitu fulani kwa wepesi na ufanisi zaidi kuliko wengine.
Binadamu wote tunazaliwa sawa. Bila ufahamu wala kipaji chochote kile.
Utofauti huja pale tunapoanza kujifunza mambo na vitu.
Hapa ndio kuna ambao huelewa kwa haraka zaidi na kufanya mambo kwa kiwango cha juu zaidi, na wengine huelewa polepole na kufanya mambo kwa kiwango cha wastani au kidogo.
Full stop!Hakuna anaye zaliwa anajua.
Wote tunazaliwa tukiwa hatujui chochote.
Utofauti unakuja pale tunapoanza kujifunza vitu, kuna ambao huelewa kwa haraka zaidi. Na wengine huelewa polepole.
Hakuna anayezaliwa na kipaji cha aina yeyote ile. Isipokuwa utofauti huja pale tunapoanza kujifunza mambo.
Ninachoendelea kuikataa ni kuwa hakuna mtu anayezaliwa na uwezo wa kufanya kitu.Mkuu umeongea facts,na hicho ndicho nimeelezea huko juu,lkn bird 🐦 mi sijaelewa anataka majibu gani,naona kakamaa na msimamo wake!!!,
Anatakiwa atambue kwamba ubongo wa binadamu una pande mbili au umegawanyika mara mbili,kuna upande wa akili inayofikika na upande wa akili isiyofikika ( subconscious mind),, conscious mind ndo upokea dhamili, yaani kile tunachojifunza aidha kwa kuona ,kusikia,kuhisi nk,kutokana na mazingira tulimo na kufundishwa mfano shuleni nk.
Sasa subconscious mind huko ndo kuna kipaji,,unapolala ukaota jambo hapo unakuwa umeamsha upande huu, hili kufanyia na hilo jambo likawa dhamili lazima ihusike ili kupata data,kwa lengo la kupata ufanisi katika jambo husika,,mfano watu wawili wanaweza kuwa wote wanaelimu sawa,lkn katika utendaji wa kazi mmoja akawa na ufanisi kuliko mwenzake,,je wajua kinawatofatisha ni nini ?,ni kipaji tu..ndipo hapo unapokuta mwenye kipaji, kwingine wanaita wito,huyu mwenye wito ufanya kazi kwa bidii na kuridhika na furaha tele,lkn asiye na wito ufanya kazi ini mradi tu siku ipite,ni kama vile analazimishwa kufanya kazi afanyayo.
Sisi tunachokikataa siyo kuuelewa haraka, tunachokikataa ni madai kuwa mtu huzaliwa tayari akiwa na uwezo wa kufanya kitu au jambo fulani ambapo nyinyi mnasema ni kipaji.Kuna ambao wanelewa kwa haraka mambo ya elimu . Na kuna ambao wanaelewa haraka kwenye ufundi. Na kuna ambao wanaelewa haraka kwenye sanaa na michezo. Hapo ndipo unakuja kujua maana ya kipaji.
Neno kipaji ndo linatuharibu sisi waafrika, linatuaminisha kuwa watu fulani wamezaliwa na uwezo fulani na sisi hatuwezi kitu funi kwa sababu hatujazaliwa na uwezo wa kitu hicho.Siwezi kusema chochote ila nadhani wewe huna kipaji nikushauli tu kwamba binadamu ana akili sana lakini binadamu huyo huyo ni mvivu wa kufikiri.
Binadamu akipata changamoto huamsha ubongo kutafuta suluhu kama hana files alizo save kuhusiana na changamoto aliyo nayo haiwezi kulitatua,.(kupata suluhisho)
Huko kuelewa haraka ndio talent yenyewe, nilichogundua you guys mnachanganya talent na skill.Hakuna anaye zaliwa anajua.
Wote tunazaliwa tukiwa hatujui chochote.
Utofauti unakuja pale tunapoanza kujifunza vitu, kuna ambao huelewa kwa haraka zaidi. Na wengine huelewa polepole.
Hakuna anayezaliwa na kipaji cha aina yeyote ile. Isipokuwa utofauti huja pale tunapoanza kujifunza mambo.
Sasa mbona ana vipaji vingi wakati tulikubaliana kuwa kipaji huwa ni kimoja tu😀.Mkuu kipaji hakuna?. Okay twende na Leonardo Da Vinci ambae alikuwa mtihani bahati sana kama wewe.
LEONARDO DA VINCI
Leonardo Da Vinci alikuwa Anatomist, Architect, Astronomer, Botanist, Cartographer, Engineer, Geologist, Hydro-dynamasist, Mathematician, Musician, Theater producer, Inventor. Sasa Noma zaidi ni Jamaa alikuwa anaweza kuchora picha na mkono wa kushoto alafu mkono wa kulia anatandika advanced calculus na abstract algebra kwao wakati mmoja, wait a minute, kama hujaelewa jamaa alikuwa anaweza kwao mkono wa kulia ukawa anapiga mtihani wa physics advance alafu mkono wa kushoto anapiga mtihani wa wa pure mathematics. Mkuu imagine jamaa maandishi yakee yote aliyaandika kwao mirror scripts na aliandika kutoka kulia kwenda kushoto badala ya kushoto kwenda kulia na ili uweze kusoma yale maandishi lazima umulike kwenye kiyoo.. Mkuu bado tu hamna kipaji?.... Mwaka 1994 Bil Gates alinunua notebook ya jamaa kwa dola milion 30 ilokuwa na madini ya ugunduzi wa vitu mbali mbali, unaweza ukaimagine bilion 70 ya mwaka 94 ni shs ngapi ya leo?...Mkuu acha kabisa.
Yaaah alifanya hivyo vyote, jamaa ndio inasemekana jitu lenye akili nyingi kuwah kutokea ujue ni hatari sana mtu mkono wa kushoto unachora na wakulia unatandika equation za physics. We kamsome alafu utakuja na majibuSasa mbona ana vipaji vingi wakati tulikubaliana kuwa kipaji huwa ni kimoja tu😀.
Alizaliwa na uwezo wa kufanya hivyo vitu vyote ulivyovitaja?