Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Kwa nini?
Lamine Yamal ana nini?

Ningerudisha umri nyuma Ningefanya vema kuliko anavyofanya Yamal.
Umeanza majisifu sasa. Vipaji vipo na watu wanazaliwa navyo. Ukiwa na kipaji na ukawa na commitment kubwa, nakuhakikishia asiye na hicho kipaji hawezi kukufikia kamwe. Tatizo wengi wenye vipaji huwa wanakosa utayari na kujitoa kwa dhati (willingness and determination)
 
Mkuu kwani neno 'kipaji' kwako unalielewaje?

Hivi uanelewa tofauti ya hobby na kipaji?

Nikuulize swali dogo, mnapokuwa vijana:
Kwanini mmoja apende udereva, mwingine apende ualimu, mwingineapende uhandisi nk nk na kila mmoja aione kazi anayoifanya ama kuipenda mwenzake, yeye haiwezi?

Embu fikiria mara mbili mbili katika kuchambua majibu ya utafiti wako huo.

Wewe kung'ang'ania sanaa ya uchoraji mpaka kuwa mahiri ni kipaji chako hicho, mwingine hawezi hata akifundishwa, maana anakuwa hapendi toka rohoni mwake.
Kipaji wanasema ni uwezo wa asili ambao mtu huzaliwa nao ambapo uwezo huo humfanya mtu kufanya kitu fulani kwa ubora.

Hapo kwenye uwezo wa kuzaliwa nao/ uwezo wa asili ndipo ninapopata ukakasi kwa sababu naamini hakuna mtu anayezaliwa akiwa na uwezo wa kufanya kitu fulani.

Mtu anaweza kupenda udereva au ualimu kwa sababu Kuna kitu kinamsukuma kufanya kile kitu, pia si kitu anachokipenda mtu anaweza kukifanya kwa ubora mkubwa na hii inatokana kutotuliza akili yako pale unapokifanya kitu husika.
 
Umeanza majisifu sasa. Vipaji vipo na watu wanazaliwa navyo. Ukiwa na kipaji na ukawa na commitment kubwa, nakuhakikishia asiye na hicho kipaji hawezi kukufikia kamwe. Tatizo wengi wenye vipaji huwa wanakosa utayari na kujitoa kwa dhati (willingness and determination)
Hao wasio na kipaji na kukosa utayari wewe uewajuaje kama wana vipaji? Nipe na mfano.
 
Mkuu kuna Talent na Skill/ Kipaji na Ujuzi,
Kipaji hakifundishwi, ni uwezo wa asili wa kuona au kufanya jambo fulani kwa namna fulani.

Ujuzi ni kitu ambacho tumekuwa wazuri na tunapenda kufanya lakini tumefundishwa kwa namna moja au nyengine.

Na kuna Desire/Tamaa ya jambo fulani,
Tamaa ni muhimu zaidi kuliko talanta. Unaweza usijione wewe ni bora katika jambo fulani lakini ukiwa na hamu ya kuendelea na kuendelea kujifunza unaweza kufikia chochote.

Me naona Desire is more important than talent.
 
Habari ya muda Great Thinkers!!

Wakuu nimegundua kuwa hakuna kitu kinachoitwa kipaji (talent) katika Dunia hii.

Wazungu hupenda kutumia dhana au neno kipaji wakimaanisha mtu kuzaliwa akiwa tayari ana uwezo wa kufanya kitu fulani kwa mfano kucheza mpira, kuimba, kukimbia. Wamefanya na wanafanya hivi ili tujikatie tamaa ya kufanya mambo makubwa kama gunduzi za kisayansi na mengine mengi.

Binafsi nilishawahi kujaribu kukatishwa tamaa na jamaa mmoja, hii ni mara baada ya kuona mimi najaribu kuchora. Jamaa aliniambia wewe wala usihangaike maana huna kipaji cha kuchora,maneno haya yalininipa hasira ya kupambana zaidai ndiyo maana leo hii mimi ni miongoni mwa wachoraji wakubwa hapa Tanzania (hii ni mara baada ya kugundua kuwa hukuna kipaji duniani)

Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa tayari na uwezo wa kufanya jambo fulani (kipaji), watu wote wanazaliwa sawa lakini namna ya kufikiria ndiyo humfanya moja afanye jambo fulani kwa urahisi kuliko mwingine.

Hebu jiulize haya maswali na uyatafakari kwa kina.

-Je, kama mpira wa miguu usingegunduliwa Messi angekuwa na kipaji cha nini?
-Kusingekuwa na mchezo wa riadha Usain Bolt angekuwa na kipaji gani.
-Je, Kuna kipaji cha kujamiiana?
-Kuna kipaji cha kula?
-Kuna kipaji cha kunywa pombe?
-kwa nini walokole wana uwezo wa kukariri mistari ya bibilia na kuichambua lakini wanashindwa kukariri quotations kutoka kwenye vitabu vya fasihi wakati yote ni maandishi?

Cc Monetary doctor Poor Brain uzuri_hatujuani.

Bye bye 👋.
Hoja yako bado haija prove existence ya kipaji ipo au haipo.

Kipaji kipo ila , is why tuna mathematicians, scientits na watu wanao excel katika field mbali mbali

Kuna watu wanafanya baadhi ya shughuli effortless, as if they have figure it out, while wengine waki struggle au kutumia nguvu kubwa

Kipaji ni zawad ambayo mtu anayo, anaweza fanya jambo fulani kwa urahisi sana na kwa usahihi kuliko mtu mwingine. Na si wote wanakuja navyo
 
mtu anazaliwa na kipaji bhana tusidanganyane na ndomana tuna majinias wakukalili darasani,tuna watu walotumia uwezo wao tuka pata,moto,umeme,ndege,magari,piki piki ,intanet n.k, afu wakafa zao na hakuna mtu wakuziba nafasi zao kilichobaki dunia imebaki kujifunza falsafa zao ili ielimike...kwa kuongezea tu mtu mwenye kipaji sio rahis kufeli maishani maana ana plan b nyingi.maana kipaji ni neema anayozaliwa nayo mtu,unashangaa mtu unasoma nae we unajitesa ye nikupiga kelele tu ila akiingia class anawaburuza wote,mfno mimi tangia nizaliwe sijawahi kuferi na hata nikiferi nasimama tena kwanjia ya ajabu yaani linakuja wazo la ajabu ukilifanyia kaz linaleta matokeo ya ajabu yaani na plan b kwa wing .kiufupi huwa hata mi najishangaa,nilijiona mjanja nikafanya utafiti nikagundua ninema tu,kwahiyo kama umefanikiwa usidharau watu maana umebebwa na neema hunautofauti na hao wengine ikiondoka neema hiyo huna chako
 
Jamie Vardy $ Shaggy nao hawakuwa na vipaji kwa majukumu yao ya awali kabla ya kuwa Football Striker na Reggae Dance Singer?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Screenshot_2025-05-14-11-12-40-65_680d03679600f7af0b4c700c6b270fe7.jpg
Screenshot_2025-05-14-11-22-47-07_680d03679600f7af0b4c700c6b270fe7.jpg
 
Habari ya muda Great Thinkers!!

Wakuu nimegundua kuwa hakuna kitu kinachoitwa kipaji (talent) katika Dunia hii.

Wazungu hupenda kutumia dhana au neno kipaji wakimaanisha mtu kuzaliwa akiwa tayari ana uwezo wa kufanya kitu fulani kwa mfano kucheza mpira, kuimba, kukimbia. Wamefanya na wanafanya hivi ili tujikatie tamaa ya kufanya mambo makubwa kama gunduzi za kisayansi na mengine mengi.

Binafsi nilishawahi kujaribu kukatishwa tamaa na jamaa mmoja, hii ni mara baada ya kuona mimi najaribu kuchora. Jamaa aliniambia wewe wala usihangaike maana huna kipaji cha kuchora,maneno haya yalininipa hasira ya kupambana zaidai ndiyo maana leo hii mimi ni miongoni mwa wachoraji wakubwa hapa Tanzania (hii ni mara baada ya kugundua kuwa hukuna kipaji duniani)

Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa tayari na uwezo wa kufanya jambo fulani (kipaji), watu wote wanazaliwa sawa lakini namna ya kufikiria ndiyo humfanya moja afanye jambo fulani kwa urahisi kuliko mwingine.

Hebu jiulize haya maswali na uyatafakari kwa kina.

-Je, kama mpira wa miguu usingegunduliwa Messi angekuwa na kipaji cha nini?
-Kusingekuwa na mchezo wa riadha Usain Bolt angekuwa na kipaji gani.
-Je, Kuna kipaji cha kujamiiana?
-Kuna kipaji cha kula?
-Kuna kipaji cha kunywa pombe?
-kwa nini walokole wana uwezo wa kukariri mistari ya bibilia na kuichambua lakini wanashindwa kukariri quotations kutoka kwenye vitabu vya fasihi wakati yote ni maandishi?

Cc Monetary doctor Poor Brain uzuri_hatujuani.

Bye bye 👋.
1747211391268.jpeg

Hicho ni kipaji cha kuchonga au sio. Hiyo sanamu ilichongwa miaka 800 iliyopita.
 
Hoja yangu ni kuwa watu wanazaliwa wakiwa wanafanana yaani hakuna mtu anayezaliwa akiwa na uwezo wa kufanya kitu fulani.
Kila mtu anazaliwa akiwa na uwezo wa asili wa kufanya mambo kwa ustadi wa kipekee unaomtofautisha na watu wengine. Uwezo huo ndio unaitwa Kipaji.

Kipaji kina kawaida ya kutoa msukumo mkali sana wa kutenda yahusianayo na Kipaji husika. Kwa mfano, kitendo cha wewe kuanza kutafakari kuhusu michoro(uchoraji) kinatokana na msukumo unaosababishwa na Kipaji cha uchoraji kilichopo ndani yako. Asiye na Kipaji cha uchoraji hawezi kufikirifikiri kuhusu michoro(uchoraji) kama ufanyavyo wewe(Hana huo msukumo ndani yake)

Hata hivyo Kipaji ni kama Mbegu kinapaswa kumwagiliwa(kuendelezwa) ili kioneshe ubora wake vinginevyo hufifia.
 
Mkuu kuna Talent na Skill/ Kipaji na Ujuzi,
Kipaji hakifundishwi, ni uwezo wa asili wa kuona au kufanya jambo fulani kwa namna fulani.

Ujuzi ni kitu ambacho tumekuwa wazuri na tunapenda kufanya lakini tumefundishwa kwa namna moja au nyengine.

Na kuna Desire/Tamaa ya jambo fulani,
Tamaa ni muhimu zaidi kuliko talanta. Unaweza usijione wewe ni bora katika jambo fulani lakini ukiwa na hamu ya kuendelea na kuendelea kujifunza unaweza kufikia chochote.

Me naona Desire is more important than talent.
Unaweza kufundishwa kitu na kujifunza mwenyewe. Kwa hiyo unamaanisha ukijifunza mwenyewe ndo kipaji na ukifindishwa ndo skills, si ndiyo?
 
Hoja yako bado haija prove existence ya kipaji ipo au haipo.

Kipaji kipo ila , is why tuna mathematicians, scientits na watu wanao excel katika field mbali mbali

Kuna watu wanafanya baadhi ya shughuli effortless, as if they have figure it out, while wengine waki struggle au kutumia nguvu kubwa

Kipaji ni zawad ambayo mtu anayo, anaweza fanya jambo fulani kwa urahisi sana na kwa usahihi kuliko mtu mwingine. Na si wote wanakuja navyo
Ni kitu cha kuzaliwa nacho?

Hebu nijibu kwanza hapo.
 
mtu anazaliwa na kipaji bhana tusidanganyane na ndomana tuna majinias wakukalili darasani,tuna watu walotumia uwezo wao tuka pata,moto,umeme,ndege,magari,piki piki ,intanet n.k, afu wakafa zao na hakuna mtu wakuziba nafasi zao kilichobaki dunia imebaki kujifunza falsafa zao ili ielimike...kwa kuongezea tu mtu mwenye kipaji sio rahis kufeli maishani maana ana plan b nyingi.maana kipaji ni neema anayozaliwa nayo mtu,unashangaa mtu unasoma nae we unajitesa ye nikupiga kelele tu ila akiingia class anawaburuza wote,mfno mimi tangia nizaliwe sijawahi kuferi na hata nikiferi nasimama tena kwanjia ya ajabu yaani linakuja wazo la ajabu ukilifanyia kaz linaleta matokeo ya ajabu yaani na plan b kwa wing .kiufupi huwa hata mi najishangaa,nilijiona mjanja nikafanya utafiti nikagundua ninema tu,kwahiyo kama umefanikiwa usidharau watu maana umebebwa na neema hunautofauti na hao wengine ikiondoka neema hiyo huna chako
Kwa mfano mtu aliyetengeneza balbu aua aliyegundua moto alijaribu mara ngapi? Kama alijaribu zaidi ya mara Moja basi hajazaliwa na uwezo huo.
 
Kila mtu anazaliwa akiwa na uwezo wa asili wa kufanya mambo kwa ustadi wa kipekee unaomtofautisha na watu wengine. Uwezo huo ndio unaitwa Kipaji.

Kipaji kina kawaida ya kutoa msukumo mkali sana wa kutenda yahusianayo na Kipaji husika. Kwa mfano, kitendo cha wewe kuanza kutafakari kuhusu michoro(uchoraji) kinatokana na msukumo unaosababishwa na Kipaji cha uchoraji kilichopo ndani yako. Asiye na Kipaji cha uchoraji hawezi kufikirifikiri kuhusu michoro(uchoraji) kama ufanyavyo wewe(Hana huo msukumo ndani yake)

Hata hivyo Kipaji ni kama Mbegu kinapaswa kumwagiliwa(kuendelezwa) ili kioneshe ubora wake vinginevyo hufifia.
Kwa mfano ukizaliwa kwenye jamii isiyojua chochote kuhusu mchezo wa mpira wa miguu (hawajui kama Kuna mchezo huo) na mtoto mwenye kipaji cha mpira akazaliwa katika jamii hiyo, je naye atakuwa anaufikiria mpira ilihali hajawahi kuuona wala kuusikia?

Cc Infropreneur
 
Back
Top Bottom