Habari ya muda Great Thinkers!!
Wakuu nimegundua kuwa hakuna kitu kinachoitwa kipaji (talent) katika Dunia hii.
Wazungu hupenda kutumia dhana au neno kipaji wakimaanisha mtu kuzaliwa akiwa tayari ana uwezo wa kufanya kitu fulani kwa mfano kucheza mpira, kuimba, kukimbia. Wamefanya na wanafanya hivi ili tujikatie tamaa ya kufanya mambo makubwa kama gunduzi za kisayansi na mengine mengi.
Binafsi nilishawahi kujaribu kukatishwa tamaa na jamaa mmoja, hii ni mara baada ya kuona mimi najaribu kuchora. Jamaa aliniambia wewe wala usihangaike maana huna kipaji cha kuchora,maneno haya yalininipa hasira ya kupambana zaidai ndiyo maana leo hii mimi ni miongoni mwa wachoraji wakubwa hapa Tanzania (hii ni mara baada ya kugundua kuwa hukuna kipaji duniani)
Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa tayari na uwezo wa kufanya jambo fulani (kipaji), watu wote wanazaliwa sawa lakini namna ya kufikiria ndiyo humfanya moja afanye jambo fulani kwa urahisi kuliko mwingine.
Hebu jiulize haya maswali na uyatafakari kwa kina.
-Je, kama mpira wa miguu usingegunduliwa Messi angekuwa na kipaji cha nini?
-Kusingekuwa na mchezo wa riadha Usain Bolt angekuwa na kipaji gani.
-Je, Kuna kipaji cha kujamiiana?
-Kuna kipaji cha kula?
-Kuna kipaji cha kunywa pombe?
-kwa nini walokole wana uwezo wa kukariri mistari ya bibilia na kuichambua lakini wanashindwa kukariri quotations kutoka kwenye vitabu vya fasihi wakati yote ni maandishi?
Cc
Monetary doctor Poor Brain uzuri_hatujuani.
Bye bye 👋.