Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Jamie Vardy $ Shaggy nao hawakuwa na vipaji kwa majukumu yao ya awali kabla ya kuwa Football Striker na Reggae Dance Singer?

Ubinadamu ni kaziThe humanity is work.
View attachment 3333387View attachment 3333388

Hiyo bidii ndiyo kipaji chenyewe sasa, kwanini Wazungu huangalia vitu wapendavyo kuvifanya sana kisha huwapeleka shule kusomea hivyo vitu hadi ukubwani na wakibobea kuvifanya kwa ufanisi huviitaje?

Kwanini wasiwaache tu waendelee kuvifanya wenyewe bila ya kuelekezwa na kuongozwa wakiamini ni vipaji na watakuwa navyo kwa ubora zaidi kuliko wakipelekwa kusomea na kwa muda mrefu tu?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Itabidi tubadili definition ya kipaji mkuu. Tusiifananishe na instinct.
 
Kwa mfano mtu aliyetengeneza balbu aua aliyegundua moto alijaribu mara ngapi? Kama alijaribu zaidi ya mara Moja basi hajazaliwa na uwezo huo.
nikuulize swali hilo wazo la kitu kinachoitwa balbu alilitoa wapi? na kwanini kati ya watu wote duniani ye ndo alikuja na wazo hilo?, nikuulize nani alimpa akili edison ya kwamba kuna kitu kinaitwa balbu? najua edison alipata wazo la balbu baada ya rafiki yake kuvumbua gari lakin nikwanini ni edison tu na si mwingine?
 
Jamie Vardy $ Shaggy nao hawakuwa na vipaji kwa majukumu yao ya awali kabla ya kuwa Football Striker na Reggae Dance Singer?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
View attachment 3333387View attachment 3333388
Kujijua wewe ni Nani ?
Umebeba potential gani ndani yako ukawa hujui Hadi kuja kujua na kuamua kuondoka hofu na kuamini kuwa wewe ni mziki na utakomaa ulipwe Ada na Sio mshahara bhasi umesogelea chemi chemi ya maisha yako
 
Bado siamini kama mtu anazaliwa akiwa na uwezo wa kitu fulani.

Mtu aliyezaliwa akiwa na uwezo kwenye masuala ya architecture akizaliwa bushi hicho kipaji chake ataenda kukifanyia kazi wapi?

Natambua kuwa huko ulaya watoto wanaruhusiwa kujarib vitu mbalimbli ili kujua ufansi wao uko katika kitu gani lakini kuwa na ufansi kwenye vitu hivyo hakumaanishi kuwa waliozaliwa na uwezo huo bali Kuna other factors.
Kufanya ni hatua ya mwisho kabisa ya kudhihirisha Kipaji cha mtu. Kuna process unairuka nayo ni THINKING. Huyo atajikuta anaumba mastructure na mashape ya kufa mtu kwenye akili yake. Haijalishi yupo mjini au bush!
 
Mtoto anaambiwa ajaribu vitu mbali mbali ili kuona ni wapi anakuwa na urahisi wa kufanya au kutekeleza(kipaji). Hauwezi kuwa na urahisi wa kufanya kila kitu ? Kile ambacho ni kigumu kwako kufanya ni kirahisi kwa mtu mwingine. Na kile ambacho ni kirahisi kwako ni kigumu kwa mtu mwingine. Ndio maana kuna watu ni rahisi wao kufanya biashara. Na kuna watu wana mitaji lakini kila biashara wakigusa inafeli. Tumeshuhudia Kigangwala amepiga hela lakini kila biashara aliyofanya ilifeli.
 
Kipawa -Jinias - Hali ya juu ya utendaji.....Hapa ndipo yanapozaliwa madaraja na ukuu wa Watu.
Kasome post yangu ya pili kumjibu mleta mada Kuna jibu lako pale.

Utaalamu wa kutenda mambo fulani yaani kuliona Jambo ktk vipande vyake vyote kabla hujalifikia kilaza wa field hiyo atabakia kushangazwa tu.
Kuhusu utendaji wa hali ya juu mkuu sikupingi, ninachokipinga na dhana hii ya kusema Kuna watu wanazaliwa na uwezo fulani (kipaji) yaani mtu anatoka tumboni akiwa na uwezo fulani tofauti na watu waliptoka tumboni kama yeye.

Tunatoka tumboni wote tukiwa mbumbumbu lakini kutona na kujifunza kulingana na mazingira basi tofauti ya kiutendaji kati ya mtu mmoja na mwingine huanza kuonekana.

Naomba definition ya neno kipaji ibadishwe mara Moja.
 
nikuulize swali hilo wazo la kitu kinachoitwa balbu alilitoa wapi? na kwanini kati ya watu wote duniani ye ndo alikuja na wazo hilo?, nikuulize nani alimpa akili edison ya kwamba kuna kitu kinaitwa balbu? najua edison alipata wazo la balbu baada ya rafiki yake kuvumbua gari lakin nikwanini ni edison tu na si mwingine?
Mazingira yalimsukuma kufanya hivyo, yawezeka angezaliwa huku Afrika hata asingepata wazo hilo. Kwa mfano wazungu wa kutaka bara la ulaya wamefanya gunduzi nyingi kutakana na mazingira yao kutokuwa conducive kama ya huku afrika.

Huwezi kugundua ngalawa au meli halafu unakaa porini bali ukiwa karibu na maji.
 
Kufanya ni hatua ya mwisho kabisa ya kudhihirisha Kipaji cha mtu. Kuna process unairuka nayo ni THINKING. Huyo atajikuta anaumba mastructure na mashape ya kufa mtu kwenye akili yake. Haijalishi yupo mjini au bush!
Kwa hiyo akifikiria masua la ya construction bila kudhihirisha tayari anakuwa na kipaji cha hicho kitu?
 
Wengi sana na walikuja tambulika muda ushasogea sana kiumri.
Naamini watu wote wanapozaliwa wanakuwa sawa lakini wanapozi kukua utafauti huanza kujitokeza due to several factors.
 
Mkuu Uko Sahihi Lakini Iko Hivi Kwa Upana Zaidi

Kitu TALENT(Kipaji) Kipo Kabisa Tena Bila Doubt.100%
Katika Kundi kubwa la Watu Wengi Lazima Kuwepo mtu Mmoja Au Wachache Wenye Pure Talent.Sasa Utagunduaje Pure Talent???
Iko Hivi Kuna Watu Natural Kabisa ama Tuseme Biological Wamezaliwa Na Uwezo Wa Kufanya Jambo Fulani.
Wao Labda Watahitaji Maelekezo Kidogo Ama Muda Mwingine Wasipewe Maelekezo Na Wakafanikisha Jambo.
Wabrazili Wengi Wana Pure Talent Za Kucheza Mpira.Sasa Jiulize Why Wabrazili Wametamba Ulaya Miaka ya Nyuma Wengi Na Hawakutokea Academy?Why Sio Wa-Norway,Sio Wa-Finland Wala Wadenmark?
Mtaan mtaan Tu Mtu Anaonekana Huyu Mkali Kwenye Mpira(Ronaldinho)
Wazungu wanapagawa Wanampeleka Ulaya.Hajapita Academy Sana Wala Kuelekezwa Na Anakuja Kuintroduce Skills Mpya Kwenye Mpira?
Utasema Amejifunza?

Lakini Sasa Kwa Upande Mwingine
Kuna Kitu Inaitwa Law of Use n Disuse.Kiungo Chochote Katika Mwili Wa Binadamu Kina Uwezo Wa Kuadapt Jambo Fulani Na Kuwa Bora Kadri Siku Zinavyokwenda Mbele.

Sasa Tuendelee
Iko Hivi Wapo Wenye "TALENT" Fulani Mfano YA Music Production,Drawing Ni Lazima Kuna Mafunzo Kidogo Wapitie Ili Wawe Bora Zaidi.
Tuseme Master j,P Funky,Nahreal Hawana Talent Sababu Walipitia School Of Music Kupata mafunzo ya mziki kidogo?HAPANA Wanavyo.
Ila Walihitaji Training Kidogo ILA USISEME HAWANA TALENT ETI WALIADAPT Na watu wengine Wakijaribu Wataweza Kutengenez Midundo Mikali Kirahisi Rahisi Tu..BIG NO.
IKIWA Huna Talent Husika Unaweza Fanya Trainings Lakini Hutokua Mbunifu Na Kuadd Extra Things Hii Hasa Hasa Kwenye Sanaa.
Zaidi Zaidi Utacopy
Mfano Utasikua Msanii Fulani Anasound Kama Msanii Fulani,Ni Kwamba Anayecopy Mara Nyingi Huishia Kuwa Bora LAKINI Hana Pure Talent.Sio Bunifu
Na Hawa Wapo Wengi Sio Kwnye Mziki Hata Kwenye Mpira na Kada Zingine.

Kwa Kumalizia Mfano Hawa Music Producers...Hawa Hawazaliwi na Uwezo Wa Kutengeneza Mziki Directly Kwa Asilimia Mia,Hawazaliwi Wakijua Kucheza Vifaa Vya Muziki e.g Piano,Violin,Guitar.
Lakini Sasa Mwisho Wa Siku Baada Ya Training Wanakuwa Bora Vipaji Vinafunguka.
Ikiwa Huna Talent Sasa ya Music Hata Ufanye Mazoez vipi Au Uwe Trained Kiwango Gani Huwezi Kuwa Kuwa Mkali Kiwango Cha Juu..unaishia Kukaririshwa machords,mascale ma intervals Lakini Huna Creativity

Kwa Kuhitimisha Ni Hivi
1.Kuna Kundi La Kwanza Hawa Huzaliwa Na Pure Talent Na Hawahitaji Mafunzo Sana Kufanya Ubunifu.
Mfano Wolfgang Mozart Kwenye Music Composition, Ronaldinho Gaucho Kwenye Soka Ama Usain Bolt Kwnye Riadha.
Pure Talent Huwa Bunifu,Hazitumii Nguvu Mno na Very Passionate.
-Ukiona Una Hivi Jua Una Pure Talent
2.Lakini Kuna Kundi La Pili La Kujifunza,Kuadapt Kwa (Mawazo,Vitendo,)Mwisho unakuwa Mkali.UBONGO UNATANUKA,MWILI Unaadapt Mwisho TALENT INAONEKANA.
3.Talentless
Hawa hawawezi Jambo Hata wafundishwe Vipi Au Wawe Trained Kiasi Gani.
Na Hawajazaliwa Kufanya Jambo Husika.
 
Mtoto anaambiwa ajaribu vitu mbali mbali ili kuona ni wapi anakuwa na urahisi wa kufanya au kutekeleza(kipaji). Hauwezi kuwa na urahisi wa kufanya kila kitu ? Kile ambacho ni kigumu kwako kufanya ni kirahisi kwa mtu mwingine. Na kile ambacho ni kirahisi kwako ni kigumu kwa mtu mwingine. Ndio maana kuna watu ni rahisi wao kufanya biashara. Na kuna watu wana mitaji lakini kila biashara wakigusa inafeli. Tumeshuhudia Kigangwala amepiga hela lakini kila biashara aliyofanya ilifeli.
Swali la mwisho. Je, hao wanaofanya mambo kwa urahisi unadhani waliozaliwa na uwezo huo au Kuna other factors behind.
 
Swali la mwisho. Je, hao wanaofanya mambo kwa urahisi unadhani waliozaliwa na uwezo huo au Kuna other factors behind.
Ni walizaliwa nayo, Usain Bolt mafanikio yake ni genetics, Michael Phelps Mafanikio yake ni Genetics, Nimetoa mfano wa genious Zawadi Mdoe nikakuambia mama na baba yake walikuwa maprofesa SUA. Na watazania hatufanikiwi kwa sababu hatuthamini vipaji tulivyobarikiwa.
 
Mazingira yalimsukuma kufanya hivyo, yawezeka angezaliwa huku Afrika hata asingepata wazo hilo. Kwa mfano wazungu wa kutaka bara la ulaya wamefanya gunduzi nyingi kutakana na mazingira yao kutokuwa conducive kama ya huku afrika.

Huwezi kugundua ngalawa au meli halafu unakaa porini bali ukiwa karibu na maji.
sawa kwanza nini maana ya kipaji,kipaji ni uwezo au kipawa anachozaliwa nacho mtu .mfano charles page alipataje akili ya kuvumbua ndege wakati ni mwafrika? jibu ni kipawa au zawadi aliyopewa na MUNGU.AMBapo kupitia yeye watu wanaingia shuleni kujifunza kanuni alizo tumia kuunda ndege,na ndomana ndege zinaendelea kuzalishwa na kuboreshwa hata baada ya yeye kufa
 
Back
Top Bottom