makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 37,696
- 109,218
Kipaji kipo, lakini kanuni ya practice makes perfect inafanya kazi, ila haiondoi uwepo wa KIPAJI
📌📍📍🔨🔨🔨.Ni kweli hakuna mtu anaezaliwa na uwezo wa kufanya jambo fulani,.. bali uhalisia ni kwamba mtu "A" atakua vizuri na mtaalamu kwenye jambo fulani kuliko mtu "B" kutokana na sababu zifuatazo:-
1. Mazingira,,.. Mazingira yana nafasi kubwa sana ya kumfanya mtu apende jambo fulani kutokana na kuliona hapa kuna mtu atakuliwa kwenye jamii ya wapenda uvumbuzi, michezo na kadhalika... yaani Mtoto anayekua kwenye jamii ya wanamichezo au wasanii ana nafasi kubwa ya kuathiriwa na mazingira hayo.
2. Kupenda jambo fulani,.. hapa sasa kutokana na shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye mazingira inamfanya mtu kuwa na mapenzi na shughuli fulani ambayo ipo kwenye jamii hivyo atajikuta anajifunza shughuli hiyo na kujikuta akiongeza ujuzi zaidi hadi kuwa mtaalamu haswa...,Mtu anapopenda kitu, anakuwa tayari kutumia muda, nguvu, na maarifa kukiendeleza., hivyo utakuta anafanya mambo makubwa na kushagaza kwenye fani husika.
3. Akili ,.. hapa ndiyo panapoleta tofauti kubwa lazima tukubaliane kwamba kiwango cha akili kinatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine na ndiyo maana utaona watu 10 wanafanya jambo moja tuchukulie mfano ni wachoraji,. ila utakuta 1 au 2 kati ya hao anatoa kitu bora zaidi., hapa uwezo wa akili kukumbuka, kuamini kwenye uwezo wake na kufikiria kwa haraka zaidi umetengeneza gap kati ya watu.
so, kutokana na hivyo vitu vitatu hapo juu sisi ndiyo tunakosea kwa kusema kwamba mtu fulani amezaliwa na uwezo fulani(talent) kumbe haipo hivyo ni mazingira, mapenzi juu ya task fulani na akili ya mhusika.
Lamine Yamal angezaliwa Tanzania asingekuwa na uwezo kama alionao Leo.Useless thread,vipaji vipo na kama unabisha nenda kacheze mpira kama Messi tukuone
Mkuu point ya vipaji kuendelezwa unaipotezea.Lamine Yamal angezaliwa Tanzania asingekuwa na uwezo kama alionao Leo.
Hata Messi na Ronaldinho wangezaliwa Tanzania wasingekuja na uwezo kama ule japoku Tanzania Kuna mchezo wa soka.
Lamine angekuwa Tanzania angecheza mpira lakini uwezo wake ungekuwa wa kawaida.Mkuu point ya vipaji kuendelezwa unaipotezea.
Hayo mazingira kwanini yamfavour yeye na kuacha wengine?Lamine angekuwa Tanzania angecheza mpira lakini uwezo wake ungekuwa wa kawaida.
Lamine anashine si kwa sababu alizaliwa na uwezo wa kucheza boli bali mazingira yanamfavour.
Haya kwa nini wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wana uwezo mkubwa kuliko wa timu ya taifa ya Tanzania?Hayo mazingira kwanini yamfavour yeye na kuacha wengine?
Mkuu swali ambalo linatakiwa kujibiwa kwamba ni kitu gani ambacho hufanya mchezaji mmoja kuonekana bora kuliko wenzake na hali ya kwamba watu wapo katika mazingira sawa na hufanya mazoezi sawa?Haya kwa nini wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wana uwezo mkubwa kuliko wa timu ya taifa ya Tanzania?
Je ni Kawa sababu wenye vipaji ya soka wanazaliwa tu Uingereza?
Haya jibu la swali lako ni kwamba wote hamwezi kufanya jambo katika kiwango sawa. Yamal anawazidi baadhi ya wachezaji kama Feisal Salum anavyowazidi baadhi ya wachezaji wa hapa Tanzania.
Huyu fei toto ambe kwa huku mnasema ana kipaji na anafanya mazoezi akienda kwenye ligi kuu ya Uingereza anawekwa benchi na wachezaji ambao nyinyi mnadai kuwa hawana vipaji lakini wote wanafanya mazoezi😂😃😅.
Cc implicit memory Nomadix Al-mukheef
Mkuu ukisoma comments zangu toka mwanza hayo mambo nimashayaelezea vya kutosha na ukipata muda jaribu kuangalia zile comments nahisi utakubaliana na mimi kuwa hakuna kipaji.Mkuu swali ambalo linatakiwa kujibiwa kwamba ni kitu gani ambacho hufanya mchezaji mmoja kuonekana bora kuliko wenzake na hali ya kwamba watu wapo katika mazingira sawa na hufanya mazoezi sawa?
Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa anajua kuendesha Baiskeli,. ila ukiwachukua watu 10 na kuwashindanisha kwenye mchezo wa kuendesha baiskeli mmojawapo ataonekana bora kuliko wengine.Mkuu swali ambalo linatakiwa kujibiwa kwamba ni kitu gani ambacho hufanya mchezaji mmoja kuonekana bora kuliko wenzake na hali ya kwamba watu wapo katika mazingira sawa na hufanya mazoezi sawa?
Akikujibu tafadhali unitag😎.Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa anajua kuendesha Baiskeli,. ila ukiwachukua watu 10 na kuwashindanisha kwenye mchezo wa kuendesha baiskeli mmojawapo ataonekana bora kuliko wengine.
Je, hapo utakua sahihi ukisema huyo aliyeshinda amezaliwa na kipaji cha kuendesha baiskeli?
Sasa ni nini kinachomfanya Messi aonekane anajua kuliko wengineHaya kwa nini wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wana uwezo mkubwa kuliko wa timu ya taifa ya Tanzania?
Je ni Kawa sababu wenye vipaji ya soka wanazaliwa tu Uingereza?
Haya jibu la swali lako ni kwamba wote hamwezi kufanya jambo katika kiwango sawa. Yamal anawazidi baadhi ya wachezaji kama Feisal Salum anavyowazidi baadhi ya wachezaji wa hapa Tanzania.
Huyu fei toto ambe kwa huku mnasema ana kipaji na anafanya mazoezi akienda kwenye ligi kuu ya Uingereza anawekwa benchi na wachezaji ambao nyinyi mnadai kuwa hawana vipaji lakini wote wanafanya mazoezi😂😃😅.
Cc implicit memory Nomadix Al-mukheef
Ni kile kinachofanya Fei toto kuonekana mchezaji mzawa Bora kwa sasa kwenye NBC Premier league.Sasa ni nini kinachomfanya Messi aonekane anajua kuliko wengine
KIPAJINi kile kinachofanya Fei toto kuonekana mchezaji mzawa Bora kwa sasa kwenye NBC Premier league.
Niambie kwanza kinachofanya Feisal kuonekana bora kuliko wachezaji wengi (japo si wote) wazawa kwenye NBC Premier league.
Kaka ambaye ni miongoni mwa wachoraji wakubwa nchini na uliyejifunza uchoraji kwa siku mbili tu mbali na hongera zangu kwako. 🙏🏾Tupia hapa kazi kadhaa ulizochora ili kutuInspire sie tunaopambana kujifunza kuchora kwa miaka kenda bila mafanikio.Habari ya muda Great Thinkers!!
Wakuu nimegundua kuwa hakuna kitu kinachoitwa kipaji (talent) katika Dunia hii.
Wazungu hupenda kutumia dhana au neno kipaji wakimaanisha mtu kuzaliwa akiwa tayari ana uwezo wa kufanya kitu fulani kwa mfano kucheza mpira, kuimba, kukimbia. Wamefanya na wanafanya hivi ili tujikatie tamaa ya kufanya mambo makubwa kama gunduzi za kisayansi na mengine mengi.
Binafsi nilishawahi kujaribu kukatishwa tamaa na jamaa mmoja, hii ni mara baada ya kuona mimi najaribu kuchora. Jamaa aliniambia wewe wala usihangaike maana huna kipaji cha kuchora,maneno haya yalininipa hasira ya kupambana zaidai ndiyo maana leo hii mimi ni miongoni mwa wachoraji wakubwa hapa Tanzania (hii ni mara baada ya kugundua kuwa hukuna kipaji duniani)
Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa tayari na uwezo wa kufanya jambo fulani (kipaji), watu wote wanazaliwa sawa lakini namna ya kufikiria ndiyo humfanya moja afanye jambo fulani kwa urahisi kuliko mwingine.
Hebu jiulize haya maswali na uyatafakari kwa kina.
-Je, kama mpira wa miguu usingegunduliwa Messi angekuwa na kipaji cha nini?
-Kusingekuwa na mchezo wa riadha Usain Bolt angekuwa na kipaji gani.
-Je, Kuna kipaji cha kujamiiana?
-Kuna kipaji cha kula?
-Kuna kipaji cha kunywa pombe?
-kwa nini walokole wana uwezo wa kukariri mistari ya bibilia na kuichambua lakini wanashindwa kukariri quotations kutoka kwenye vitabu vya fasihi wakati yote ni maandishi?
Cc Monetary doctor Poor Brain uzuri_hatujuani.
Bye bye 👋.