Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Hili ndo jibu sahihi kati ya majibu yote.
Na jibu hili linadhihirisha kuwa hakuna kipaji.
 
Hapo kwenye mabo ya miili uko sahihi kwa mfano umbo lake linamfanya kuwa na uwezo wa kipiga chenga za haraka haraka.

Lakini bado naamini binadamu wote wanazaliwa sawa lakini mazingira na namna ya kufikiri ndo vinachangia mtu kuweza kufanya jambo fulani kwa urahisi.
 
Ndo kipaji chenyewe hicho, kuna yule jamaa wa kitambo wa kuitwa Wabogojo, alikua na uwezo wa kujikunjakunja mithili ya mtu asie na mifupa, kile ni kipaji ambacho hata ukijifunza sio rahisi kua kama yeye.

Mwisho wa siku unakubali kua ndivyo alivyozaliwa.
 
Je, wanyama nao wana vipaji?
 
Kama nawewe Great Thinker wa jf kazi ipo.

Unakili wazi kuwa uliambiwa kuchora ni kipaji sio? Basi wewe ukapata hasira ya kujifunza zaidi hadi ukawa bora sio?

Sasa kuna dogo wangu anaye nifuata kabla hata hajaanza kusoma chekecheka alikuqa akiona karamu yyte iwe ya wino au mkaa basi anachora wanyama anaowajua.

Baada ya kufika la pili tu alikuwa na uwezo wa kuchora kwa bora mno! Niambie huyu ni kipaji au alijifunza? Alijifunizia wapi wakati wakubwa zake hakuna mchoraji?


Maswali uliyouliza majibu yake yote unayo unadhani wana liadha wote wako tu huko Olympic?

Kuna jamaa wanafunguka kana kwamba wana motor mguuni na hutawaona wanafanya mazoezi popote pale!!

Uelewe hata yule aliyengudua mpira nae anakipaji hicho.

Kuhusu kula wewe hata iweje huwezi maliza kg1 ya mchele yaani mchele ununuliwe then upikwe uwe wali halafu jamaa mmoja tu na nusu ya maharage anakula ana maliza.

Kuna jamaa3 tu walikuwa wanakula mbuzi mzima (kienyeji) mkubwa sio wachezaji wa mpira sio wachezaji wa mieleka jamaa wanakula sio poa
 
Je, wanyama nao wana vipaji?
Hilo sijafahamu, ila wanyama wana tabia tofauti tofauti kulingana na aina zao.

Sisi binadamu tunaita kipaji kwasababu kwa mtu mwingine kufanya kiwepesi, kwa haraka au kwa ufanisi kama afanyavyo huyo mwenye "kipaji" ni changamoto.
 
Nilitumia siku tatu tu kujifunza kuchora
1.Kuingia kuchora ukidhani unajua kila kitu....ukakuta hujui.
2.Ukarudi ukijua hujui na ukaamua Urudi kuchora ili kujisahihisha.

3.Ukarudi kuchora ukijua sijui ila Nina uwezo... Kwa kulinganisha michoro yako na ya wazoefu.

Ulitumia Muda gani kutambua hatua hizi ?
 
Kaa chini ufikirie kwa nini huyo mdogo wako alianza kuchora na baad ya kufika la pili alianza kuchora vizuri zaidi.

Pia fikiria kwa nini wewe ulipokuwa mdogo ulikuwa na hati/mwandiko mchafu lakini Leo unandika vizuri na kama unatumia mkono wa kulia kuandikia hebu Leo jaribu kuandika kwa mkono wa kushoto halafu unipe mrejesho.
 
Kila mtu ana Kipaji ila kimebeba vitu viwili.
1.uwezo kama huna uwezo kujua kipaji chako kuanzia kimwili mpaka kiroho itakuwa ngumu kujua uwezo wa kipaji chako.

2.mazingira ili nimethibitisha kwa watu ambao wmeenda nchi au maeneo vikatambulika vipaji vyao bila wao kujua.
Mfano kwa nini USA inaweza kukusaidia kujua kipaji chako kuliko huku TZ mtu mpaka unazeeka ujawahi kutambulika umuhimu wa kipaji chako mfano lissu.

3.watu au jamii inayokuzunguka.
Ili linaweza kuonesha kipaji chako au kutokuonesha kipaji chako.Ndio maana bila wcb reyvan ,konde na zuchu wasingejulikana.
Unakumbuka kipaji konde kilizimwa kipindi cha BSS
 
Hilo sijafahamu, ila wanyama wana tabia tofauti tofauti kulingana na aina zao.

Sisi binadamu tunaita kipaji kwasababu kwa mtu mwingine kufanya kiwepesi, kwa haraka au kwa ufanisi kama afanyavyo huyo mwenye "kipaji" ni changamoto.
Ukitumia ubongo vizuri kitu chochote unaweza kuifanya kiuwepesi shida ni kwamba watu wengi hatuamini kuwa Kila kitu kinaanza na idea kabla ya tendo halisi.

Watu wengi wanaoshindwa ni wale wanaoamini katika kufanya kitu pasipokufikiria kiundani kwa mfano Leo hii kutokana na ukuaji wa say si na teknolojia watu wanasumbuliwa sana na mental laziness yaani mtu hata hesabu ya kujumlisha anakimbilia kwenye kalkuleta.
 
Yote kwa yote tunaziliwa sawa lakini mazingira plus uwezo wa kutumia akili zetu plus mapenzi yetu juu ya jambo fulani ndo yanaleta utauti.
 
Kuhusu kuchora ni Talent MAANA UNCLE WANGU alikua na uwezo wa kukuangalia na AKAKUCHORA KAMA ULIVYO

IMAGINE MTU ANAKUTIZAMA NA ANAKUCHORA.
 
We hoja yako ni ipi?
 
SIKU ZOTE NIMEKUA NASEMA KAMA NISINGEKUA NAFANYA. HIKI NACHO KIFANYA BASI MPIRA WA MIGUU NDIO UNGELIPA BILL ZANGU ZOTEEE.

KWENYE MGUU WANGU WA KUSHOTO MUNGU ALIWEKA KIPAJI CHA AJABU CHA KUSAKATA KABUMBU NILITABILIWA KUFANYA MAKUBWA.

ILIKUCHUKUA SEKUNDE KADHAA MPIRA UKIWA MGUUNI KULITHIBITISHA HILO MIMI NILI UDHARAU MPIRA WA MIGUU

NILIKUA NA MIKIMBIO SKILLS AMBAZO NILIKUA NA KASI YAKUWAPITA WATU KAMA WAMESIMAMA

KUNA VIPAJI MZEE KAMA MWINGINE ANAVYO KILEMU MASOMO KAMA KASUMU MWINGINE ANASOMA NA KUELEWA
 
Talents zipo. Na unaanza kuziona ukiwa Shule. Kuna binadamu hata usome vipi, huwezi kuwapita kwa sababu wana uwezo mkubwa (talent) kwenye hilo eneo kukuzidi wewe.

Unachokizungumzia wewe ni "to get better" at something. Yani kwamba kila mtu akiweka juhudi katika kitu chochote basi anaweza akawa bora zaidi kuliko alivyokua mwanzo.

Sasa ukitaka kujua tumeumbwa tofauti huku duniani na vipaji vipo na ni "real", nenda kwenye competition za vitu unavyoamini kuwa wewe una talents navyo, uone katika hicho hicho unachojiamini nacho, wenzako wanakifanya katika scale gani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…