Hakuna kitu kinaleta Stress kama kuota Mvi au upara halafu bado hujajipata

Hakuna kitu kinaleta Stress kama kuota Mvi au upara halafu bado hujajipata

Et nywel zimenyonyoka kama mbwakoo, Amehlo nitakutazamaje mimi tena boss wangu na ninadhalilishwa hivi !!.

Ujue vijana msio na uzoefu wa maisha (mnayajua maisha kwa kuandika andika tu) mnafikiri kuna tofaut kubwa sana kati ya 25's -35's.

The difference is sooo minor.. tulia uone sasa. The gap too short..leo uko 25's ndio wengine mmetola toka chuo, ghafla tu unajikuta 35.. unajikita seriously umeanza kupambana at 30, boooom!! 35 hii hapa. Usicheke cheke hapa dogo Intelligent businessman ..
achana nao hata nywele zako hazijanyonyoka kama mbwa koko

kwanza ndo zinavutia
 
Jifunzeni Kwa wakurya, miaka 18 u meshaoa, una watoto wawili ndipo unaendelea na utafutaji.

Maisha ni Kupambana, muhimu Uzima,

Hakuna stress kubwa kama Binti wa 12 yrs kujazwa mimba.

Mwanaume hapati mimba!!

Hivyo Kwa sie wanaume hakuna kitu inaitwa stress, tupambane.
I second you

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Kwema Wakuu!

Ni Stress hapa!
Ni sonona hapa! Kihoro kinakaba kama pumu huku. Yaani hapa mambo sio mambo.

Kuna Watu wanakuambia umri ni number tuu lakini huko ni kufarijiana tuu!
Hakuna kitu kinauma na kuleta mfadhaiko na mtagusano kulinafsi kama kuona jua lile linazama halafu wewe mambo bilabila.

Nywele kunyonyoka kama mbwakoko mzee. Alafu ukicheki huna mbele wala nyuma sio Pouwa Washikaji.
Mvi kukuota wakati unaishi chumba kimoja sio lelemama ndugu zangu.

Fikiria mvi hizi hapa alafu huna hata mke wala mtoto. Kiumri ni miaka labda 35 hivi. Shida ni kuwa mpaka muda moja na mbili haikai.
Kila ukikumbuka ile kauli ya kusema nikiwa mkubwa nitafanya bla! Blah! Blah! Unapiga ngumi ukutani.
Nani akutake na mvi zako Budah! Yaani huna pesa alafu umejaza mvi kichwani. Ni binti gani yupo tayari kukubali kuwa nawe?
Binti gani atakubali kuwa na wewe na kipara chako na hauna Maisha.

wanasema vijana ndio huona maono bwashee! Wazee wenye mvi na vipara huota ndoto tuu. Yaani kila unaloliwaza kuna asilimia 70 kuwa ni ndoto uotayo ya alinacha.

Kipara sio shida. Shida ni pale huna mbele wala nyuma. Nyie ni mateso bila chuki. Hujui tawi gani ushike.
Yaani Upara na mvi vinakukuta ni Jobless mamaaaa! Hujui ufanye nini unafikiri Daah!

Unakipara chako kinamea polepole, au unamvi zako alafu huna pesa mbona lazima uwe introvert tuu. Yaani ndio ile unajikita mkimya maana nini sasa utaongea. Na hawa vijana wa 2000 hawana salia mtume, hawajui la muhazini wala mnadi Swala. Watakuona Babu yao ilhali hata miaka 40 huijui.
Utani utani wa kijinga na maneno ya kukutania vitazidi kushamiri.
Automatically kijiweni utaanza kupotea na utakuwa mtu wa kuwa bize for nothing.

Usiombe hiyo hali ikukute mazee! Kwanza hata ukienda vibaruani lazima uzinguliwe na matajiri kwa sababu wanajua huna chaguo, alafu mbaya zaidi lazima wakuzungushe kwenye malipo. Alafu ukijaribu kuwa mshari wanakuambia hayo mambo waachiw vijana ilhali wewe mwenyewe ndio kwanza upo miaka 35. Kudadadeki! Innalilah wainalilah Rajuun!

Chochote ukitaka kukifanya ukiwa kipara au mvi tena kwa mtaji mdogo lazima kikutie unyonge, Watu watakuwa wanakuona kama Budah fulani hivi.

Napendekeza, ukiwa below miaka 30 na umetoka familia maskini, kisha bado hauna ramani kivile.
Miaka 20- 30 ndio umri wako wa kujaribu kufanya kazi zózote na kujiweka sawa. Ndio umri wa kutafuta Pisikali moja uzae nayo yaani uanzishe familia ukiwa bado unamuonekano mzuri.

Usibeti kuwa ngoja utafute pesa Kwanza, huko ni kubet Ndugu yangu. Unaweza ukapata pesa au usipate. Lakini kwa umri wa miaka 20-30 huwezi kukosa Mwanamke mzuri wa kuanza naye familia akuzalie watoto angalàu mmoja au wawili.

Ili hata mambo yakibuma na mkeo akakuzingua uwe unafaida ya mtoto au watoto.
Lakini umechelewa kuanzisha familia kwa kubet kuwa unatafuta pesa Kwanza. Alafu umri umesogea, kipara na mvi zile alafu pesa hujapata. Ndugu yangu umekwisha!

This is Africa. Kanuni za huku ni za kipekee. Fanya kile ambacho unauhakika nacho kwa sasa na sio kubet kuwa unatafuta pesa kwanza kama vile uko Ulaya.

Elewa, huku Afrika unaweza ukawa na Juhudi, bidii na akili lakini bado maisha yakakupasua tuu. Lakini kwa Ulaya hilo haliwezekani.
Usijidanganye hapo na vishughuli vyako vya kujitafutia ambavyo vinakuingizia mia mbili mia tatu na kujipa moyo kuwa mambo yakikaa vizuri ndio utaanzisha familia. My friend, unajidanganya. Kwa Afrika labda uwe umeajiriwa tena serikalini ndio unaweza kufikiri kwa namna hiyo.

Biashara inabadilika muda wowote. Ni bora ibadilike ulishapata watoto tena na mke mzuri ambaye hata mkiachana haitalalia upande wako.

Uzee unatísha wazee! Uzee ambao haujajipata sio pouwa ndugu zanguni. Wanaosema Fainali uzeeni wanajua wanasema nini ndugu zanguni.

Tuombe Mungu atupe akili ya kutumia baraka zake lakini pia atupe uwezo wa kufanya mambo kwa wakati ili tusijetaabika.

Mwenye mvi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Haaaaaa! ni kweli kabisa, ila umri uliohutaja sio cut -off point ya kusonga mbele kwa umri kwa tamaduni za kibongo; miaka 35 bado ni kijana kabisa kwa setting na social life yetu ya kiafrika . Pia nakubaliana na mtoa hoja mwingine, wengi walio kwenye age hiyo ndio kwanza wanajitafuta, just imagine miaka 7 ya primary school, miaka 4 ya secondary school-O-LEVEL, miaka 2 ya A-LEVEL, mwaka mmoja kusubiri kuingia chuo kikuu, miaka 3-4-5 chuo kikuu, mwaka 1-2 internship, then mtaani kusaka kazi kati ya miaka 2-5 ndipo uipate, unafikiri huyu kijana atakuwa na miaka mingapi hapo? ukizingatia alianza primary kindagarten huku akiwa na miaka 6-7 baada ya kuchunga ng'ombe na kuuza mazao kwenye magulio saaana .

Kwangu tatizo si kuendelea kujitafuta tatizo unaota kipara halafu kichwani patupu , au unakuta kijana wa miaka 35 akiwa na kitambi kikubwa na muonekano wa kiutu uzima mwenye fedha wakati kila siku akipiga mizinga. Pathetic.
 
nilipokua home arusha walikua wanakuja sana
.hata mm huwa najiuliza hivyo. ni wazuri sana wakurya wa kenya tofaut na wa huku
wengi ninaowaona mimi hawana ule weusi wa wadada wengi wakenya wanao, ni wazuri sura zao zinataka kwenda kama kwenye u Ethiopia au rwanda japo wanyarwanda chocolate yao imezidi
 
Tatizo la wasomi wengi mnadhani Uzunguni ni huku Afrika.
Alafu mnavunja kanuni ya kila jambo lina wakati wake.

Kiafrika ukifikisha miaka 45 na bado hauna muelekeo hiyo ndio imeisha kwa waliowengi. Hizo Exceptional cases za wanaotoboa uzeeni usipende kuziendekeza. Hao ni éxceptional ni wateule
Umeongea ukweli kabisa, kibongo bongo hiyo age ndo nitolee hapo ni kusubiri kujiuguza visukari na presha zisizoisha
 
Back
Top Bottom