sblandes
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 6,632
- 4,737
Adui wa Demokrasia ya nchi hii ni Mbowe .
Mbowe hakuikuza Chadema Bali Mbowe alisafiria nyota za makada wenzake waliotoka CCM.
Mbowe angemkosa Slaa ni kama mkulima mwenye mpini tu usio na jembe.
Mbowe angemkosa Zito miaka ya 2010-2015 vyuo vikuu na waislam kuiamini Chadema ni kama mkulima mwenye Jembe bila mpini wake.
Mbowe angemkosa Lowasa 2015 ni kama mkulima mwenye Jembe bila kuwa na shamba la kulima.
Sasa Mbowe Mwaka huu anataka kusafiria nyota ya Lisu na Nyarandu yupo kama mkulima mwenye Shamba bila kuwa na Jembe la kulimia .
Baada ya Uchaguzi huu Mlevi huyo unayetaka kuwaaminisha wahuni kuwa ndiye aliyeijenga Chadema atabaki kama mkulima asiye na shamba wala Jembe.
Siasa sio mchezo kama kama mpira. Siasa zinahitaji ushawishi na hoja zenye misimamo imara kiroho na kijamii.
Mbowe hana mvuto wa kiroho wala kijamii .
Mbowe ni mjasiriamali mwenye haiba na hulka ya tamaa ya fedha ,wizi, ubinafsi, na mtu asiye na huruma anaposikia harufu ya madaka na fedha.
Ni kosa kubwa sana kumwamini tajiri Mbowe apiganie haki za maskini 80% wa nchi hii. Ni kujilisha upepo kumtegemea Tajiri atangulie mbele ya vitani wakati anawaza Mali zake na starehe na mademu wake.
Kujitoa muhanga kunaendana na kujaa imani kiroho ili mtu aweze kuipigania jamii bila kujali maslahi au kupoteza.
Mbowe ni muoga kuliko kunguru. Ndio maana mpaka kijijini kwake Chadema imefyata mkia kwa kumwogopa kijana Machachari na Kada wa CCM DC .Sabaya.
Kumlinganisha Zito Msomi na mwanasiasa aliyeanzisha Chama wakati mgumu kabisa huku akitukana na CCM na Chadema ni sawa na kumlinganisha Faru (Zito) na Ngiri (Mlevi Mbowe).
Mbowe amerithishwa chama kwa sababu ya ukabila tu na ukaribu wake na Mtei lakini Mbowe hana uwezo wa kuanzisha chama cha siasa duniani na hata kuzimu achilia mbali Mbinguni Patakatifu pasipohitaji walevi na wazinzi na wezi.
Siasa ni kazi na vipaji vya baadhi ya watu kama ilivyopira na michezo mingine na hata biashara na kazi nyingine.
Wanasiasa ni watu kwenye jamii wasiopenda kuongozwa wala kupangiwa jambo na wengine bila wao kushiriki. Hata mkikaa kwenye kikao cha harusi kama kuna mwanasiasa atakua msemaji sana na kutoka kuona mawazo yake ndiyo yanasikilozwa. Hata kwenye msiba wanasiasa watakuwa mstari wa mbele kuonekana.
Kwenye familia pia wanasiasa watajitokeza mbele kutaka wasikilizwe wao.
Kwa hiyo hakuna namna ya kuwazuie eti wasitoke CCM na kwenda Chadema au kutoka chadema kurudi CCM.
Dunia ndivyo ilivyo. Hakuna namana ya kuwatenganisha wanasiasa wa upande mmoja tuu wasiunge mkono upande mwingine kwenye baadhi ya mambo.
Ni vijana wachache walevi tu ndani ya Chadema wanaowaita watu wa vyama vingine wanaojiunga na chama hicho au wanaohama kuunga mkono baadhi ya utendaji wa wapinzani wao kuwa ni wasaliti. Ingekua hivyo Marekani chama kimoja kingetawala milele. Lakini kule watu wanamkataa hata kama ni MTU wa Chama chake lakini anafanya mambo ya hovyo anapingwa na ananyimwa kura na wanachama wa chama chake wanapunguza kura zake zinahamia kwa mpinzani wake.
Tanzania katika Uchanga wake imefanikiwa kuwa na siasa nzuri za ushindani wa hoja ndani ya CCM na nje ya CCM. Nchi hii ilikua ya Chama kimoja chenye upinzani mkubwa sana wa ndani hivyo usione ajabu watu kutoka nje ya CCM na kumpinga mtu waliyekua wanaimba pamoja CCM yajenga nchi.
Kumbuka Bado Afrika tunatambuana kwa makabila na dini na asili zetu.
Hata kwenye taarifa zetu kwenye fomu mbali mbali zinaeneo la kujaza Kabila lako,dini yako n.k.
Dini ,kabila na ukanda unaathiri sana siasa za Tanzania . Jambo ambalo Chama la Chama la kupindua wanafanikiwa kudumu milele madarakani kwa kutumia hayo mambo matatu.
Akiwa wa dini Fulani basi dini ile wote wataapena ishara ya kumuunga mkono hata kama atakosea watajitokeza kumuunga mkono kwa nguvu zote.
Wakiona dini haimuungi mkono huyo basi wanahamia kwenye ukanda au kabila . Yote hayo ni tatizo la woga wa mwanasiasa waliozoea kukaa madarakani na wakajiwekea marupurupu makubwa na Kuweka katiba inayowapa madaraka makubwa.
Hapo ishu sio kikundi cha watu nyuma ya pazia kupanga nani awe wapi . Huo ni uongo mkubwa. Siasa za Kiafrika zinaathiriwa na Umaskini na Katiba zinazotoa madaraka makubwa kwa watawala.
Mtawala akishika madaraka anakua ni zaidi ya mungu juu ya wanadamu wenzake mana anashila mpaka nafasi ya kupanga nani ashibe na nani aishi kama malaika na nani aishi kama shetani.
Hii hali inawafanya wanasiasa wakose misimamo zaidi ya kubaki wakiwa wanajipendekeza ili waishi kama malaika muda wote.
Hivi Mbowe na Tundu Lisu nani ni mpinzani toka Rohoni bila kujali Umaarufu, madaraka, Dhiki, kupoteza uhai, kupoteza fedha na kudai Mali za chama kama fidia ya muda na fedha zake n.k????
Bila shaka Lisu ndiye mpinzani wa kweli .
Mbowe ni Magumashi ndio maana alibadili katiba ya Chama ili afie kwenye Uenyekiti wa Chadema.
Mkitaka Mbowe arudi CCM kesho asubuhi mtoeni kwenye Uenyekiti halafu aone Mali zake zinafilisiwa na hana uwezo wa kukwapua Ruzuku kufidia mali anazopoteza .
Atakimbilia ikulu asubuhi kabisa kupiga magoti.
Nisipomtaja Mbowe kwa mabaya yake ni sawa na Mchungaji asipomtaja Shetani kwa kumlaani kuwa ashindwe.
Mlevi na Mzinzi Mbowe Shindwa na Ulegee! !!
Nchi yetu ipone kwa kuwa na siasa safi na za kidemokrasia kuanzia ndani ya vyama.
Mbowe is a total man one and half.
Mbowe hanunuliki ni kamanda si kwa magwanda bali rohoni.A freedom fighter kama jina lake Freeman.
Husweka Lupango mara kwa mara lakini akitoka ni yule yule Mbowe wa jana na leo.
Raisi Magufuli katumia mkono wa chuma kumpelekesha kama ataunga tela wapi.
Vibaraka na vikaragosi wametumiwa kumkatisha tamaa lakini wakasahau ana roho ngumu kama Senator John McCain alipotekwa na kuteswa na KGB,huko Vietnam,wakimwahidi kumuachia huru akikili upumbavu waliokuwa wamemwandikia asome,akakataa kata kata.