Hakuna kitu kinatokea kwa bahati mbaya katika siasa ya Bongo


Mbowe is a total man one and half.
Mbowe hanunuliki ni kamanda si kwa magwanda bali rohoni.A freedom fighter kama jina lake Freeman.
Husweka Lupango mara kwa mara lakini akitoka ni yule yule Mbowe wa jana na leo.
Raisi Magufuli katumia mkono wa chuma kumpelekesha kama ataunga tela wapi.

Vibaraka na vikaragosi wametumiwa kumkatisha tamaa lakini wakasahau ana roho ngumu kama Senator John McCain alipotekwa na kuteswa na KGB,huko Vietnam,wakimwahidi kumuachia huru akikili upumbavu waliokuwa wamemwandikia asome,akakataa kata kata.
 
Hahahaa... Alipigiwa saluti na wala siyo mabomu!
Bosi wa TLP ambaye amewahi kuwa "Naibu Waziri Mkuu". Jamaa ambaye enzi hizo mimi napata akili aliwahi hamasisha tuandamane na mwishoni tukapigwa sisi na kwa macho yangu nikamuona anapanda gari ya RPC kwa kupigiwa saluti.
 
Maalimu kua kitengo hilo sijui lkn akiumwa ni lazima agharamiwe na SMZ sababu yeye alikua ni makamu wa raisi huko Zenji(kipindi cha Shein) na matibabu ni sehemu ya stahiki yake kama makamu wa rais mstaafu.


Maalimu akiugua anatibiwa kama wanavyotibiwa viongozi wengine maalim alishawahi kuwa makamu wa rais incase hujui
 
Mtu imara hanganganii Madaraka.
Angekua tishio wangeanza naye kabla ya Lisu.

Mbowe ingia hata kwenye Tweets zake au Kurasa zake za FB au hata hapa JF kama kuna jambo lolote la maana analoandika ukimlinganisha na Zito, au Lisu.
Hakuna kitu anachoandika chenya hamasa.

Mbowe hawezi kununulika kwa sababu anakula mil.300 kila Mwezi za ruzuku na michango mingine bila kufungwa au hata kunyongwa kwa kuhujumu pesa za walipa kodi.
Ukitaka ujue kuwa Mbowe anipigania chadema basi hata Lipumba anaipigania CUF mana naye hataki kung'atuka.Au Mrema na Cheyo . Hao wote wanapigiwa kura za kuendelea kuongoza vyama vyao.
Hakuna Mwenyekiti wa Chama chenye ruzuku anayeweza kukiuza wakati yeye ni Mbunge pia. Auze ili iweje wakati yeye ndiye kidume ndani ya chama.

Mnakosea sana kuwadanganya watu kuwa Chadema ni Mbowe ,bila mbowe Hakuna chadema. Mnakiua chama mana watu wasiompenda Mbowe wanakichukia mpaka Chama.
Ma ukweli ni kwamba Mbowe hakubaliki kabisa huko mitaani mana wanamuona kama MTU anayengangania Madaraka.
 
Maalimu akiugua anatibiwa kama wanavyotibiwa viongozi wengine maalim alishawahi kuwa makamu wa rais incase hujui

Miss Madeko
Nilikuwa sijui,nashukuru kwa kunifahamisha. Asante sana.
 
Hakuna cha kitabu wala nini. Waweke tume huru na kubadili katiba ndiyo utaijua hiyo nguvu ya hicho kijitabu.

Hio ni kurasa mojawapo ya hicho "kijitabu"

WANYIME TUME HURU
 
Kuna msemo ulivuma sana mwaka 2015 kwamba "CCM ina kitabu kikubwa cha MBINU ZA KUSHINDA UCHAGUZI na mpaka mwaka 2015 walikua ndo kwanza wako kurasa ya 3" kwahiyo bado kurasa kibao yaan Wapinzani wa nchi hii wajipange[emoji22][emoji22]
Mbinu za CCM ni tatu tu:

Polisi+TISS

TUME YA UCHAGUZI

MAHAKAMA TU.

Hivi vyombo vikiwa huru hata waweke mamluki laki moja wanaondoka madarakani.
 
Reactions: BAK
Kwa hiyo mbowe na lissu wamekuwa serious kiasi kwamba wanawaudhi Elite,

Mipango ya Elites inavurugwa na Akina mbowe, au wakaidi maelekezo ya Elites hivyo elites wameamua kuwaadhibu,

Mbowe anatembelea magongo
Na Lisu anachechemea
 
Wewe kama huna chuki binafsi labda una lako jambo.
CCM imetumia mabavu na pesa yetu kununua wabunge na viongozi wa CHADEMA tena kwa vitisho,bila aibu.
Hata siasa ya maelewano imewashinda,yaani mmefirizika kiasi mmegeuka mabubu wa hoja?
Hivi Mwl.Nyerere ndio shule ya siasa aliowafundisha ?

Juzi Mjumbe wa Halmashauri kuu kauliza Mwenyekiti wenu kwanini wazamiaji wanapewa vyeo kuliko CCM damu damu?Akajibiwa tena bila wasiwasi kwamba CCM damu damu hamna kitu ndio maanake anasajiri kutoka nje.Kwa majibu hayo bado unaona kuna kitu au mmegeuzwa fidodido?

Mbowe ana jenga chama hadi atakapomaliza kazi ya kuondoa mbegu mbovu na pandikizi.
Wewe unalia na Mbowe Mbowe kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Kutoka 1954 Nyrere ni mwenyekiti,hadi 1987 miaka 34 ni mwenyekiti,na hata baada ya kustaafu alikuwa na nguvu ndani ya chama kuliko mwenyekiti hadi kifo chake.
Au Historia ya Chama chenu imekupita kando?
 
Nyerere hakutawala wakati wa Mfumo wa vyama Vingi .
Pia Nyerere aliingia kwenye uenyekiti akiwa Mdogo sana.
Miaka 32 alikua mwenyekiti wa TANU. Lakini pia alikua na Mbinu kama alivuo Zito.
Alihamasisha vijana wakawa Jeuri kwa kua alikua anakubalika.

Mbowe nakuambia hata kijijini kwake hana ushawishi . Yani jimboni kweke anashindwa kufanya hata mikutano kama Mbunge. Amekaa Gerezani karibu miezi sita Hakuna hata kifaranga kilichoandamana kupinga uonevu. Na wakati alipokua Gerezani Chama kilitulia na hakuna hata MTU mmoja aliyakihama Chama.
Watu wanakihama Chama sio kwa sababu ya kununuliwa lakini watu wenye upeo mkubwa hawampendi Mbowe kabisa.
Wanaompenda Mbowe ni ama watu wachache sana wa kabila lake au wale wenye maslahi na Chama na wanaoona kuwa Mbowe ndiye Chama na akiondoka wataondoka naye mana ni wazi kuwa akitokea Mwenyekiti Mpya atakisafisha chama na kuwaacha pembeni wahuni na walevi wote wanaokitumia chama kwa manufaa yao.

Kweli unaona kuwa Mbowe yupo sirious na Chama wakati ameshindwa kuwahamasisha wanachama mamilioni wanopenda Mageuzi kujenga Ofisi za Kanda na za MAKAO MAKUU.
HIVI HUONI KUWA CHAKA KIKIWA NA Majengo yake ni rasilimali kubwa sana za Chama na ni sehemu ya kuwaunganisha watu pia. Hamasa ya ujenzi wa Chama ingewaleta watu pamoja na kukifanya Chama kuwa na Pamanent Address kila Jimbo na baadae Kila Kata na hata vijijini kote tena ni nafasi ya kupima uimara na Utayari wa wanachama katika kukijenga chama chao.

Chadema kinakosa mipango ya kukabiliana na CCM ya Magufuli kwa sababu ya akili ndogo ya Mbowe. Hivi kweli unaweza kusema kuwa Unaeneza dini kama ya Uislam au Ukristo halafu hujengi Msikiti wa kuswalia Kanisa !! Utakua Kichaa kama utakubaliana na Imamu au Mchungaji au Padri atakayewaambia waumini kuwa hakuna haja ya kujenga nyumba ya ibada kwa sababu waumini wanahitaji neno la Mungu tuu!!!

Mbowe hataki Kujenga na kuwekeza rasilimali za Chama kwa sababu ya roho Mbaya na kuona kuwa watakaonufaika ni wengine watakaoshika Chama. Miaka mitano bila harakati za Kisiasa fedha zimetumika kwenye mambo ya Hovyo badala ya kujenga miundo Mbinu ya Chama. Mbowe alikua haguswi na mfumo kwa sababu ni mmoja wapo wa watu waliotumiwa na kuhujumu watu ndani ya CCM kwa manufaa ya CCM. Mbowe kwa sasa anabanwa sio kwa sababu eti mpinzani wa kweli Bali ni kwa sababu Magufuli hataki mitandao ndani ya CCM ndio maana Mbowe anakosa kazi. Kazi ilikua kutumika kuwachafua watu. Kama unabisha angalia muda wote Mbowe anamwandama Magufuli tuu wakati walikua wanamsifia wakati akiwa Waziri na kumuona ndiye waziri mchapa Kazi.
Vipi Leo aonekane Mbaya wakati anafanya Yale Yale waliyokuwa wanayapigania.?jibu ni kwamba walikua wanatumika kuwachafua watu ndio maana walikua hawaguswi. Wakati Ule Mbowe alikua hakamati wala kukaa Gerezani. Slaa ndio alivunjwa mpaka mkono.
Mbowe anatamani awe na umaarufu wa Lisu lakini anaogopa risasi.Mwishowe imebidi ajiangushe kwenye ngazi baada ya kulewa Chakari. Dili lake la kujitangaza kuwa amevamiwa likabumburuka. Hapo eti ndiyo mikakati ya Mbowe ya kujijenga kisiasa!! Khatari ksana!
 
Gud analisis
 
Swala la kutumikia tumbo halikwepek.
 
J.Zoka yuko wapi siku hizi?[/QUOTE]Labda alipewa ubaloz
 
Maalim tangu enzi za jumbe kwenye ubora wake
 
Mkuu Nyerere alitawala tukiwa na mfumo wa vyama vingi.Yeye ndio alileta mfumo wa Chama kimmoja.
Lakini alipo ngatuka akataka mfumo wa vyama vingi.
Chadema si majengo,chadema ni utayari wa wanachama kuchukuwa dola.Kwani hayo majengo ,viwanja vya michezo na miradi inayomiliki CCM ni nguvu ya wananchi wote wakati ws chama kimmoja.
Hata Mwalimu wa Propaganda zenu naona anapwaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…