Hakuna kitu kinatokea kwa bahati mbaya katika siasa ya Bongo

Mkalamo
Sijui kwanini unatumia neno ujinga. Nimeeleza jinsi Mbowe alivyochezewa "shere" hiyo haimananishi yeye ni mpinzani wa kweli. Kuhusu kuifanya "serikali isipumue" watu wengi wamewahi fanya hivyo na sio wapinzani wa kweli. Kuna wabunge wa CCM wamewahi ilaza macho hii selikali bungeni na mabaraza ya mawaziri yalivunjwa mara kibao.
Hoja ya msingi ni je,kuna dhamira ya kweli kuelekea kushika dola katika harakati zao.
Kuna mtu amewahi "ilaza macho" selikali kama Mrema wa NCCR Mageuzi? Au ulikuwa mdogo?
 
Nishawahi kusema hapa JF kuwa ktk nchi zisizo za kibepari sanduku la kura haliwezi kukiondoa chama tawala madarakani na ikiwezekana basi nyuma yake kuna influences za mabeberu.
 
mwayena.
Kumwamini mtu hutegemea namna unavyotazama mambo na uelewa.
Siasa ina mengi kuielewa inahitaji usiwe kuku uwe tai.
Hapo Kenya Raisi ajaye 2022 ni Gideon Moi. Usishangae Ridhiwani Kikwete akapata wizara 2020 na akawa bosi wetu 2025.
Nimekuelewa Mkuu, hivyo katika siasa tunajifunza kwamba kile unachotegemea kinaeza Kisiwe na kinyume chake ni sawa.
 

Umeandika kinyume kabisa cha ukweli bila shaka ukitarajia bado nchi ina wajinga wengi wa kuaminishwa chochote.

Yaani umeshindwa hata kuona jinsi dola ilivyompuuza Zitto hata atoe kauli ya kuudhi kiasi gani kumhusu JPM wakati Mbowe na makada wengine wa CHADEMA wanavamiwa na polisi kila kukicha hata kwa kuhisiwa tu kuwa wanatarajiwa kutoa kauli za β€œkichochezi”.
 
Shida yenu mnaishi kwa kukariri maisha yaani mpaka muda huu hujaelewa unapoambiwa kuna elites na hao ndiyo waasisi wa vyama unavyoshabikia.
Pangusa macho yako kisha soma tena. Sina sehemu nimeandika chama chochote.
 
Utabiri wangu sasa umetimia. BM yupo ACT wazalendo atagombea uraisi wa Bongo. Bravo
 
Maalimu kua kitengo hilo sijui lkn akiumwa ni lazima agharamiwe na SMZ sababu yeye alikua ni makamu wa raisi huko Zenji(kipindi cha Shein) na matibabu ni sehemu ya stahiki yake kama makamu wa rais mstaafu.
Mng'ato
Naomba kukuhabarisha.
Ni rasmi sasa BM anagombea kupitia ACT na Maalim anagombea visiwani. Nafikiri sasa umefahamu mpango wa "Elites".
Wasaalam
 
Mng'ato
Naomba kukuhabarisha.
Ni rasmi sasa BM anagombea kupitia ACT na Maalim anagombea visiwani. Nafikiri sasa umefahamu mpango wa "Elites".
Wasaalam
Mkuu Membe hajawahi kunipa tabu,najua atafanya kazi kama ile ya Lowassa akimaliza atarudi zake kwao CCM.

Hio ya Maalim kua eagle ndio sikua na uhakika nayo na sijabisha kwamba ni mwenzao,lolote linawezekana tu.
 
Mkuu Membe hajawahi kunipa tabu,najua atafanya kazi kama ile ya Lowassa akimaliza atarudi zake kwao CCM.

Hio ya Maalim kua eagle ndio sikua na uhakika nayo na sijabisha kwamba ni mwenzao,lolote linawezekana tu.

Mng'ato
Ndio ujue sasa kuhusu Maalim. Sasa ni wazi wataenda tumia ilani "manifesto" moja kuomba kura za watanzania. Na watatumia hela za "elites" kuendesha siasa zao.
Watakaa kamati moja kujadili mambo yao na watashare mikakati yao.
Wasaalam
 
Mng'ato
Ndio ujue sasa kuhusu Maalim. Sasa ni wazi wataenda tumia ilani "manifesto" moja kuomba kura za watanzania. Na watatumia hela za "elites" kuendesha siasa zao.
Watakaa kamati moja kujadili mambo yao na watashare mikakati yao.
Wasaalam
Kiongozi hao hawanipi shida kabisa,maana kwa mfano huyo Membe kila mtu anajua kabisa motives behind yeye kugombea.

Maalim huyo atapambana na wazenji wenzake wakina Jussa.
 
eti ndugu zito na chama chake kichanga alitoa wapi pesa 2015 yaku mzungusha mgombea urais tanzania nzima? labda unajua
Mwalisi.
Pia muulize mgombea wa ACT Anna baada ya kugombea uraisi alienda wapi?
Je,alikuwa akimfahamu Mghwira kabla ya ACT? Au anafikiri Mghwira walimkuta tuu mtaani wakamwambia njoo ugombee uraisi wa ACT?
Mmewahi kujihangaisha kumjua Mghwira ni nani? Au alikuja kuja tuu kugombea.
 
kuna maswali mawili magumu wakinijibu ntashukulu
 
Ni Mungu tu ndio anayeweza kuvuruga mbinu za wenye mbinu safi na chafu .

Kila jambo na majira yake,
Bado inawezekana sana tu ukurasa mpya kutoka kitabu kipya chenye kusomeka TANZANIA MPYA yenye kuongozwa na CHAMA CHA UPINZANI.

Namwomba Mungu mabadiliko hayo yakitokea,YATOKEE KWA AMANI,KUSIWE NA UMWAGAJI WA DAMU KWA TAIFA LETU HILI ZURI.
 
Kuna msemo ulivuma sana mwaka 2015 kwamba "CCM ina kitabu kikubwa cha MBINU ZA KUSHINDA UCHAGUZI na mpaka mwaka 2015 walikua ndo kwanza wako kurasa ya 3" kwahiyo bado kurasa kibao yaan Wapinzani wa nchi hii wajipange😒😒
Kaandika uongo na wewe hutumii ubongo Hata kidogo? ENL aliondoka Kwa hasira na alirudi Kwa vitisho, huyo mwandishi ni conspiracy theories zisizo na akili.

Unawaamini CCM wana thinktank mujarabu, Hata T-shirt wanaiga CHADEMA? Ningemuelewa angeongelea tume na Vyombo vya dola lakini si vinginevyo, and, Tume na Vyombo vya dola sio permanent solution maana tuneona 2010 hawakuwa pro CCM unless wewe ni kinda ulikuwa huna akili 2010!
 
Naona umeungaunga ili uwe mtumwa wa hisia zako!
 
Acha ulevi, nani hajui kama Zitto alipewa chama na serikali kwa kumtumia msajili kumpora Limbu? Miaka yote mnapambana Mbowe aachie uenyekiti CDM...Sabaya amefanya nini Hai? ulitaka wamfanyie nini labda ndio uelewe kuwa kila walichopanga kinafeli!
 
Nilikuwa nimeamua kusoma comments tu lakini nilipokutana na hii ya kwako nikasema nije kukupigia salute Mkuu.

I salute you Mkuu.

Hakuna cha kitabu wala nini. Waweke tume huru na kubadili katiba ndiyo utaijua hiyo nguvu ya hicho kijitabu.
 
Naam Mkuu kabla ya saa tano asubuhi watakuwa wameshaachia dola na majimbo mengi kwenda upinzani ndiyo utakuwa mwisho wa hili genge la wahuni.

Na wao wanajua wakiruhusu tume huru asubuhi tu watakua wameaga pale magogoni.
 
πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘ŠπŸ½ Hakuna Elites wala mama yake Elites bali kuna UHUNI wa hali ya juu na UBABE kupitia vyombo vya dola.

Kama si vyombo vya dola kuibeba ccm naamini uchaguzi wa 2010 Chadema ingechukua Nchi.

Mkapa katoa wito wa kutaka Tume Huru lakini humsikii yoyote yule ndani ya ccm au Serikali kutia neno ama kuunga mkono hoja ya Mkapa au kuipinga bali wameamua kupiga kimya kwa kujua fika Tume Huru ndiyo KIAMA cha maccm.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…