Hakuna mkimbizi wa kisiasa aliyekimbia utawala wa Magufuli

Sidhani uilo jina John lina mkos. Walikuwepo mpaka Sasa tuna John wengi ambao ni watu wema. Labda majina kama pombe, magufuli, jiwe, kichaa, mzilankende etc.
 
Mathayo 2:13-17
 
Hamna anaweza mchafua marehemu ili wapate nn? Wala wafaidike Nini? Magufuli Alisha pita ila truth to be told kila mtu Ana azuri na mabaya magufuli Kuna mazuri Aliya fanya ila baya ambalo na amini nae aliomba msamaha kwa mungu kabla yakuaga Dunia ni kuleta tension na mkanganyiko wa kisiasa ndani ya nchi... Magufuli Ali pioneer ikaanza kuonekana kama wapinzani sio wa tanzania wala Hawana haki za kusema wanachojisikia kwa utashi wao.... That was so bad of him
 
Lema na Lissu sio wakimbizi wa kisiasa
 
Mngeyasema haya mara baada ya uchaguzi. Wasaidizi wakuu wa Mwendakule?
 
Toa taka taka zako hapa jamaa makonda na saabaya waliyoyatenda enzi za mwendazake unadhani walikuwa sahihi
 

Ingekuwa wewe Ni Lissu unelimwa zile risasi halafu mtu yeyote asikamatwe ungebaki nchini?
 

Lazima tukubali Kuna mazuri yalifanyika na mabaya yalifanyika kwenye utawala wa Magufuli.
 
Legacy iko chini ya mashambulizi makali kama Ukraine aisee,walioumizwa,tishiwa lazima waseme maana aliyewaminya kafa. Nanyi mliokuwa mnakula pepo zama hizo kazeni buti kutetea legacy, the truth shall set us free.w

Legacy iko chini ya mashambulizi makali kama Ukraine aisee,walioumizwa,tishiwa lazima waseme maana aliyewaminya kafa. Nanyi mliokuwa mnakula pepo zama hizo kazeni buti kutetea legacy, the truth shall set us free.
watapambana na legacy yenyewe maana legacy ya jamaa ni dude kubwa mno,hawa viazi wa upigaji wanajaribu kujinasibisha na wahanga wa utawala ule,wahanga nao kichwa kichwa wanajaa kwenye kapu hilo.
 
sabaya yuko mahakamani amani imerejea wote tuseme tawire.

akili zenu nyinyi watu ni duni sana.
 
Ingekuwa wewe Ni Lissu unelimwa zile risasi halafu mtu yeyote asikamatwe ungebaki nchini?
Mbona alirudi?
Yalyomkuta Mh. Lissu simwombei binadamu yeyote yule. Hata maadui zangu.

hatahivyo....

Ukweli ni kuwa hakuna mkimbizi wa kisiasa aliyekimbia utawala wake​

 
Jiwe aliruhusu kuua, kupoteza, kutisha, kupandikiza kesi, kupindisha sheria, kuharibu chaguzi zote - yaani kifupi jamaa hakufaa kuwa kiongozi wa nchi. Angeendelea miaka mingine 10 kama wafuasi wake walivyotaka basi nchi ingekuwa afadhali ya Somalia.

Kauli hii ya Serikali inatia moyo, ingawa bado ni giza nene waliotaka kumtoa roho Lissu.
 
H
Huwezi ukamtendea mwenzio ubaya halafu uendekuomba msamaha kwa Mungu. Lazima (yaani ni LAZIMA) Kwanza umuombe msamaha uliyemkosea. Labda kuzini na mke/ mme wa mtu, huwezi kumuombea msamaha uliyemdhulumu maana italeta tafrani zaidi ktk jamii. Hiyo unatubu tu kwa Mungu.

Magufuli alifanya maovu mengi- yeye binafsi au wasaidizi wake hawa kina Sabaya, Makonda etc. Yeye alikuwa kiongozi mkuu anawajibika kwa makosa waliyotenda wengine akayafumbia macho.

Aidha mengine yalitendwa kwa maagizo yake. Hatujawahi kusikia ameomba msamaha.

Nakubaliana na wewe kuwa Hakuna anayedhamiria kumchafua Magufuli, ila kudhani kwamba alitubu makosa yake hilo hapana. Hata kama alijarbu kutubu, alikosea procedure.
 
Ujinga wote Dr ulimboka yuko wapi au mwangosi yuko wapi unafikiri tumesahau nao wana ndg walipotezwa na akina nani always mnataka kuaminisha watu kuwa J.P.M ndo kipindi chake watu walipata kupotea sio kwa hawa waume zenu wapendwa
 
CCM wameishi kwa siasa za hivi, wenyewe kutengeneza upinzani wa regime zilizopita na kuaminisha umma kuwa aliyepita ndio tatizo.

Upinzani wetu nao feki wanaishi kwa propaganda hizo hizo! Kila awamu wanakimbizana na kutuhumu watu alafu baadae wanaungana nao.

Siasa zetu ni very complicated ni bora u focus kwenye ugali wako tu otherwise utakuja kuwa disappointed ujute.
 
Eti bad assailants! Papasi kbs ww!!! Kwa akili ya kawaida bad assailants wanaweza vamia eneo la kiserikal linandwa 24/7 na mitutu then intelligence yetu ni hiyo kama Taifa hatuko salama bas.
 
Wewe unastahili kuwa kuzimu kama Magufuli mwenyewe, unatia kimyaa na ni janga kwa taifa na aibu kwa familia yako!

Na kama ni mcha Mungu umemkosea Sana Mwenyezi Mungu kutamka kitu kama hicho kwa sababu kutokana na udhalimu wa John Pombe Joseph Magufuli uliokithiri ndio maana Mungu akaingilia kati kuamua Ugomvi ili kutunusuru waja wake na bahari itulie!

Naam na kweli ndicho tunachokishuhudia sasa, Bahari imetulia, wasiojulikana walizikwa na baba yao wanubatizo Chato, hakuna kutekana Tena, kukwapua pesa za watu kwenye mabenki hakuna, kesi za uchochezi, ugaidi na kutakatisha pesa hakuna, TRA ni taasisi rafiki kwa wafanya biashara, hatuogopi kutumia mitandao ya kijamii, nchi imefunguka, watalii wamerudi nk.

Duh Mungu atupe Nini walahi! Itoshe tu kusema Asante Mama SSH na kazi iendelee!
 

Hii nguvu ya kutetea wauaji mnatoa wapi….?
 
Ujinga wote Dr ulimboka yuko wapi au mwangosi yuko wapi unafikiri tumesahau nao wana ndg walipotezwa na akina nani always mnataka kuaminisha watu kuwa J.P.M ndo kipindi chake watu walipata kupotea sio kwa hawa waume zenu wapendwa
Huu ndiyo uzuri wa mijadala kwani hata hayo ya akina Dr Ulimboka na Mwangosi yanapaswa kujadiliwa pia ila uelewe hayo ya Kikwete hayasafishi udhalimu wa Magu na crew yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…