Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Hiyo mikoa maisha mdebwedo sana inawafaa wavivu na wajinga Maana hutumii akíli nyingi kuishi.

Tanzania ni DAR, ARU, MWZ na DDOM tu. Kwingineko tutakuja kutalii tu kipindi cha likizo kupanga natural air.
Sasa mbona huko mnakotumia akili nyingi Kuna maskini wa kutosha shida nini bwashee? Akili zinakuwa zimefikia mwisho au? 😀😀
 
Mkoa wa Mbeya umejaaliwa kila kitu unachokijua wewe..

Kwa hapa Tanzania sijaona Mkoa Mzuri wa Kuishi kushinda Mbeya..
Nikweli na naunga mkono hoja
4.Kilimo.

Mbeya Ina Ardhi nzuri ya kulima Kila aina ya zao kuanzia mbogamboga,matunda,nafaka Hadi pareto na chai.
Mchele wa Mbeya, Super Kyela ndio mchele wa grade 1.
Maharage ya Mbeya ndio maharage yanayoongoza kwa ulaini, kuyapika hadi yaive maji ni mara moja tuu!. Tena maharage yenyewe ya Mbeya, sio tuu ni maji mara moja bali pia ni matamu hayo!.
Kuna ubaya mmoja wa watu wa Mbeya hukuusema, hawana kabah, as a result watu wasio na kabah wanaitwa Wambeya na wanapenda umbea!.

Na kuna uzuri mmoja wa wanawake wa Mbeya, sio wachoyo, wana roho mzuri na kwenye yale mambo yetu yale, ni kama maharage ya Mbeya, maji mara moja!.

Na kwenye siasa, siasa za Mbeya ni very interesting, kwenye ubunge wa Mbeya mjini, nimewahi kuuliza "Maharage ya Mbeya maji mara moja" ni kauli ya kweli? Ni kwenye maharage tu au hadi kwa wanambeya? Kama kauli huumba, Jibu sahihi ni Oktoba 2020!
P
 
Mambo ya mchele wa Mbeya
 
Usisahau kuwa Mbeya ni kinara wa ufirauni

 
Tupo wengi ukichukua wastani Lazima tuoneka tupo Chini.

By the way kipenda Roho
hula myama mbichi. Ila Tanzania ni mikoa niliyokutajia Kwa huduma za uhakika
Mko wengi ila mnazalisha kidogo Kwa Lugha rahisi ni kwamba mumeishiwa akili na wavivu.
 
Nimesema along the road.
Mbeya hakuna pulling factor ktk mji.
Mwanza kuna ziwa linaloleta utitiri wa watu. Kuna viwanda vya samaki, biashara ipo juu. Ni center ya mikoa ya Shy, Kagera, Mara, Tabora, Singida nk.
Mbeya ipo pembezoni sana watu wa Njombe ndio wamejaa. Mwanza iache tu kama ilivyo mbeya haitakuja kuifikia.
Mbeya asilimia kubwa wanategemea kilimo cha kujikimu, hawana ufugaji mkubwa,wala uvuvi, viwanda vichache sana kulinganisha na majiji mengine.
 
Kigoma,Ukerewe,Bukoba Kuna Ziwa vipi mbona watu hawajakaa? Mtwara na Tanga Kuna bahari Kwa nini pulling factor ya bahari haijawavuta?😁😁

Acha porojo sababu nilizokupa ndio za kitaalamu.
 
Mbeya bana, napapenda sana hasa wilaya ya kyera, vijiji vya kule kwao Prof. Mwandosya hadi kule Mwakaleli -Tukuyu hii.

Hali ya hewa unaweza ukaishi kule usijue kama kuna dasalama, wanakijiji wa huko siyo wachoyo mtu akiwa na ng'ombe au kuku wanahakikisha na wewe unapewa ili ufuge, yaani maziwa na mayai kule ni kama ugali/maharagwe jera au boding skuli.

Pale Mwakaleli muda wa jua kupunga ni saa 5 kwenda saa 6 tena linaonekana kwa 45min ukilikosa hadi kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…