Hakuna namna ya kumshurutisha Mungu ili aje arekebishe hizi 'bugs' zilizotokea kwenye uumbaji wake?

Hakuna namna ya kumshurutisha Mungu ili aje arekebishe hizi 'bugs' zilizotokea kwenye uumbaji wake?

Mkuu Mungu ndo alikuwepo kabla ya chochote kwa mujibu wa imani.

Na uwezo wa kuzuia yote hayo yasiwepo anao/alikuwa nao.

Lakini pia alijua yatakuwepo pamoja na impact yake.

Sasa kwa nini aliruhusu mimi sijui [emoji848]
Aliwapa baadhi ya viumbe wake uhuru wa kuchagua. Ni jambo zuri sana.
 
Hizo ni kazi za shetani
Sikumbuki kama shetani aliwahi kuumba kitu chochote kwa mujibu wa hekaya za dini. Hivyo, kila kitu ni cha Mungu. Mfano, ubaguzi. Ni kwanini waarabu na wazungu walitupachika majina yao na kuleta dini zao huku wakikataa na kuua yetu na zetu? Ufisadi, ni kwanini dini zinachuma fedha kwa watu wetu wakati miungu yao wanasema ni tajiri na ina uwezo? Mauaji pia ni kazi ya Mungu hasa ikizingatiwa kuwa ndiye aliyeumba kila kitu. Hata ukabila ni kazi ya mungu hasa ikizingatiwa alipendelea baadhi ya makabila na kuyachukia mengine. Ikija kwenye vita ndo usiseme. Dini zote zimeshiriki vita mojawapo ikiwa ni ile ya kueneza ukoloni Afrika ili kuendelea kutunyonya na kutuibia. Hivyo, malalamiko yako mwanangu yaelekeze kwa mwenyewe muumbaji.
 
Aliwapa baadhi ya viumbe wake uhuru wa kuchagua. Ni jambo zuri sana
Tunaamrishwa kuchagua yaliyo mema na si vinginevyo.

Sababu ni kwamba ukienda kinyume/kutenda mabaya utaadhibiwa.

Maana yake tunatakiwa kufanya yaliyo mema tu.

Ndo maana ya adhabu.
 
Hayo nimadogo mno Mungu kuingilia. Mungu anaingilia mambo makubwa kama dunia kugongwa na sayari nyingine ama kumezwa na manyota makubwa zaidi kuliko jua. Mungu analinda vitu vingi kiasi kwamba haya matatizo nimadogo sana kuyaona maana yananafasi chini ya 0.0000000000000000000000000000001 ya mambo yanayomkabili anayotakiwa kurekebisha. Jiulize kila nyota nijua na inamasayari huenda yakawa na viumbe na kuna matilioni ya manyota na yote anayalinda
Anayalindaje sasa ?
 
Siyo kwamba hapati burudani, yoooote hayo Mungu kakupa wewe utashi wa kuchagua JEMA ama BAYA, sasa kama wewe umechagua JEMA na mwenzako kachagua BAYA, mtashirikiana vipi kwenye meza moja kusukuma maendeleo ya aina yote ile??

Changamoto ni kwamba, kwenye jamii yetu kuna michanganyo wa kutosha kiasi kwamba mengine yamekuwa shida kwa wengine na kwa wengine siyo shida
Ukizaliwa huna figo ama unaishi mara magonjwa hayo sijui kongosho, utumbo umeoza, sijui moyo umevimba hapo choice inakuaje
 
Huko kutest mnafananisha Mungu mkuu na mwadamu.

Unapotest maana yake huna uhakika, ina maana Mungu hana uhakika na uumbaji wake?
Mungu hajakuumba kama makazi yako ya kudumu hapa Duniani, kulielewa hili inabidi usome ugomvi wa mwanadamu na shetani. Upo hapa duniani kama mapito tu.

Mitume wote ambao ni vipenzi vya mwenyezi Mungu wamepata shida, Kina Ibrahim walichomwa moto, yusuph alitupwa kwenye kisima na baadae kufungwa, Musa aliwindwa karibia maisha yake yote, Ayubu alikuwa na ugonjwa usiopona, Yona akaliwa na samaki, Nuhu na safina etc.

Kifupi mkuu tabu, shida, vita, na mengineyo ni moja kati ya mitihani mwenyeZ Mungu ametuumbia, na mwenyeZ Mungu ndio mlipaji mkubwa, shida zote utakazozipata hapa duniani na kuvumilia na kumtegemea yeye basi atakulipa siku ya mwisho.
 
  • Vita
  • Ufisadi
  • Tozo
  • Mauaji
  • Ukabila
  • Uchawi
  • Wizi
  • Ukahaba
  • Makafara
  • Husda
  • Usengenyaji
  • Utapeli

List goes on...
Mkuu ; hebu zitazame vizuri hizo na uzione kama ni FURSA. Kwa mfano vita- ingekuwaje watengenezaji/viwanda vya silaha, ajira za Wanajeshi (including Police)n.k. wangepata wapi kula yao(earn their living) hakuna biashara/hakuna ajira.
au labda tuseme Wizi; kusingekuwa na wezi basi wauzaji wa nondo na watengenezaji Grills wangekosa kazi, watu wasingelikuwa waangalifu kwa mali zao, Ajira za walinzi binafsi ingekuwa hakuna , list goes on.......
Acha Mungu aitwe Mungu aisee.
 
ibilisi yupo kazini, Anaanzisha kisha anatoa comments yeye mwenyewe ili kuvuta na kupotosha watu wa Mungu kwa kigezo cha "uhuru wa kuongea".

Na aturehemu Mungu Mwenyewe maana sisi tu wadhambi na wachafu sana katika fikra, matendo na roho.

Tusamehee Ee Mungu na Bwana wetu.
 
Hiyo imekaa poa. Kwa Wakristo(na yeyote anayependa) soma Marko 7: 18-23.
 
Mungu hajakuumba kama makazi yako ya kudumu hapa Duniani, kulielewa hili inabidi usome ugomvi wa mwanadamu na shetani. Upo hapa duniani kama mapito tu.

Mitume wote ambao ni vipenzi vya mwenyezi Mungu wamepata shida, Kina Ibrahim walichomwa moto, yusuph alitupwa kwenye kisima na baadae kufungwa, Musa aliwindwa karibia maisha yake yote, Ayubu alikuwa na ugonjwa usiopona, Yona akaliwa na samaki, Nuhu na safina etc.

Kifupi mkuu tabu, shida, vita, na mengineyo ni moja kati ya mitihani mwenyeZ Mungu ametuumbia, na mwenyeZ Mungu ndio mlipaji mkubwa, shida zote utakazozipata hapa duniani na kuvumilia na kumtegemea yeye basi atakulipa siku ya mwisho.
Nakuelewa mkuu mitihani ipo na kiimani ni Mungu mwenyewe ndo aliileta ili tuipote na kufuzu.

Swali linakuja kwa nini aweke mitihani kwa viumbe wake ilhali yeye ni mkamilifu?

Shuleni tunapewa mitihani kama namna ya kutupima kama tumeelewa somo, ni namna ya walimu (wanaadamu wasio wakamilifu) kujihakikishia kile walichofundisha kimeeleweka.

Mungu kutupa sisi mitihani ni kama vile hana hakika na kile alichokiumba kama kitamtii au la.

Kwa nini iwe hivyo wakati ni yeye ni mkamilifu asiye na kasoro?
 
Back
Top Bottom