Hakuna Taifa lililoendelea kwa kujipendekeza na kujidharau

Yani Kenya ni nchi maskini walitakiwa rais wao aje Tanzania kujitambulisha.. Kwanza Kenya haijapata uhuru
 
Aisee! Uelewa wako wa nchi za nje una short circuit. Ebu jitathmini tena!
 
Mtaishia kubweka tu lkn kazi inasonga na majirani zetu tayari wameshuhudia kuwa mama Samia ndiye kiongozi bora .
Ha ha ha, si kubweka ni mawazo na maoni. Hapa unapigia mbuzi gitaa. Unachojumuisha watu kimakundi na kitimu mie hata siwaelewi natoa mawazo kwa utashi wangu. Endelea na ngoma zako
 
anacho jaribu kuwakilisha muandishi ni kwamba tusiwe tegemezi. tujikwamue kwa jituhada zetu
Kuwa tegemezi ni ile tabia ya ama kuomba au kusubiri kusaidiwa, lakini kukaribisha wawekezaji sio utegemezi, kuwa na wawekezaji wengi kunaongeza tax base, kunaongeza fursa za ajira na many other multiplier effects, tusijifungie sana
 
Naona ndugu yangu unaiona Kenya kama tajiri sana. mfumo wao ni wakibepari toka zamani. Lakini Kenya kuna masiki wa kutupwa kuliko Tanzania. Watu wengi wanalia uhaba wa ardhi. Kenya naijua toka utoto nimekulia Kenya baadae nikarudi Tanzania kisha nikaenda kusoma huko. Kwa upande mwingine nina asili ya hkuo na ndugu zangu. Japo mimi ni mtanzania.
Kenyatta hakufuata njia halali za kujimilikisha, ndiyo maana alikuwa katika vita kubwa na Jaromongi odinga, ambae alikataa mfumo wa Utawala wake, na Ouko, ambae aliuwawa kimazingira tu. hadi leo wakenya hawapendi huo mfumo.
Swala la ardhi tanzania liko sawa na nchi za scandinavia, ardhi ni yaserikali na mtu upewa dhamana ya kumiliki hiyo ardhi. Mbona haijaathiri uchumi wa nchi za scandinavia. Ambazo zilikuwa na mwelekeo wa kijamaa zaidi. Hasa sweden. Hivyo sidhani kwamba ardhi ni shida kwa sera za kitanzania.
Si kwamba Kenya wanatuzidi kiihivyo. ni mazidiano ya kwaida kama ilivyo, Norway wanaizidi Sweden na nimajirani ambao wanakizana kiuchimi. Hiyo ni kawaida. lakini haijatupa kutufanya sisi watanzania kuwanyenyekea wakenya na kuwabembeleza.
Hivi slum kubwa Africa unajua ipo wapi na ni kwanini? Tanzania ulishaona hiyo slum kubwa kiasi hicho? Hatujafikia hapo kuwaona waKenya kama miungu watu.
 
Tatizo ni umasikini uliosababishwa na viongozi, wananchi hawawezi kuwa confidence wakati wana njaa na pesa hawana, wakijaribu kupata pesa wanafilisiwa, tangu nchi imepata uhuru Serikali inaona matajiri kama mashetani au wahaini, Hakuna nchi masikini au waty masikini wanaheshimika popote duniani, Watu wanaotoka kwenye mabara mengine ukiwauliza wanaona nini wanapokutana na Waafrika jibu ni wanaona umasikini. Umasikini ni Laana, na utajiri ni Baraka kutoka kwa Mungu
 
Swali hao matajiri walipataje utajiri wao kihalali au kuuibia serikali. Mbona matajiri kama Bakheresa akina Dewji biashara yao ni halali na hatuwasikii wakilalamika au kusema wanaonewa. Wala kusikia wanakwepa kodi. Tanzania kuna matajiri wengi waliokula fedha ya serikali isivyokihalali na wengine kuhusika na madawa ya kulevya.
Nchini Sweden kuna makampuni Makubwa yalibanwa kodi na serikali wakaamua kukimbia nchi, lakini baadae walirejea kwani hata huko walikokwenda walibanwa. Watanzania matajiri wanachukia kodi hasa wale wanaojua wanafanya biashara kijanjanja.
Watanzania tubadilike tulipe kodi. Tusipende dezo. Kodi ndiyo itabadili maisha yetu.
 
Magufuli hakuwa la Rais, yule naisi aliletwa kuharibu nchi yetu
 
Hii Misukule ya JPM inaboa sana!

Unajua hawa wehu kinachowauma ni kuona Samia anafanya yale ambayo JPM alikuwa hafanyi!!

Yaani yakiona Samia anafanya yale ambayo Jiwe alikuwa hafanyi basi inaona Samia anamtoa kasoro JPM, wakati wao wanaamini Jiwe ni Mungu Mtu ambae wakati wote alikuwa sahihi!!!

Walivyo Mazuzu, wanasahau kwamba wanaipa KE credit ambayo wala hastahili, manake wanaichukulia KE kama Beberu fulani hivi lenye maguvu na uwezo wa kutupoteza kabisa!!

Kila nikijiuliza hivi hii KE wanayoigopa namna hii imewahi kuirarua rarua na kuifunika nchi ipi wala sipati jibu; na hapo ndipo nakuja kubaini kumbe ni vile tu wanataka Samia aendeleze yote ya JPM... mazuri na ya kipumbavu!
 
Hakuna mwenye haja yakutaka kujua matatizo ya kenya maana hayo hayatuhusu tunachotakiwa sisi kujua na kukifanyia kazi ni tutanufaikaje na rasilimali tulizonazo na ujirani wetu na kenya.Haya ndo mambo tunapaswa kujadili kwa kina sio hizo porojo zingine unazoleta maana unazileta kwa mtazamo wako binafsi na hayo ni maisha ya wakenya na lazima ujue hakuna nchi ambayo haina matatizo yake ya ndani kwa wananchi wake.
 
Mnawasifia sana na ndiyo mnaochukulia mfano. Ndo maana nikaeleza mtazamo wa maisha yao. Sijakurupuka. Na si mtazamo wangu hiyo ni reality. Rasilimali zimekuwepo, ndo hao hao waKenya wamekuwa wakiwaibia. Kenye iliongoza uuzaji wa Tanzanite. Kenya ilelita watalii kutumia mbuga na mlima Kilimanjaro bila kulipa kodi. Leo ndo unasema kutumia raslimali.
Inahitaji tubadilike Kifkira, bado tumefungwa na kumwabudu Kenya. Shida si rasilimali, bali Fikra. Ukikomboleka kifkra, na utaanza jua maendeleo siyo kila siku kumwabudu huyo Kenya wenu.
 
Tatizo watu mliaminishwa kuwa maendeleo ni vitu na ubabe ndio ubora.

Sasa leo hii mnapewa somo kamili la ni nini maana ya neno maendeleo naona mnaanza kuweweseka
 
Paragraph iko wapi wewe mbuzi.


Mimi naona lundo la maandishi. Takataka kabisa
 
Swali ni Nani aliewatetemekea?? Ujue Kuna mambo ni yakipuuzi Sana...uko kuwatetemekea ni kukoje acheni siasa za kale za kipuuzi ambaz hazijengi chchte zaidizaid zinaukiza wananchi ambao biashara na kazi zao zinamuingiliano na hilo taifa...mama kafanya heko Sana wafanyabiashara wa mahindi walikuwa wana stress na hali mbaya kisa ubabe uchwara.....
 
Lakini unaposema tumejishusha una maan gani na wapi tulipojishusha?? Wapi tulipojidharau
 
Haya. Tumekusikia. Unanung'unika, kuuma na kupuliza. Mataga na wana-Lumumba mupo na hoja?
 
Wengi hawatakuelewa ila umesema ukweli tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…