Hakuna Taifa lililoendelea kwa kujipendekeza na kujidharau

Mambo mengine uliyoyaandika au hujui au hutaki kufuatilia ili ujue.

China chini ya sera za kujifungia za Mao, iliendelea kuwa maskini kwa miaka mingi. Wachina walikuwa mpaka wanavaa nguo zenye viraka.

Maendeleo makubwa ya China, yametokea kuanzia miaka ya 1990 baada ya kuruhusu uwekezaji wa nje. Makampuni makubwa toka America, Ulaya na Australia yalienda kuwekeza China. Ndipo uchumi wa China ulianza kukua kwa kasi.

Mpaka leo, China ndiyo inayoongoza katika kuvutia uwekezaji toka Ulaya na America. Kila mwaka China inapata uwekezaji wa nje unaofikia thamqni ya dola bilioni 80.

Katika makampuni makubwa kabisa 10 nchini China, kampuni ya China ni moja tu, Huawei. Mengine yote ni makampuni ya Ulaya na America.

Hakuna nchi hata moja Duniani aliyowahi kupata maendeleo ya haraka bila ya kuruhusu uwekezaji wa nje.

Ni Uingereza ndiyo iliyowekeza America enzi za Utumwa. Ni Ufaransa iliyoenda kuwekeza Canada. Ni Canada na Uingereza zilienda kuwekeza Australia. Ni US iliyoenda kuwekeza Ujerumani na South Korea. North Korea, mpaka leo, watu wao wanahangaika hata namna ya kupata chakula kutokana na kushindwa kuchangamanisha.
 
Two wrongs never make a right...Na watoto wa marehemu ni wengi mkumbuke nao pia ni wapiga kura...Twendeni polepole...Tutengeneze umoja wa nchi na tulinde maslahi ya nchi kwa faida ya kila mtu...Kama alivyomaliza mwenda zake na wengine pia wajifunze cheo ni dhamana!
 
Kama china ingeingia kwenye kutojifungia isingelalamikiwa kwa kuvunja haki za binadamu...Mpaka leo China ina mambo ambayo haijayafungua...Hakuna nchi ambayo ilianza kwakujiweka wazi...Hata uingereza unayoisifu kuna wakati ilikuwa na sheria kali za kufanya kazi hadi wazungu wakachukia ukristo...Walibeba mawe mazito kujenga majengo makubwa, reli etc
 
H
Uhusiano upi ulikuokuwa umearibika? mbona timemwona Kinyatta akija hapa mala mbili na tukampa tausi!kuna nchi gani iliyovunja ubarozi na Tanzania wakati wa Magufuri? Mwambie mama yenu aache kujipendekeza ,asara nikubwa kuliko faida.
 
H

Uhusiano upi ulikuokuwa umearibika? mbona timemwona Kinyatta akija hapa mala mbili na tukampa tausi!kuna nchi gani iliyovunja ubarozi na Tanzania wakati wa Magufuri? Mwambie mama yenu aache kujipendekeza ,asara nikubwa kuliko faida.
Hasara mlizo tusababishia ilibidi muda huu muwe korokoroni.

Na rais ataendelea kufagia uchafu woote .
 
Hasara mlizo tusababishia ilibidi muda huu muwe korokoroni.

Na rais ataendelea kufagia uchafu woote .
Tanzania imepiga atua kubwa Kiuchumi na Kimiundombinu,katika utawala wa Magufuri,pasipo kuwapigia magoti hao manyangau na Mabeberu na mambo yakawa sawa, alichokifanya Magufuri ni kujenga ukuta ili wasiweze iba madini yetu,na yakawa mafanikio makubwa kwa Jpm, wakati Magufuri anaingia madarakani kenya alikuwa wanaongoza kwa GDP 100 na Tanzania GDP 45, miaka mitano tu Tanzania ilfikia GDP 70 kutoka 45, Apo amna msaada wa mabeberu ni akili tu, Alafu inasema Magufuri kafanya uhalibifu,nikwatakwimu zipi hizo?
 
CAG report inajionyesha.
Majirani hakuna aliyekuwa karibu naye hata kina Kagame na m7 hawakuja kumzika.

Mama leo hii kaona haifai kuishi na majirani bila maelewano na wafanya biashara wa mazao kama mahindi yaliyo kuwa yamezuiliwa mpakani sasa swaaafiiiii .
 
Kwa taarifa yako wanufaika wote wa Mwendazake including wanaojiita wanyonge, tunawaita wasukuma
 
Miundo mbinu ipi imejengwa Rais akiwa Magufuli? Iweke hapa halafu tutakuambia nani aliyafuta fedha au nani alianzisha?

Huu ushamba wa kusema Magufuli aliimarisha miundombinu wakati alimalizia tu kazi za wenzie lazima tuukomeshe. Taja sasa
 
Wala sijakosea, maana ndiyo wanashangilia vitendo viovu vya Mwendazake
 
SI
Miundo mbinu ipi imejengwa Rais akiwa Magufuli? Iweke hapa halafu tutakuambia nani aliyafuta fedha au nani alianzisha?

Huu ushamba wa kusema Magufuli aliimarisha miundombinu wakati alimalizia tu kazi za wenzie lazima tuukomeshe. Taja sasa
Siwezi bishana na njinga anataka kila kitu kutafutiwa,inaonekana wewe bado unaishi kwa baba yako,bado unaakili tegemezi, Tafuta lipoti za ADB,WB na AIFM liport 2019-2020, uwe unashugurisha ubongo wako,sio kila kitu kusimuliwa na baba.
 
Siku zote lazima ujifunze kwa waliotangulia. Kenya walishatangulia. Lazima tuangalie njia walizopita.

Ukiwa na jeuri kama ya Jiwe Ndio hayo ya kujiaminisha ujinga mwisho wa siku unaanza kuitumbukiza nchi kwenye shimo
Hakuwa sawa yule Mzee katika kuhandle issues za diplomacy. Ila sio kila kitu tukivamie kichwa kichwa. Tutapigwa sasa hivi
 
SI

Siwezi bishana na njinga anataka kila kitu kutafutiwa,inaonekana wewe bado unaishi kwa baba yako,bado unaakili tegemezi, Tafuta lipoti za ADB,WB na AIFM liport 2019-2020, uwe unashugurisha ubongo wako,sio kila kitu kusimuliwa na baba.
Yaani nitafute ripoti za WB wakati ninajuwa kuanzia Nyerere alifanya nini, nakuwa Mwinyi alijenga kitu gani, mchango wa Mkapa ninaujua na kazi ya Kikwette hatujaisahau.

Huyu mshamba amewajaza ujinga na wajinga mkajaa. Amejisifia uwongo akiwa hai, na mapunguani mnaendelea kumwabudu. Pumbafu kabisa
 
Mzunguko wa pesa haupo mtaani jamani, me nachokiomba pesa zipatikane ili hali isiwe mbaya zaidi hayo mengine ya kuwa na utajiri wa kukupita ni kujirisha upepo duniani tunapita tu
 
una uhakika asilimia100% North Korea wanahangaika kupata chakula?
 
Huyu jiwe huyu aliharibu sana watanzania maana walidhan bado tupo zama za kale za mawe

Huwezi kujifanya mbabe wakati had toilet papers unategemea uagize nje , na kiburi cha kipumbavu na misimamo ya kipuuzi ndiyo iliyo leo tunasomeka miongoni mwa mataifa masikini.
 
Huyo anayewasifia wakenya ni wale wavivu wakufikiri.Ninachokijua ni kwamba sisi ndio ambao tumezubaa ndo maana wakenya wanaonekana ni bora kati yetu sasa ilo ni tatizo letu,tunachotakiwa ni sisi tubadilike ili tuingie kwenye ulimwengu wa ushindani kwenye kila nyanja na hilo litatupa nafasi yakurekebisha ujinga mwingi ambao tumeufanya uko nyuma.Mambo yote unayoyalalamikia ni mambo ambayo yametokana na uzoba wetu lakini pia mimi sidhani kama nchi hii haina watu wenye upeo wakutosha wakujadili mambo kwa kina kwa maslahi ya taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…