Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Nilishawahi kufika Mafinga tena ilikuwa ni July aisee nilioga siku ya kwanza tu siku zingine 5 sikuoga nilifikia pale Lutheran VTC baridi mnoo kwanza niliposhuka tu kwenye gari nikaitupa ile juice niliyoinunua nikanunua gloves na mzura lakini wapiii mpaka naondoka pale nikaenda kuoga Mbeya mjini, na kuna sehemu kule Mbeya kama unaenda Tunduma panaitwa kwa Mpemba napo ni 🥶
Mafinga hapo mjini cha mtoto ukitaka balaa ingia ndani huko ndo utakutana na balaa lenyewe .
 
Niliwah kukaa hapo nikiwa shule Kwa miaka 4, nikaja kupita last year, baridi imepungua sn compare na those days 2000 - 2005, nakumbuka mvua za barafu zilikuwa zinanyesha Mpaka teacher anasimamisha kipindi but now namiss sn kuishi maeneo hayo Mishe Tu zinatubana huku Dar, ( Kawawa JKT)

Kama baridi la Sasa liko hivi sijui ilikuwaje Miaka Kumi na tano iliyopita àmbayo umeitaja

NI hatari Sana hasa Kwa Kazi kama bodaboda
 
Niliwahi kulala pale Njombe nikaagiza chai mimi nikabugia kwa sababu sikuona ikitoa moshi, kuja kuamka asubuhi mdomoni nimejaa vidonda kama vyote kumbe ilikuwa ya moto na mimi sikuhisi chochote kwa sababu ya baridi kali

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
Kuna siku nimetoka DSM nawahi Njombe nikapanda IT nimeshuka Makambako saa 7 usiku ,,,halafu nilitoka na sweta la kibishoo ile siku nilikoma nililala na viatu gesti yaani noma aisee.
 
Niliwahi kulala pale Njombe nikaagiza chai mimi nikabugia kwa sababu sikuona ikitoa moshi, kuja kuamka asubuhi mdomoni nimejaa vidonda kama vyote kumbe ilikuwa ya moto na mimi sikuhisi chochote kwa sababu ya baridi kali

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app

Pole Sana Mkûu.
Ukitaka uifaidi ya Mafinga au njombe Njoo Bila tàarifa za huku, alafu ukose hotel au lodge Aiseeh! Utaimba sauti ya tano
 
1. Tembea duniani ukutane na baridi. Ya Mafinga cha mtoto.

2. Niliwahi kuishi Lesotho baridi mpaka Maji kwenye mabomba yanaganda. Mambomba hayatoi maji.
kwa hiyo mwendo wa kunikishana vikwapa tuu usubuhi
 
Back
Top Bottom