Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Mafinga ni habari nyingine Nina experience napo kimsingi usemacho ni kweli kabisa Kuna Uzi wangu humu nilishawahi kuomba msaada wa blanket

Uliomba blanket mkuu😄😄 ulifanikiwa?
 
Kuna siku nimetoka DSM nawahi Njombe nikapanda IT nimeshuka Makambako saa 7 usiku ,,,halafu nilitoka na sweta la kibishoo ile siku nilikoma nililala na viatu gesti yaani noma aisee.
Bahati mbaya ilikuwa ni siku yangu ya kwanza sikubeba hata sweta nilikuwa natetemeka kama kinda la ndege

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Sogea Makambako utaandika uzi wenye paragraph 200 kuhusu bodaboda wa Makambako kitovu cha baridi
Kwenye swala la uaminifu Mafinga nawapa 90 hiyo 70 ni ndogo nakumbuka nikiwa nataka usafiri nawapaga magenti wale pesa nawachia na namba yangu ya simu sina hata tiketi lakini gari ikikaribia wananipigia jamaa wale walikua hawana kabisa tamaa ndogo ndogo.
 
Sasa kuna siku nimeshuka pale mafinga...
Nikasahau begi kwa gari..
Nikachukua boda sasa nakuta boda kavaa elements ina manguo nguo mengi kichwani sikujua bana..

Alipoanza kufukuza gari mkuu weeee weee ile show nikasema kule si pa kuchezea
Uliona km anakuletea ubishoo 😂
 
Baridi la Mafinga huwa Kali mwezi wa sita, WA7 na wa8 mwanzoni. Sisi ambao tumekaa kule na kusoma kule miaka ya 90 baridi lilikuwa kali tofauti na vile ilivyo sasa ndiyo maana nyumba zetu ilikuwa ujenzi wake ni muhimu kuweka sehemu ya kuwasha moto sebuleni ili kutengeneza joto. Sisi shuleni tulikuwa tunaanza kushika pencil saa nne asubuhi​
 
Umenikumbusha shule ya watoto inaitwa Southern highland,ipo mafinga..halafu bweni kuanzia vidudu.baridi lile hapana..
Unakuta huko vijijini ndani ndani kuna lile nardi la hatari mfano makete au kitulo huko...

Unakuta watoto bado wanatembea peku
 
Back
Top Bottom