Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Ukweli tuuseme tu, jahazi limeanza kumshinda mama. Sio kwa ugumu wa maisha huu!
Yaani Watanzania wanatozwa tozo ambazo hata mkoloni na roho yake mbaya asingethubutu kuwatendea namna hiyo.
Wengi wetu vipato vyetu ni vilevile, lakini gharama za maisha zimepata mara dufu! Kwa lugha rahisi tumekuwa masikini zaidi.
Ni tozo tozo tozo kila kona, wakati huohuo kila kitu kimepanda bei, uwezo wa kufikiri wa mheshimiwa waziri wetu wa fedha umegota kwenye tozo tu. Yeye na timu yake kila wakiumiza vichwa bado jibu lao ni tozo zaidi!
Ni nani anayenufaika na hali hii? Au ndio wale wafanyabishara walioitia 'sirikali' mfukoni wa awamu ilee wamerudi kukusanya vyote walivyopoteza wakati wa JPM?
RIP JPM.