Hali ni mbaya, Watanzania wengi wamekuwa masikini zaidi awamu hii ya sita

Hali ni mbaya, Watanzania wengi wamekuwa masikini zaidi awamu hii ya sita

Upumbavu mtupu. Aya ya mwisho ndio imeanika upumbavu wako wa wazi wazi
Ni ukweli ulio wazi kuwa matatizo haya hayakuwapo wakati wa JPM, sio unafiki, siri wala kificho. Inawezekana Mpango alikuwa waziri bora kuliko Nchemba au JPM alikuwa rais bora kuliko huyu wa sasa. All in all rais ndio kiongozi wa serikali, kwahiyo haya yote kayaleta mama.
 
Madelu hawezi ku manage uchumi, huwezi kuendesha nchi kwa kutegemea kuokoteza tozo......uchumi unajengwa kwa sera bora jumuishi za kiuchumi na fikra sahihi. Siyo kukusanya tozo na kufuja kwenye matumizi ya anasa ya magari ya kifahari na misafara iliyosheheni viieite......
 
Halafu kuna wengine wanaagizwa wajipimie😁😁😁

Tozo zipi hizo ambazo zinakufanya kuwa maskini?

Bora hata ulivyosema kupanda Kwa Bei,hata hivyo kupanda bei Kwa vitu ni faida kwa wauzaji lakini huwa shida ikiwa watu hawana uwezo wa kununua..

Mwisho kama bia zinazidi kuuzika na watu wanajaa Bar,kumbe maisha sio magumu kwa kiasi hicho.
Mithali 31-6: "Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini."

Baa tunaenda kujisahaulisha machungu ya uchumi wa awamu ya 6.
 
Ukweli tuuseme tu, jahazi limeanza kumshinda mama. Sio kwa ugumu wa maisha huu!

Yaani watanzania wanatozwa tozo ambazo hata mkoloni na roho yake mbaya asingethubutu kuwatendea namna hiyo.

Wengi wetu vipato vyetu ni vilevile, lakini gharama za maisha zimepata mara dufu! Kwa lugha rahisi tumekuwa masikini zaidi.

Ni tozo tozo tozo kila kona, wakati huohuo kila kitu kimepanda bei, uwezo wa kufikiri wa mheshimiwa waziri wetu wa fedha umegota kwenye tozo tu. Yeye na timu yake kila wakiumiza vichwa bado jibu lao ni tozo zaidi!

Ni nani anayenufaika na hali hii? Au ndio wale wafanyabishara walioitia 'sirikali' mfukoni wa awamu ilee wamerudi kukusanya vyote walivyopoteza wakati wa JPM?

Eeh hayati JPM rais wa wanyonge, utusamehe siye wakosefu tuliokukosea adabu na kukusemasema vibaya wakati ule, sasa yametukuta, hatujui kama kuna tumaini au hali ndio hii hadi 2030. Anyway, pumzika kwa amani, kwa maana wewe haukutuangusha ila sisi tulikuangusha.
Mkuu ishu kama izi lazimanuwe nanjustification ya takwimu sio umeshiba ugali kisha unakuja na hoja nyepesi sanaa kama wazee wa kahawa vijiweni
 
Tuwe wawazi shida ilianzia awamu ya 5 na pia kwa sasa kuna matatizo chungu nzima yameiangukia Dunia hata kama lingekuwepo lile dubwana la Chato bado hali isingekuwa nzuri kwani budget yote ingeelekezwa kwenye machuma chuma plus mahelicopter ya ulinzi plus msako wa mtu anayeitwa Kigogo aishiye Twitter
Lile dubwana la chato pamoja ja mapungufu yake lakini lilikuwa na akili nyingi na uwezo mkubwa wa kufuatilia mambo mengi in details.

Maza ame 'delegate' mambo mengi yeye yupo bize kuzunguka huku na kule. Management ya kufanya delegation kila kitu bongo hautoboi.
 
Awamu pesa imerudi mtaani japo vitu vimepanda bei ila pesa tu imerudi mtaani huo ndo ukweli

Na ugumu wa maisha ulianza awamu ya tano kukaza vyuma
Kweli kila mtu na zama zake, mimi awamu ya tano vyuma vilikaza lakini maisha yalikuwa na stability, kwasasa mambo ni vurugu tupu.... Lakini wanasema historia ni mwalimu mzuri, mama akiendelea hivi basi tutajikuta tunaishi kama 1985-1995.
 
Watanzania kulilia inatusumbua sana badala ya kukaza buti. Sasa tozo gani inayokatwa hata kulalamikia mamlaka ya rais kiwango hiki. Tembea uone nchi zanazokata tozo ndio utaelewa, kuhusu maisha kuwa magumu asilimia kubwa ya watanzania tumezowea kuletewa samaki nyumbani na sio kwenda kuvua baharini. Tukazeni mikanda tuvuke mto
Mataifa yote yenye kodi kubwa inakwenda sambamba na huduma bora za jamii tena za bure! Kwa umasikini wa watanzania kuwa toza utitiri wa kodi ni kuwaongezea umasikini tu. Watakaonufaika na awamu hii ni wafanyabishara wakwepa kodi, na watumishi wa serikali wataponea kwenye rushwa kutokea kwenu.
 
Ukweli tuuseme tu, jahazi limeanza kumshinda mama. Sio kwa ugumu wa maisha huu!

Yaani watanzania wanatozwa tozo ambazo hata mkoloni na roho yake mbaya asingethubutu kuwatendea namna hiyo.

Wengi wetu vipato vyetu ni vilevile, lakini gharama za maisha zimepata mara dufu! Kwa lugha rahisi tumekuwa masikini zaidi.

Ni tozo tozo tozo kila kona, wakati huohuo kila kitu kimepanda bei, uwezo wa kufikiri wa mheshimiwa waziri wetu wa fedha umegota kwenye tozo tu. Yeye na timu yake kila wakiumiza vichwa bado jibu lao ni tozo zaidi!

Ni nani anayenufaika na hali hii? Au ndio wale wafanyabishara walioitia 'sirikali' mfukoni wa awamu ilee wamerudi kukusanya vyote walivyopoteza wakati wa JPM?

Eeh hayati JPM rais wa wanyonge, utusamehe siye wakosefu tuliokukosea adabu na kukusemasema vibaya wakati ule, sasa yametukuta, hatujui kama kuna tumaini au hali ndio hii hadi 2030. Anyway, pumzika kwa amani, kwa maana wewe haukutuangusha ila sisi tulikuangusha.
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake[emoji23]
 
Back
Top Bottom