Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Jamaa is very radical.

Nakumbuka kipindi kile cha kesi ya mashekhe wa uamsho alikua anawahamasisha wananchi kuwachangia mawakili wa mashehe wa uamsho.

Inashangaza mtu kuchukua upande wa mtuhumiwa wazi wazi wakati upo ndani ya serikali inayowashitaki hao mashehe.
 

Mkuu Maalim Seif alipoteza cheo cha Uwaziri Kiongozi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko alichopoteza huyo jamaa. NA akakaa ndani miaka miwili 2 .
Maalim Seif ni habari nyengine kabisa.
 
Huyu Othman anajua idadi ya wazanzibari walioko huku Tanganyika na biashara zao?
Muungano ukivunjika hawa wote watalipa vibali vya ajira.
 
Kwahiyo unataka tuwaache ili waikaloe zenji..muungano unamapungufu yake sana..ila kuipa uhuru kamili zenji ni kuhatarisha maisha ya watanganyika.

Tunazijua itikadi hizo zikikita mizizi..

#MaendeleoHayanaChama

Halafu nawewe unajiita mwana mabadiliko. Dah kwa kweli Tanzania kukomboka bado sana.
 

Kuwa Raisi sio hoja toshelezi, tatizo ni mfumo na sio Raisi. Hata yeye Raisi akiamua, Kuna TISS, JWTZ na Baba yao CCM wote watamshuhulikia mapema sana. Hivo vyombo vitatu ndivyo vinavyoulinda huu Muungano uchwara kwa hali yoyote. Sababu kuu ya katiba ya Warioba kukwama ilikua ni suala hili hili la Muungano.

Suala la muungano litatuliwa na wananchi wenyewe kwa umoja wetu tukiamua kutumia People's Power. Hakuna option nyengine.
 
Wazenji wengi hawana fahamu kuwa Muungano huu ni "iron-clad" yaani hauvunjiki sababu waliouanzisha ni marehemu kwasasa.

Wapiga kelele kama hao kina Othman ni kuwatumia "watu wasiojulikana" tu wapelekwe chocho na kutulizwa!
Ukiwatumia "wasiojulikana" ili wapelekwe "chocho", basi nyie wapeleka watu chocho ndiyo mnakuwa mmeshindwa na sio wakweli. Kuua/kupoteza watu sio suluhisho, bali ni ushenzi na uwendawazimu kwa wafanyao hayo...!!

Permanent Solution ya hii kitu inayoitwa "muungano wa Tanganyika & Zanzibar" ni kuipeleka kwa wananchi kwa njia ya "referendum" na swali liwe moja tu tena liulizwe kwa uwazi "unataka muungano au la" basi

Kabla ya watu kuamua, kampeni za wazi zifanyike na kila upande utetee NDIYO au HAPANA kwa kutoa sbb za kushawishi wananchi ili waamue ..
 
Ni ngumu sana kuvunja muungano huu, ni ngumu sana tena sana tu.

Familia karibu zote za Wazanzibar wana ndugu Bara, tumechanganyika sana.

Nimeishi Zanzibar kwa miaka 2 hivi, wenye shida kubwa ni Wapemba, ila hawa wa kutoka unguja hawana tofauti sana na wa Tanzania Bara, ni kama watu wa Kilwa tu. Kule Pemba ndio wao hujiona kama wanaonewa na hawaoni umuhimu wa Muungano.

Hizi chokochoko zina nguvu zaidi PEMBA na si UNGUJA.
 
Huyu Othman anajua idadi ya wazanzibari walioko huku Tanganyika na biashara zao?
Muungano ukivunjika hawa wote watalipa vibali vya ajira.

Mkuu unajua kuna watanganyika wangapi walioko Zanzibar?
 
Wazanzibar wanaotaka kujitenga ni wahuni tu Kwa Sababu kihalali Watanganyika ndo wanaunizwa na huu muungano Watu wanamiliki uchumi wa Tanganyika halafu Leo wanajiona wanjanja na kuanzia kulia eti wanaonewa huu ni ujinga tu .
 
Chuki zenu haziwez kufichika kamwe
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu
Wazanzibar wanaotaka kujitenga ni wahuni tu Kwa Sababu kihalali Watanganyika ndo wanaunizwa na huu muungano Watu wanamiliki uchumi wa Tanganyika halafu Leo wanajiona wanjanja na kuanzia kulia eti wanaonewa huu ni ujinga tu .
 
Wazenji wengi hawana fahamu kuwa Muungano huu ni "iron-clad" yaani hauvunjiki sababu waliouanzisha ni marehemu kwasasa.

Wapiga kelele kama hao kina Othman ni kuwatumia "watu wasiojulikana" tu wapelekwe chocho na kutulizwa!
Ndio mnaloweza tu hilo lá wasiojulikana washenzi wakubwa.

Hakuna mzanzibar anaehitaji muungano isipokuwa hão mliowaeka ili kutimiza matakwa yenu ya kiunyonyaji na kwanini mng'ang'anie wakati hampati faida mnayoipata huko znz.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Hayo ndio mawazo mgando mtu akiwa tofauti ya maono na nyinyi hafai. Nanllomo.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Wewe huoni faida ya umoja amani na undugu..kingine bahari na vilivyomo.

Muungano unafaida nyingi..mpungufu yaliyopo yalekebishwe tuwe na serikali moja ama tatu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na kwakuwa Rais wa JMT ni Mzanzibar huyu jamaa hakuna wa kumnyamazisha, awamu ya sita ndio ya kuclear dhuluma zote walizofanyiwa Wazanzibar.
Huyu atawasumbua sana CCM kwa ujinga wao tu, wa kuamini kwamba njia nzuri ya kunyamazisha upinzani ni ku'appease', kama kutoa hongo za nafasi za uongozi.

Njia hiyo ilikuwa ikisaidia wakati wa Maalim, lakini siyo kwa huyu Othman.

Njia nzuri ya kushughulika na huyu ni kumkabili na kupambana naye moja kwa moja bila ya kupepesa macho mbele za wananchi kwa kueleza manufaa yanayotokana na muungano. Ni kupambana naye kwa hoja wananchi waamue wenyewe. Wakishaelewa vyema, watampuuza. Akikosa 'platiform' amekwisha kazi.
 
Anatumia udhaifu wa CCM kujibaraguza hivi.

Huu muungano ulipoanzishwa, ile ilikuwa ni hatua ya mwanzo tu. Lengo lilikuwa ni kuendelea kuuimarisha kadri watu wa pande mbili walivyoweza kushirikiana na kuelewana.
Badala ya kufanya juhudi kuuimarisha muungano, CCM wakazembea, na kundi lililokuwa halitaki muungano huko visiwani likapamba moto na kuanza kulegeza/kudhoofisha badala ya kuimarisha muungano.

CCM wakadhani njia bora ya kuwatuliza hawa ni kuwakubalia mambo waliyodai. Kila walipowapa jambo moja, wanaanza kudai la pili. Sasa wamefikia hatua ya kudai uhuru kamili, yaani kuvunja muungano.

Sioni kiongozi mwenye uwezo wa kuwakabili hawa kwa wakati huu, na kelele zitakuwa kubwa sana, hasa wakati huu wa Samia.
 
Kwa hiyo mtu anayepewa ulaji na kutulia kumbe ndio mzuri kuliko asiyenyamazishwa na ulaji?
Mkuu, mimi sjasema hivyo. Hiyo itakuwa ni tafsiri yako mwenyewe juu ya nilichoandika mimi.
 
Huyu ni katika wanafunzi wa Siasa Maalim Seif kama ulikua hulifahamu. Hapo akiwa na Ismail Jussa wakiwa wadogo sana.
View attachment 2280695
EeeeenHeeee!

Ahsante kwa taarifa, na hasa hiyo picha.

Lakini si mwanafunzi hutokea akamzidi mwalimu wake? Ni nadra sana kumpata mwanafunzi akawa 'replica' wa mwalimu aliyemfundisha.
 
Kwahiyo unataka tuwaache ili waikaloe zenji..muungano unamapungufu yake sana..ila kuipa uhuru kamili zenji ni kuhatarisha maisha ya watanganyika.

Tunazijua itikadi hizo zikikita mizizi..

#MaendeleoHayanaChama
Fear of the unknown...

Ndio nyie mnaogopa kuiondoa Ccm madarakani kwa kuinyima kura mkiogopa upinzani kushika dola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…