Kauli za mitandaoni aziwezi kuwa za taasisi yeyote labda kama mchangiaji ni verified user na anamamlaka ya kuongelea misimamo yake; na CCM wanavikao vyao vya kuamua na msemaji wao rasmi.
Katika suala la vikao vya CCM kuna unafiki pia. Hawa CCM wa Zanzibar wapo kimya hata pale penye upotoshaji
Nyuma ya pazia watu kama akina Nahodha Vuai wana hoja zile zile za OMO
Mimi ni raia tu na sina shida na Othman Masoud naheshimu msimamo wake; sipendi tu njia zake za kutunga uongo wake katika kuhamasisha agenda yake.
Nami kama wewe si hoji haki yake ya kuongelea muungano kwa jinsi anavyoona, ninapingana na hoja zake za uongo, ubabaishaji na uzushi. Napingana na hoja zake za kujificha nyuma ya hoja wakati ana agenda kuu mbili
1. Chuki iliyofuruta dhidi ya Watanganyika na hata nahoji hivi Watanganyika wanachama wa ACT-Wazalendo wanakubali vipi dhalili kutoka kwa OMO
2. Hoja zake za kuzua uongo. Mfano, ni ile ya ''colligiate' ya Marekani ambayo haipo na hata kama tutaibadili kuwa electoral college kama ilivyo bado haikidhi haja zake.
Mfano wa pili ni unafiki. Watangazaji walimuuliza kuhusu sukari kuziwa kuingia kutoka Zanzibar, OMO hakujibu kwasababu anajua serikali ameruhusu vitu kutoka Zanzibar viingie tu bara bila kodi kupitia suluhu za kero zilizofanyika kwa siri zikiongozwa na Philip Mpango VP na Mwigulu Nchemba .
Hawa watu wawili wapo katika rekodi zetu ipo siku tutawakumbusha sisi Watanganyika
Hili ni kwa gharama za Watanganyika kwasababu Zanzibar inatumika kama uchochoro wa kukwepa kodi
Matokeo yake ni tozo na kodi kwa Mtanganyika kwa TRA kukosa mapato kwa uchochoro wa Zanzibar
Lakini imefikia hatua kama ni mahusiano basi Zanzibar ni ‘high maintance’ partner. Kila siku wanajipya tunawapa na bado wanalalamika raisi Samia alipoingia tu aliagiza maswala ya mapato na mikopo ishughulikiwe na washafanya hayo.
Tunatumia rasilimali nyingi sanakuweka huu muungano badala ya kuzitumia maeneo yanayosaidia nchi yetu
Mfano mapato ya simu tunagawana na Zanzibar, yaani simu ipigwe bara kuna asilimia inakwenda Zanzibar!!
Orodha ni kubwa inatosha tu kusema kuna gharama kubwa
Ifike mahala tuseme enough ya kugawa kwani lazima tuwafurahishe wao tu waende tu.
Nadhani wakati huo ni sasa, waacheni waende kuwa Singapore kama anavyosema OMO wa ACT
Hakuna athari zozote za kiuchumi wala kiusalama kwetu zaidi ya kupata taifa lingine lakujumuika na Kenya, Burundi, Rwanda na Zambia ambao kutwa wanalilia bidhaa za chakula kutoka Tanzania. Na hayo mahoteli wanayofungua ni opportunity kubwa kwa wakulima wa Tanzania baadae.
Tumembeleza vya kutosha tuwaache sasa waende wenyewe awataki.
Hakuna! na hakuna Mtanganyika atakayepoteza chochote au lolote! hakuna
Hawa Watanganyika wanachama wa ACT wajue kupitia kauli za chuki za OMO kwamba ACT si yao