Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Umenikumbusha enzi za marehemu Ng'wea..,kuna siku nilimkuta Msasani mwisho kule asubuh hana hata nguo nadhani nae alilewa sana usiku huo,....siku nyingine tena nilikutananae maeneo flani yaani yupo rafu kichizi/kachoka nadhani pia ni madawa yale.

Chaajabu baadhi ya wasanii wenzake na wadau wa muziki walikuwa wanajua hilo..,ila baada ya kufa ndio kila mtu anampa sifa na kutoa msaada na wakati kipindi yupo hai wala hakuwa anapata hizo sifa!! kwa jinsi nilivyokuwa namuona kwa hadhi ya Ng'wea hakustaili ile hali alihitaji msaada zaidi.

Na kwa Chid nadhani ni mpaka afe ndio watu waanze kushtuka japo najua kuna baadhi ya wadau walishataka kumsaidia..,lakini wasanii nadhani ndio wanapaswa kuwa mstari wa mbele kwny hilo swala la kumsaidia msanii mwenzao.
Chanzo ni masela Mavi

RIP Zizi
RIP Ngwair
RIP Pancho Latino

Chanzo cha yote ni masela Mavi
 
Faida ya ngada hiyo!!
Hawa wasanii hawapendi kuingia kwenye huo uraibu, lakini mfumo mbovu wa usimamizi muziki hapa tz ndio unawaumiza na kujikuta wanatumbukia kwenye huo mtego wa madawa.

Jaribuni kumsikiliza vizuri dudubaya katika interview alizofanya hivi karibuni. Jamaa kaongelea mfumo wa muziki ulivyo mbovu na wa hovyo sana, wasanii wanapitia mengi sana, kwenye huu muziki kuna mijitu inawanyonya mpaka wanabaki ngozi halafu inawatema.I
 
Umenikumbusha enzi za marehemu Ng'wea..,kuna siku nilimkuta Msasani mwisho kule asubuh hana hata nguo nadhani nae alilewa sana usiku huo,....siku nyingine tena nilikutananae maeneo flani yaani yupo rafu kichizi/kachoka nadhani pia ni madawa yale.

Chaajabu baadhi ya wasanii wenzake na wadau wa muziki walikuwa wanajua hilo..,ila baada ya kufa ndio kila mtu anampa sifa na kutoa msaada na wakati kipindi yupo hai wala hakuwa anapata hizo sifa!! kwa jinsi nilivyokuwa namuona kwa hadhi ya Ng'wea hakustaili ile hali alihitaji msaada zaidi.

Na kwa Chid nadhani ni mpaka afe ndio watu waanze kushtuka japo najua kuna baadhi ya wadau walishataka kumsaidia..,lakini wasanii nadhani ndio wanapaswa kuwa mstari wa mbele kwny hilo swala la kumsaidia msanii mwenzao.
Yan ulimkuta hana nguo yuko uchi au
 
Umesema ukweli japo ni mchungu. Dunia na maisha kwa ujumla hayana huruma. Ndiyo, watu kama hawa wakishafika hiyo stage ya uteja wanahitaji msaada kwani wenyewe wanakuwa hawana uwezo wa kujisaidia tena, lakini kiuhalisia kwa maisha ya kitanzania hili ni gumu kutokea. BTW si ni watu wa CCM hawa? Au inawapenda wanapokuwa wazima tu?
Familia huwa zinapambana sana na kufanya kila namna inayowezekana kumsaidia mwana familia anaekuwa kwenye changamoto hiyo, watu wengi hudhani familia imewatenga na kuwasahau watu wenye shida kama za chidi. Jibu ni hapana, wengi wakishakuwa na hali hiyo kwanza nyumbani hawatulii na huona sio eneo salama kwao kabisa. Na hii ni kwa sababu hujiona kuwa wapo sawa.

CCM watakutumia ukiwa timamu tu.
 
Haya maisha yamejaa mambo mengi sana usipokua makini utakufa kwa stress.... Mfano mm haya maisha ninayoishi ni tofauti kabisa na matarajio yangu, najiona kabisa nime underachieve.... Naamua tu ku-smile coz nikileta tu ujuaji nitajikuta nazungumzwa kwenye topic moja na wakina child benz
 
Chidi ni rapa mkali sana ila mfumo wa nchi kwenye mziki wa hip hop haujampa mafanikio kulinganisha na alichotoa(uwezo wake) imepelekea kupata msongo wa mawazo na kutumbukia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Mtu mwingine anayekuja kwa sifa ni Young dee soon kitaumana.
teja ni teja tu hata angepewa bilions atabaki kuwa teja. Kinachomsumbua ni kile alicholisha ubongo wake. Nakumbuka miaka flani Ray C kabla na yeye hajawa teja aliwahi kusema Chd Benz anatumia Madawa ya kulevya kilichofuata alimkung'uta ngumi za kutosha. Hivo suala ni la kwakwe yeye mwenyewe si la jamii wala taifa. Kipindi anafanya mziki mdo kipindi na wanzake kina Sugu. AY, FA , Lady JD na wengine pia walikuwa wanafanya mziki, wao waliwezaje kusastain?
 
Yaani uyaharibu maisha yako kisha utarajie msaada kwa wengine wakusaidie?
Masela Mavi unaowafuata wao ukiwa safi wapo na wewe ila ukiwa ovyo hawapo na wewe hio ndio inachowaumiza wengi, ifike wakati masela Mavi uachane nao tu ukiachana na masela Mavi Maisha yanajiset yenyewe ukikomaa nao mwisho ndio hivyo utaishiwa pumzi hivi wanakuona na wasikusaidie masela Mavi sio watu
 
Kuna tetesi kuwa maza ake anamdekeza sana japokuwa si kazi rahisi kupambana na mraibu wa madawa ya kulevya wandugu,

Kunae ndugu mpaka sasa anaishi kama chokoraa wakati kwao uwezo upo tena mkubwa tu lkn ndo hivyo wameshindwa kumsaidia wakimpeleka vituoni anatoroka nk wameamua kumuacha ajipambanie hata akienda kwao hawamruhusu kuingia ndani anaishia nje
 
Chidi ni rapa mkali sana ila mfumo wa nchi kwenye mziki wa hip hop haujampa mafanikio kulinganisha na alichotoa(uwezo wake) imepelekea kupata msongo wa mawazo na kutumbukia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Mtu mwingine anayekuja kwa sifa ni Young dee soon kitaumana.
Upo sahihi sana. Miaka ile ya 2007 wanakuja kina Jah Rule Tanzania, Chid ndie alikuwa msanii kinara wa hip hop Tanzania anaye-repesent muziki wa hip hop anafanyiwa interview kuhusu ujio wa kina Jah Rule.

Kidogo cha kuongezea, inawezekana hii hali yake ipo upande wa kiroho pia.
 
Kuna tetesi kuwa maza ake anamdekeza sana japokuwa si kazi rahisi kupambana na mraibu wa madawa ya kulevya wandugu,

Kunae ndugu mpaka sasa anaishi kama chokoraa wakati kwao uwezo upo tena mkubwa tu lkn ndo hivyo wameshindwa kumsaidia wakimpeleka vituoni anatoroka nk wameamua kumuacha ajipambanie hata akienda kwao hawamruhusu kuingia ndani anaishia nje
Chid mboni alishapona au wewe unazungumzia nini Chid kinachomsumbua sasa hivi ni tungi anakunywa sana na alishashauriwa na Daktari aache mitungi Ila Mzee anarudi kule kule sababu ni masela wanaomzunguka wale masela wa Ilala wote anabidi awapige chini ndio wanaomrudisha SHIMONI
 
Umeongea point. Wanyonyaji katika hiyo sekta ya music ndo wamewafikisha wengi hapo mahala oabaya walipofika, miongoni kwao Tod na q.chief. Vijana walikuwa na vipaji lakini wanyonyaji wakawadhibiyi na kuwakamdamiza na kiwataka wafate SHERIA zao kandamizi na wakiuliza tu wanapotezwa kwenye industry, muziki Yao haipigwi... management za kinyonyaji miongoni kwao marehemu Ruge na Joseph kusaga na kina chief kumbe... Diamond mjanja sana alkwasanukia mapema akatupa huko, ingawa mpaka Sasa sio kwamba yupo salama sana sababu bado wamemganda na wanampa percentage kidogo hapo wasafi...let's wait and see kama atafanikiwa kwenye hiyo seven media
Kwani wasafi sio yake?
 
Chidi ni rapa mkali sana ila mfumo wa nchi kwenye mziki wa hip hop haujampa mafanikio kulinganisha na alichotoa(uwezo wake) imepelekea kupata msongo wa mawazo na kutumbukia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Mtu mwingine anayekuja kwa sifa ni Young dee soon kitaumana.
Mimi sikubaliani na wewe. Enzi akiwa kwenye peak alikuwa ni msanii ambaye alikuwa ana shows nyingi ana make ela ndefu shida ni pale alipotaka kuishi maisha aliyokuwa anayaona kwenye TV ya kutembea na msululu wa watu na kuwalisha na kuwanywesha na kuishi the same lifestyle kama la black American movies.
Haya ni matokeo ya kufanya uchaguzi mbovu maishani. Kwa kipindi chake na pesa aliyokuwa anapata kwa kipindi hicho ilikuwa nyingi angefanya kitu. Sidhani mtu kama Jay Mo alipata pesa nyingi kuliko Chid, but alifanya uamuzi sahihi.
Sasa hivi ni vigumu sana kumsaifia Chid kwanza kila anayetaka kumsaidia anageuka adui. Refer kisa chake na Diamond. Kaingiza vocal kwenye wimbo wake kumboost, kweli wimbo ukaenda hata mimi nilikuja kuusikiliza baada ya kuona ile performance yao, later anamkandia.
Chid kutumia madawa kaanza kuyatumia akiwa kwenye peak, akitumia madawa na pombe. So pesa imekata tayari ashakuwa addicted na madawa.
 
Back
Top Bottom