DOKEZO Hali ya ghorofa la "Hall Two", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikoje? Mara ya mwisho kulikuwa na habari kwamba limeinamia upande mmoja

DOKEZO Hali ya ghorofa la "Hall Two", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikoje? Mara ya mwisho kulikuwa na habari kwamba limeinamia upande mmoja

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wakati nikibukua pale jalalani, ilitokea sintofahamu kwamba jengo la ghorofa la Hall Two, linainama/linatitia kwa kuelekea upande wa nyuma kwa taratibu sana.

Woga ulipita, na nadhani hata kwenye media iliwahi kujadiliwa. Kwa janga la kariakoo, nawasihi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia watoe taarifa ya jengo hilo ambalo "linameza" maelfu ya wanachuo kwa staili ya kubebana.
Eksipansheni jointi
 
Wakati nikibukua pale jalalani, ilitokea sintofahamu kwamba jengo la ghorofa la Hall Two, linainama/linatitia kwa kuelekea upande wa nyuma kwa taratibu sana.

Unaweza kusoma UDSM hall 2 na 5 zenye ghorofa 11 hazina muda mrefu zitadondoka

Woga ulipita, na nadhani hata kwenye media iliwahi kujadiliwa. Kwa janga la kariakoo, nawasihi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia watoe taarifa ya jengo hilo ambalo "linameza" maelfu ya wanachuo kwa staili ya kubebana.
Hatuombei mabaya, lakini, "ukiona mwenzako ananyolewa..."
 
Ndio sababu daima tunayakumbuka maelekezo ya Shujaa JPM juu ya majengo haya ya hovyo ndani ya nchi yetu.

Siku anaagiza majengo ya k.koo yapimwe Na yasiyo Na sifa yapigwe nyundo walio wengi waliona jamaa anazingua Sana eti Sasa Huo udikteta. Sasa shughuri Imeanza Na waliokuja Kwa kumpinga Sana ndo hao hao sasa Hivi wanajifanya kutoa maagizo eti sijuhi vitu Gani. Sasa wamegundua dhamira ya Mwamba ilikuwa nyeupe kama theruji ...nchi hii majengo mengi yanajengwa Na Nondo Za vyuma chakavu but no one cares.

R.I.P JPM 🙏
 
Wezi wa kura,

Wapotoa HAKI, wezi wa Sanduku la kura,

Wavuruga uchaguzi wa mitaa sasa hivi mko bendera fuata upepo,

Mmejivika uingeneer kuongelea ujenzi wa magorofa kana kwamba yalijengwa ktk utawala wa CHADEMA.
 
kuna mengine mawili yapo pale MUST mbeya,...ni hostel mbili zilijengwa na WABONGO,....zimejaa nyufa mpaka basi,..wahusika wanapaka rangi tu,.......

na hilo linatokea chuoni,..tena chuo cha engineering
dah mbona ani hatari, wahusika wafanyie kazi hizi mambo si utani hata nini
 
Kwa Main campus sehemu niliyokua naweza kuishi kwa Amani ni Hall 6... Hizo za gorofa ndefu kuna kipindi watu walikua wanaenda kuchota maji chini wanapanda na Lift na zikawa zina tabia ya kukwama mara kwa mara, pia nakumbuka kuna Hall moja walisitisha kabisa kulaza wanavyuo baada ya kuinama!
 
Na Habari ndo ikaishia hapo au..........wanasubiri kwa hatua zaidi?
 
Hall2 na hall5 toka 2007-2010 nikiwa pape jalalani ilikuwa kawaida vipande vya concrete kupasuka na kudondoka na vina cracks za kutosha kimsingi zilishafika mwisho wa maisha
 
N
Nchi ya Tanzania inajiendea tu.Ndiyo maana Mimi niliamua kuhamia nchini Rwanda.Rwanda hakuna huu uhuni wa kujenga majengo chini ya kiwango .
Naam, hapo ni KAZI kwa viwango, ukileta za kuleta Chali. Hata lami barabarani ni Safi .
 
Back
Top Bottom