Hali ya maisha ya Mtanzania ni ngumu sana. Rais asipochukua hatua sasa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi

Mapori still yapo mengi tza hatuna tatizo la overpopulation,watu waendelee kuzaa tu.ukitoka tu kibaha kilometer 3 nje ni mapori tupu.
Tuache kukaa mijini,fursa zipo maporini huko
Wewe upo huko maporini au wote tumebanana hapa hapa Dar?
 
Unapigia mbuzi gitaa tu. Nafikiri kenge hasikii mpaka atoke damu sikioni baada ya kupigwa hasa.
 
Lini ushawahi kuskia mtanzania anasema maisha mazuri? Mwanadamu haridhiki hata umpe nini, hizi kelele za kawaida tu
Kweli kabisa, kila awamu ilikuwa na itaendelea kuwa na walalamikaji.

La muhimu mtu afanye kazi ajitahidi kujikwamua kwa mipango yake mwenyewe
 
Maneno bora kabisa. Tumeongea sana na sasa kilichobaki ni actions.
 
Hatutaki tena maneno tunataka actions
 
Hatutaki tena maneno tunataka actions
Ktk suala la KATIBA mpya, tutatoka wengi mno makundi mbalimbali.

Hamasa na Elimu iendelee bila kuchoka.

Watu waelimishwe Kwa staha na upole jinsi Gani Katiba mbovu iliyopo inavyohusika kuwabebesha mzigo mzito wananchi Ili kuwanufaisha kundi dogo.

Tutashinda. Amen
 
Hivi Kuna yule Mama Mkurugenzi Mkuu wa NBS,kile cheo ni cha Ki-Chief?
Yule mama takwimu zake zimejaa uwongo mwingi sana,hivi ni kweli kwa mfumuko huu wa bei za bidhaa,ni 4.9% kweli [emoji1787].
Mimi naona mfumuko wetu wa bei upo kati ya 10% na kuendelea.
 
Mama anapambana na Gridi ya taifa ya umeme chini Engineer Kipara Makamba kwa gharama ya Bilioni 500 badala ya kupambana na inflation!!
 
Gharama za maisha zimepanda ni matarajio yangu serikali ingekua imeshapeleka muswada wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi. Na ni mategemeo yangu bajeti mpya itakwenda kuongeza mishahara na kima cha chini
Subirini Mama afumue Gridi ya taifa ya umeme,bei zitashuka tu!
Leo yupo Ikulu ya Magogoni anasainisha mikataba ya Bilioni 500 na Wakandarasi!
 
Hizi mvua tu zikikata kabla ya swala hata la chakula kuwa ghali, mabwana TANESCO watawaletea story kwamba maji yameisha hivyo watakata umeme siku nzima.

Wenye wanauza vitu vya kuhifadhiwa kwenye friji wakatafute kaz nyingine
 
Kama umezoea sijui asali, kuhongwa, kusaidiwa, usidhani ni wote. Sisi wengine tumefika tulipo kwa kupambana hasa, kwa kutambua thamani ya muda, kuyatafuta maarifa kila yalipo, na kuhakikisha wakati unatafuta the highest productivity katika kila unachofanya.

Ndiyo maana nyakati zote, hata uje utawala gani, hutasikia nalalamika eti nimeshindwa kuyapata mahitaji ya muhimu ya familia.

Sina ubia ndani ya Serikali, sina wa kumtetea kulinda udhaifu wake ndani ya Serikali ila nautambua wajibu wangu kama myu binafsi kwa nafsi yangu, familia yangu na jamii. Wajibu wa Serikali unafuata baadaya wajibu wangu.

Nimeishi katika nchi 8 za Afrika, 2 za Ulaya, 1 ya America ya Kaskazini, 2 America ya Kusini, na 2 za Asia. Kote huko, ukiondoa Australia, usipopambana, maisha mazuri utakuwa unayasikia tu kwa wengine. Mishahara ipo juu lakini bei za vitu zipo juu sana. Australia, maji ya kunywa yanauzwa kwenye chupa kama za soda, bei unaambiwa ni dola 3 za Australia, karibia dola 2.5 za Marekani. Hiyo ni zaidi ya sh 5,000 za Tanzania. Ukiwa wa kulalamika tu, unadhani utaweza kuyanywa hata hayo maji? Japan, kuna watu wanafanya kazi mpaka kwa waajiriwa wawili ili apate pesa ya kutosheleza mahitaji yake.

Anayejua mahitaji yake ni wewe mwenyewe, siyo Serikali. Ujiwekee msimamo wa kuhakikisha maisha yanaenda hata pale ambapo ulichokitegemea toka Serikalini hukipati.
 
Kuwa na katiba mpya siyo dili sana, issue ni je, itafuatwa? Inaweza ikawepo na watu wakaendelea kuisigina tu. Hii tu inasiginwa sembuse katiba mpya? Kuna muarobaini upo mahali ila si katiba mpya.
 
Kuwa na katiba mpya siyo dili sana, issue ni je, itafuatwa? Inaweza ikawepo na watu wakaendelea kuisigina tu. Hii tu inasiginwa sembuse katiba mpya? Kuna muarobaini upo mahali ila si katiba mpya.
Mamlaka makubwa ya Rais ndo mzizi wa fitna, mengine yafuata.
 
Brother tafuta shamba Lima mandindi hekari 1 utapata gunia 30
Lima mpunga utapata gunia 40
Lima maharage utapata gunia 9

Mungu katupa mvua na ardhi
Wewe umekaa kulia lia ujinga ujinga
 
Ushauri mzuri
Yeye apambane ngazi ya familia
Kulalamika ni ujinga tuu kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…