ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Njaa imepanda kichwani [emoji16][emoji16]Ukiwa chawa halafu kichwani mweupe ni mzigo....
Na bado
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Njaa imepanda kichwani [emoji16][emoji16]Ukiwa chawa halafu kichwani mweupe ni mzigo....
Hawa waache wachapike wamekimbia mashamba wanakuja kulalama.mjinitatizo mnakimbilia kukaa mjini wakati hamna kipato
Wewe upo huko maporini au wote tumebanana hapa hapa Dar?Mapori still yapo mengi tza hatuna tatizo la overpopulation,watu waendelee kuzaa tu.ukitoka tu kibaha kilometer 3 nje ni mapori tupu.
Tuache kukaa mijini,fursa zipo maporini huko
Unapigia mbuzi gitaa tu. Nafikiri kenge hasikii mpaka atoke damu sikioni baada ya kupigwa hasa.Nilimsikia akisema anakopa ili afanye kitu cha kuacha alama, hivi legacy inajengwa kwa kuacha daraja kubwa au flyover!? Nyerere aliacha legacy dunia nzima kwa aina ya uongozi, fikra na falsafa zake, leo legacy imekuwa kuacha miradi mikubwa mikubwa kwa gharama ya kuacha nchi kwenye madeni yasiyotamanika.
Hivi kweli hii ndiyo namna ya ku-manage uchumi kwenye nchi maskini kama Tanzania! badala ya kuwekeza kwenye maendeleo ya wananchi walio wengi unaenda kuwekeza kwenye mamiradi yasiyo na kichwa wala miguu yanayotumia pesa nyingi, kununua ndege kwa cash, bila kusahau matumizi ya anasa ya serikali maviieite huku ukikamua hata savings ndogo za watu kwa njia ya tozo.
Ajira hazitolewi, mishahara haieleweki......pesa zinaenda kulipa mikopo iliyochukuliwa kwa pupa.
Kweli kabisa, kila awamu ilikuwa na itaendelea kuwa na walalamikaji.Lini ushawahi kuskia mtanzania anasema maisha mazuri? Mwanadamu haridhiki hata umpe nini, hizi kelele za kawaida tu
Maneno bora kabisa. Tumeongea sana na sasa kilichobaki ni actions.Viongozi wa juu Serikalini wananufaika na Ugumu wa maisha wa Raia.
1. Unapolipa vat kwenye bidhaa madukani, Serikali inapata pesa za kununua mafuta kwenye V8 za viongozi.
2. Unaponunua Mchele 3,500 Kwa kilo, jua Basha anatunisha mfuko kwenye Kampuni zake za kuuza nafaka Kenya na somalia.
3. Unapolipa 55,000 nauli ya Dar Mwanza, Kuna kampuni ya mwigu na wenzie kupitia Mama Esther wanatajirika kupindukia.
4. Unaponunua maji 500 Kwa ndoo moja, uwe na HAKIKA Wizara ya maji wanatumia mwanya huo kuomba pesa hazina kutatua changamoto hiyo, na pesa zikitoka ZINAPIGWA.
5. Unaponunua bundle la internate Bei juu, Pena anapata posho Kutoka makampuni hayo, ananufaika na Bei ya vifurushi kuwa juu.
6. Unaponunua mafuta ya kupikia Lita Tano Kwa 30,000 uwe na HAKIKA Kuna TOZO na Kodi zaidi ya 5000 Kwa Kila dumu imeingia Serikalini na inatoka Kwa matumizi ya kawaida ya viongozi.
Serikali haiwezi kupunguza mzigo wanaoubeba raia, sababu kwao sisi ni chanzo Cha mapato Yao.
Tuungane kudai KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA Ili kuondoa mifumo kandamizi inayoumiza wengi kuhudumia Wachache.
Amen
Rudi kijijini kalimeIla kiukweli hali ni mbaya sana mtaani, mzunguko wa pesa amna kabisa vitu bei juu ni hatari sana
Hatutaki tena maneno tunataka actionsHivi tunavyoongea maandamano yameanza kiripotiwa mataifa mbalimbali,
Endeleeni kupuuza sauti za Raia, itawatokea puani,
Mnapandisha Bei ya mbolea, na mbolea wanauziwa madalali Si wakulima halafu mnawambia wakalime,
Wakivuna mazao mnawalangua Kwa Bei chini na mnaweka Kwa maghala na kuuza nje ya nchi,
Hii ni 2023, mtatoka mapangoni mlikojificha. Hali inayoendelea haitapita hivi hivi,
HUKUMU juu ya viongozi waovu imeamriwa.
Tusubiri.
Ktk suala la KATIBA mpya, tutatoka wengi mno makundi mbalimbali.Hatutaki tena maneno tunataka actions
Hivi Kuna yule Mama Mkurugenzi Mkuu wa NBS,kile cheo ni cha Ki-Chief?Ee Mungu nipe hekima yako niweze kuandika kitu kitakacho weza kuwapa uwelewa viongozi wenu juu ya Hali ilivyo mbaya kwa wananchi wake [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Awali ya yote Samia mama naomba elewa Hali za Watanzania ni mbaya Sana na inatisha kweli kweli [emoji24][emoji24][emoji24]
Tujiulize sisi kama taifa tumemkosea wapi Mungu na je viongozi wetu hamuoni jinsi wananchi wanavyo teseka
Ukitaka kujuwa udhaifu wa mtu mtese usimpe chakula nyie kama viongozi juu ya hili mmeliweza wananchi hawana chakula kabisa
Swali la kujiuliza mama hivi kweli shilling 10000 haitoshi kabisa Kwa bajeti ya siku kwa familia mfano mdogo tuu nikuonyeshe mama
Familia yenye watu 5 tu baba mama na watoto 3
Asubuhi baba aache 10000
Asubuhi wanunue vitafungwa tu 2000
Watoto wapewe nauli za shule 1000×3=3000 hii ni nauli pamoja na hela ya kula shuleni
Mchana mama haha chochote labla mama amejikaza kanunuwa mihogo ya 1000 na bibi nyingi Akala
Mfukoni imebaki 4000 je hii hela itatosha kwa chochote kile ila waweze kula jioni
Mchele kilo ni 3500
Mafutaa pishi ni 500
Mkaa 2000
Mboga za majani 1000
Nyanya +karoti + kitunguu 2000
Je swali kwenye Ile 10000 baba alio acha asubuhi imebaki shingapi
Naomba ujue kitu kimoja mama watu wanao umia juu ya huu mfumuko wa bei ya chakula ni wananchi wa chini sio wa juu [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Je wewe kama RAIS una waza juu ya hili just imagine wewe unatumia shingapi kwa siku juu ya chakula jaribu kuchukuwa 10000 alafu ujaribu kuibajetia kama itatosha kwa chochote kwanzia asubuhi Hadi jioni
Ushauri wangu huu ni Muda muafaka wa serikali kusitisha kuuza nafaka nje mama naomba achana na Bashe kabisa huyu ni mfanyabishara mkubwa wa mahindi Kenya na wewe unalijuwa Hilo
Tueni Yale mazao yaliyopo kwenye ghala la taifa yauzeni kwa bei nafuu maana Hali ni mbaya mtaani huku
Wekeni mikakati ya kuboresha sekta ya kilimo kwa kuwapa vijana mikopo wakalime ili kukabiliana na hili tatizo la njaa siku za mbeleni huko
Ukiendele kufubaza shingo juu ya hili nililo kuambia tutakumbana na baa la njaa ifikapo mwezi wa 6 mwaka huu
Pia angalia mishahara ya watanzania sio rafiki kabisa na Hali ya uchumi ilivyo
Una mlipa mtu 300000 kwa mwezi huyu mtu kulingana na hesabu ya siku anapokea 10000 hapo bado hajalipa Kodi, NSSF anabakiwa na shingapi hapo lakimbili na nusu je hiyo laki mbili na nusu itatosha kumwendesha maisha kwa mwezi mzima embu fikirieni juu ya hili
Boresheni mishahara kwa sector zote private sector hawajaongezewa hela Hadi saa hizi Ina maana Hawa sio Watanzania je gharama za maisha zimepanda kwa wafanyakazi wa serikali tuu
Mnakwenda kutengeneza kizazi ambacho ni hatari sana Kwa hili taifa
Hakuna ajira Kwa vijana na wanao hitumu ni wengi je Nini kinaenda kutokea Hadi ifikapo 2035
Sina mengi ya kuyasema zaidi ya hayo kwa unyenyekevu mkubwa na shukuru mwenyezi Mungu kwa kunifungulia haya na kuyaona na kukueleza mama nimekuwa mnyenyekevu kwako kwaajili ya watanzania wote [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Kingine japo sio Cha mwisho angalia mama swala la vifurushi vimekuwa ni hatari sana
Shilingi elfu Moja unapata MB 490 mama hii sio Haki kabisa nape ni kidonda katika hii wizara haiwezeka kuwa hivi mnawanyosha Sana wananchi wa chini SEMA neno Moja juu ya hili swala na hakika utarejesha matumaini kwa wananchi wa Hali ya chini
[emoji120][emoji120][emoji120]
Mama anapambana na Gridi ya taifa ya umeme chini Engineer Kipara Makamba kwa gharama ya Bilioni 500 badala ya kupambana na inflation!!Nadhani auwajui Watanzania, hii inabaki tu kama hadithi uliyoisimulia siku ya leo.
Na bi samia na ccm yake wala hawajali na hawana hofu kwani wanatujua hatuna mpango wa kudai haki zetu dhidi ya haya maumivu.
Umeibaini standard ya hiyo elimu watoto wanayoifuata?? Ni uchafu mtupu, ndio huo unaotupa div4 na zero kwa 80%, na km hatuko tayari kutoka nje kuwaeleza watawala juu ya matendo na uovu wao dhidi yetu basi tutulie makalio yakiwa juu ili sindano zituingie haswaaa.
Overrr
Subirini Mama afumue Gridi ya taifa ya umeme,bei zitashuka tu!Gharama za maisha zimepanda ni matarajio yangu serikali ingekua imeshapeleka muswada wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi. Na ni mategemeo yangu bajeti mpya itakwenda kuongeza mishahara na kima cha chini
Hizi mvua tu zikikata kabla ya swala hata la chakula kuwa ghali, mabwana TANESCO watawaletea story kwamba maji yameisha hivyo watakata umeme siku nzima.Aliyeshiba hamjui mwenye njaa, wahenga walisema. Tuombe tu Mungu, mvua za masika zinyeshe maskini tuweze kujipatia chakula chetu.
Pia kumbuka damu ni nzito kuliko maji, huyo bwashee hawezi kufunga mipaka wakati ndugu zake hawana chakula. Sana Sana atawahimiza waje wakati wa mavuno, waingie mpaka huko vijijini ndani ndani wakusanye shehena ya kutosha na wasafirishe makwao.
Kama umezoea sijui asali, kuhongwa, kusaidiwa, usidhani ni wote. Sisi wengine tumefika tulipo kwa kupambana hasa, kwa kutambua thamani ya muda, kuyatafuta maarifa kila yalipo, na kuhakikisha wakati unatafuta the highest productivity katika kila unachofanya.Haya uliyoandika hapa yangekuwa yamekamilika kama ungeonesha role ya serikali, na vipi serikali imetimiza wajibu wake kufanikisha hilo. Nakuona unaendelea kuficha madhaifu ya serikali kwenye hili suala, naamini sababu inayokufanya uwe hivyo ni ile ile asali.
Kuwaambia watu waache kukimbilia kazi nyepesi za kubangaiza, wakati ndizo zilizopo, kwasababu serikali imeshindwa kuwapa wahitimu wa vyuo kazi nzito unazotaka wafanye, ni kuwaonea wapambanaji, show some respect!.
Serikali inayojielewa, ikishatambua changamoto wanazopitia raia wake, lazima itafute namna ya kuwapunguzia maumivu, mfano, serikali ikishajua raia wake wengi wanafanya kazi nyepesi, zinazowapa kipato kidogo, ni lazima ifanye iwezalo kupunguza mfumuko wa bei, hawa wapambanaji hawawezi control hilo.
Zaidi, unaposema watu watazame family planning, hapa napo unatengeneza tatizo jingine mbele ya safari, tunaona kwenye baadhi ya nchi zilizoendelea, hata kama teknolojia inayowarahisishia kufanya kazi zao, usiyatazame haya mambo kwa jicho la upande mmoja.
Kuwa na katiba mpya siyo dili sana, issue ni je, itafuatwa? Inaweza ikawepo na watu wakaendelea kuisigina tu. Hii tu inasiginwa sembuse katiba mpya? Kuna muarobaini upo mahali ila si katiba mpya.Ktk suala la KATIBA mpya, tutatoka wengi mno makundi mbalimbali.
Hamasa na Elimu iendelee bila kuchoka.
Watu waelimishwe Kwa staha na upole jinsi Gani Katiba mbovu iliyopo inavyohusika kuwabebesha mzigo mzito wananchi Ili kuwanufaisha kundi dogo.
Tutashinda. Amen
Mamlaka makubwa ya Rais ndo mzizi wa fitna, mengine yafuata.Kuwa na katiba mpya siyo dili sana, issue ni je, itafuatwa? Inaweza ikawepo na watu wakaendelea kuisigina tu. Hii tu inasiginwa sembuse katiba mpya? Kuna muarobaini upo mahali ila si katiba mpya.
Ushauri mzuriUkiona hali inazidi kuwa mbaya, tazama mahitaji ya familia yako, ili uone yale yasiyoyalazima uyaondoe.
Mahitaji mengine huwa tunayaendekeza kwa sababu za kimazoea tu, kama vitafunwa asubuhi, muhimu washibe asubuhi, watashiba nini na vipi, jiongeze baba wa familia kwa kushirikiana mawazo na mama yao, wanawake wengi huwa wako vizuri kwenye budget.
Muache Samia apambane kwenye ngazi ya taifa, wewe pambana na mwenzio kwenye ngazi ya familia.