Haya uliyoandika hapa yangekuwa yamekamilika kama ungeonesha role ya serikali, na vipi serikali imetimiza wajibu wake kufanikisha hilo. Nakuona unaendelea kuficha madhaifu ya serikali kwenye hili suala, naamini sababu inayokufanya uwe hivyo ni ile ile asali.
Kuwaambia watu waache kukimbilia kazi nyepesi za kubangaiza, wakati ndizo zilizopo, kwasababu serikali imeshindwa kuwapa wahitimu wa vyuo kazi nzito unazotaka wafanye, ni kuwaonea wapambanaji, show some respect!.
Serikali inayojielewa, ikishatambua changamoto wanazopitia raia wake, lazima itafute namna ya kuwapunguzia maumivu, mfano, serikali ikishajua raia wake wengi wanafanya kazi nyepesi, zinazowapa kipato kidogo, ni lazima ifanye iwezalo kupunguza mfumuko wa bei, hawa wapambanaji hawawezi control hilo.
Zaidi, unaposema watu watazame family planning, hapa napo unatengeneza tatizo jingine mbele ya safari, tunaona kwenye baadhi ya nchi zilizoendelea, hata kama teknolojia inayowarahisishia kufanya kazi zao, usiyatazame haya mambo kwa jicho la upande mmoja.