Si kweli kuwa mradi wa SGR una hali mbaya kihivyo.
Labda unapitia changamoto za kawaida za miradi mikubwa.
Miradi mikubwa dunia nzima huwa na changamoto zake, zingine ni kubwakubwa , haimaanishi kuwa changamoto hizo hazwezi kutatuliwa kwa namna moja nyingine.
Changamoto ambayo miradi mingi mikubwa ya Tanzania tutegemee kukukmbana nazo ni ucheleweshaji usioepukika kiwepesi kwa mfumo wetu wa Design Procurement and Build.
Mfumo huo inabidi tuwe na watu efficient sana wa kusimamia makandarasi katika hatua zote. Ikumbukwe kuwa malipo kwenye utaratibu huu huwa yanafanyika kwa kwanza makadirio halafu kwa au purchased na halafu as built.
Kuna uangalifu na umakini mkubwa sana hapo unatakiwa uwepo. Maana kipande kwanza mkandarasi na washauri wanalipwa kwaa makadirio, halafu kuna malipo ya vilivyonunuliwa, mara zote gharama huwa juu kuliko makadirio, na pakishajengwa, napo kuna malip ya as built.
Matokeo yake makadirio yanakuwa ya juu sana, ndiyi kwa mara ya kwanza Tanzania tunasikia kuna mabaki ya pesa nyingi za miradi. Nalo pia tatizo. Zikipunguwa tatizo na zikizidi Tatizo.