Hali ya SGR ni mbaya na mradi haujulikani utakamilika lini

Nani kakwambia mradi umesimama!?

Mbona hamjiongezi kufatilia zaidi ya kusaka vijarida vya udaku na kuleta hapa

Mradi unaenda vizuri zaidi ya jana
Sawa mkuu.

Sasa tueleze, kipande cha Dar hadi Moro tutapanda treni lini? Hili ni swali dogo tu kwako, mtu mwenye uhakika wa unachozungumzia, kama ulivyoonyesha kwenye maneno yako machache hapo juu yasiyokuwa na ushahidi wowote.
 
This is unaccepatable huu mradi haiwezekan ukaachwa ukafa itakuwa loss kubwa ya takriban trillion 23+ sisi kama taifa hatuiwez hii hasara na fedhea
Nyinyi kama taifa mlishawahi kufanya nini, ndio umekwama sasa. Mnaleta mkwala mbuzi kutishia kuuma!
 
Sawa mkuu.

Sasa tueleze, kipande cha Dar hadi Moro tutapanda treni lini? Hili ni swali dogo tu kwako, mtu mwenye uhakika wa unachozungumzia, kama ulivyoonyesha kwenye maneno yako machache hapo juu yasiyokuwa na ushahidi wowote.
Kwanza vipande vyote kutoka Dar Hadi Dom vimeisha kinasubiriwa ni vichwa kutoka Kwa manufacturer,Kituo Cha umeme Cha Chalinze tayari na pia bwawa la umeme by June litakuwa tayari.

So Sgr mtapanda 2024 July
 
Umeandika takataka tuu, mifano Yako yote ni Majitu yaliyofeli

View: https://twitter.com/dseinsights/status/1714656045472022755?t=loeQXffQR5gwMpN-TITeJA&s=19
 
Sasa hapa ndio umeandika nini we Jamaa.

Unamkumbuka Kwamba VP Mpango alisema Mkandarasi wa bwawa la Nyerere hana uwezo na limejemgwa chini ya kiwango? Aliyewaleta hao Wakandarasi unawajua? Waliomleta huyu aliyefilisika kwenye Sgr humjui?

Muwe mnatunza kumbukumbu sio mnajaza mavi vichwani.
 
Ni uzushi ndio maana hawawezi kuwataja.

Mkandarasi ametangaza kufilisika hana pesa watu wanasema eti mkandarasi aliwalipa ten percent ndio amefilisika,hii ni akili au matppe na jitu zima linaamini.hizi takataka za Kigogo.

Ndio maana hawezi taja Kwa sababu ni uzushi.

Ukipenda cheap haya ndio matokeo yake.
 
This is unaccepatable huu mradi haiwezekan ukaachwa ukafa itakuwa loss kubwa ya takriban trillion 23+ sisi kama taifa hatuiwez hii hasara na fedhea
Utafanya nini??
 
Kwanza vipande vyote kutoka Dar Hadi Dom vimeisha kinasubiriwa ni vichwa kutoka Kwa manufacturer,Kituo Cha umeme Cha Chalinze tayari na pia bwawa la umeme by June litakuwa tayari.

So Sgr mtapanda 2024 July
Mimi sikuuliza yote hayo, nimeuliza tu hilo la Dar-Moro, kwa sababu hadithi kama hizo zako ziliimbwa toka miaka mitatu iliyopita kukihusu kipande hicho tu basi!
 
Miradi ya SGR na Nyerere Dam ni muhimu sana Kwa maendeleo ya watoto wa tz, ni Bora serikali waibe Kila kitu watumalizie hii miradi. Ikiisha serikali itavuna mabilioni na hata tozo hawatatukamua kubwa!

Kenya SGR Yao iliishia njiani Naivasha kwa ufisadi za kutosha, kwasasa wanalaumiana , mradi wao hauna faida na deni raia wanalipa , kumbe nasisi Bongo ni viazi tu kama Kenya, hii ngozi nyeusi inawezekana Ina laana Maana Mama yetu sijui anaishi nchi Gani Ina Maana halioni hili? Kwanini halisemei? Maisha yenyewe mafupi tu!
 
Wewe unajulikana toka siku nyingi kuwa ni mpumbavu/chizi tu fulani ambaye hupoteza muda wake mwingi humu akibandika uchafu, sasa unataka nijihusishe kweli na mtu kama wewe?
Huna akili wewe na huyo unaemtetea aliyeanzisha Sgr tembo mweupe kwenda kusiko na maana yeyote kiuchumi.

Napendekeza somo la basics of economics liwe la lazima Kwa watu wote hususani viongozi Ili walau wajue scale of preference itasaidia ukurupukaji kama wa kina Mwendazake.

We mpumbavu hakuna mwananchi ana shida na Sgr Nchi hii na Wala haitasaisia chochote kama ambavyo Tazara haijasaidia chochote
 
Mimi sikuuliza yote hayo, nimeuliza tu hilo la Dar-Moro, kwa sababu hadithi kama hizo zako ziliimbwa toka miaka mitatu iliyopita kukihusu kipande hicho tu basi!
Muulize Mwendazake aliyewaambia itakamilika 2019 akafa hata 70% hakufikosha.

Nimeshajibu hapo awali kama hujasoma rejea post sawa wewe mbuzi wa Simiyu.

Mwisho kabisa siko Dar Kwa Sasa,Kwa mara ya mwisho Kwa hiyo section ni Daraja la Juu la kuingia bandarini kule ndio palisalia kwingine kote ilishakamilika kitambo.
 
Najuwa historia kuliko unavyodhani, Nchi haiendeshwi kwa kutegemea mtu nchi ni mfumo kwa maana hata huyo mtu kesho akiwa hayupo mfumo bora ndio unaendesha nchi. Sasa nikuulize wewe Sokoine unamkumbuka kwa lipi kubwa? utasema walishika waizi na wahujumu uchumi, sasa nchi yenyewe wakati wake ilikuwa umefilisika zero sasa watu wataiba nini? nchi haikuwa na mradi wowote zaidi inatafuta pesa kulipa mishahara tu. Kuwe na sheria wewe umeshutumiwa unapelekwa mahakama maalumu, umepatikana na hatia hukumu inatolewa unataifishwa kila kitu na unaenda ndani. Kama sio mahakama basi mfanyakazi ameajiriwa na ajira inasheria zake za kazi, kuwe na sheria kuundwa idara nyeti ya kumuweka mtu kitu moto na kuonesha shutuma za kweli au hapana ukiwa na ushahidi wa vielelezo ni kama audit halafu sheria inachukuwa nafasi yake.

Kama wewe bado unaishi kwa mawazo ya Sokoine basi tuna hasara kubwa, wale ndio walileta umaskini nchi hii kuwatisha watu kufanya biashara mpaka kumwaga vyakula chooni na pesa sababu wao kila mwenye pesa alikuwa muhujumu uchumi lakini hawaku deal na wazi wa mali ya umma walijikita na matajiri, ndio wakazidisha umaskini nchi hii. Sokoine ukiambiwa orodhesha hapa nini kikubwa alifanya kusaidia kuinua uchumi wa nchi hii? zero zaidi ya ukali. acha kukaririri kusifia viongozi waliokuwa chachu ya umaskini nchi hii waliwavisha watu matairi kama viatu halafu unataka nikae hapa ni mtukuze, kwa lipi?
 
Na wewe ukianza nani kamleta nani alisema hivi wewe ndio ujiulize unaandika nini. Mradi wowote kuna kampuni inalipwa kusimamia viwango kwa maana inamsimamia yule anayejenga na mradi unajengwa kutokana na design ukienda kinyume anawajibika msimamizi wa mradi. Shida watu wajinga kama wewe mliaminishwa tunajenda kwa pesa za ndani bila kuuliza zimetoka wapi na makofi mkapiga.
 
Swala sio nani analiowa kusimamia viwango,ukishaingia Chaka ni Chaka tuu.Nikuwekee hapa video ya VP.akisema hayo?

Tushaingizwa Chaka sana na watu msio na akili na wakurupukaji

View: https://twitter.com/dseinsights/status/1714657248348188950?t=nIDMqFsrszp2RFU9ub0Stw&s=19
 
Sasa VP anamwambia nani? anamlalamikia nani? yeye si VP yuko kwenye serikali? huo sio wajibu wake kutoa majibu? ukiuona kiongozi analalamika badala yakuja na solution ujue huyo ni takataka.
 
Sasa VP anamwambia nani? anamlalamikia nani? yeye si VP yuko kwenye serikali? huo sio wajibu wake kutoa majibu? ukiuona kiongozi analalamika badala yakuja na solution ujue huyo ni takataka.
Makosa yalishafanywa na awamu ya 5,yeye hanuwa kwenye nafasi ya maamuzi ya Rais labda Ushauri lakini Jiwe alikuwa hashauriki ndio maana hata bwawa likechelewa Kwa sababu ilibidi mchina badala ya kuwa subcontractors akageuka kuwa mkandarasi Mkuu Juu ya dalali yule wa Kiarabu aliyeletwa.

Makosa kama hayo ndio yalifangika Kwa mkandarasi Yapi Merkezi aliyefilisika Sasa anatafuta mshirika mwenye Nguvu za hela awe joint venture.

Kwa nini yote haya sababu ni Moja Mwendazake yeye alitaka kuwa injinia, project meneja, Waziri wa Fedha,evaluator, IGP,Rais yaani haambiliki.
 
Narudia tena ukiwa kiongozi ni lazima uwe na uwezo wakuja na solution, kiongozi yoyote akija madarakani na kuanza kulaumu kiongozi aliyepita huyo hafai kuwa kiongozi. Madaraka yanapita mikononi mwa watu na yako mazuri na mabaya yanafanyika. Sasa awamu tano zote zimepita mi mwendo wa kurekebisha na kuendeleza mazuri na kumbuka ni chama kimoja CCM. Sasa turudi kwenye topic, VP alikuwa waziri wa fedha awamu ya 5 na waziri muhimu katika awamu ile na hapa ndio tunakosa maadili ya kuwa viongozi, Mimi kama naona sikubaliani na jinsi unavyofanya jambo fulani unaomba kuondoka kwenye serikali hiyo ili upate muda wa kutoa maoni yako huru, huwezi kukaa kimyaa halafu leo useme mimi sikuhusika hapana ni udhaifu wa mtu kuwa kiongozi. Ukiwa ndani ya serikali ni collective responsibility hutaki una resign ndio mwanamme mwenye msimamo. ukibaki ndani wewe ni sehemu usikimbie kuwajibika.

Ndio maana kocha akiondoka anaondoka na jopo lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…