HALIMA MDEE, FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO UMEPELEKA WAPI?
Bunge la JMT limetunga Sheria iliyoanzisha na kusimamia fedha za mfuko wa Jimbo kwa lengo la kurahisisha na kumsaidia Mbunge wa kuchaguliwa Jimboni kupata fedha hizo kwa lengo la kurahisisha kutatua changamoto mbali mbali za Maendeleo katika jimbo mfano kusaidia kuboresha majengo na miundombinu mbali mbali za mashule, barabara, hospital na kunawakati zinaweza kutumika katika kusaidia makundi mbali mbali katika Jamii.
Ina kadiriwa kiasi Cha bilioni 3 hutolewa kwa kila Jimbo kwa kipindi Cha miaka yote 5 ya utawala wa Mbunge wa Jimbo wa kuchaguliwa likiwemo Jimbo la kawe lakini chakushangaza fedha hizo zimetumika kinyume na utaratibu wake.
Katika Nyakati tofauti Halima Mdee ameziomba fedha hizo za mfuko wa Jimbo kwa matumizi flani yakiyopitishwa na kamati inayotambulika kisheria lakini Mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo hazipeleki kwa walengwa ambao ni wananchi badala yake zinatumika kujenga chama kitaifa na kuwakoshesha wananchi wa Kawe Maendeleo ambayo hadi hivi leo Kuna sehemu bado Zina changamoto kubwa.
Hali hiyo ya matumizi mabaya ya fedha hizo imempa wakati mguu katika kampeni zake za kuwania Ubunge kwa Mara ya tatu mfululizo lakini wananchi wamemkataa mpaka atakapo waeleza zaidi ya bilioni 2 zimepotelea wapi maana katika ripoti yake ya utekelezaji inaonyesha bilioni 1 tu umetumika lakini bilioni 2 hazijulikani hazipo.