TheMnyonge
JF-Expert Member
- Mar 25, 2022
- 738
- 1,886
Una maoni chanya lakini nakukumbusha pia kwamba, CCM imefanya mara nyingi tu kuwafukuza uanachama wanachama wake, alifukuzwa Sofia Simba, Jesca Msambatavangu, Benard Membe na wengine wengi tu katika historia!..Katika kitu ambacho CCM inawapiga bao upinzani ni uwezo wa kutunza watu ! Si kwamba hawakwaruzani bali misingi ya chama inatambua kuwa chamacha siasa chochote msingi wake ni watu .
Leo hii unampiga chini mdee! Je unakumbuka sakata la Makamba na Kinana au lile la Nape au lile la Lowasa hawa wote hawakuwahi kufukuzwa CCM kwakuwa “Mtu si Mbwa”
Kuna wanachama wengi wenye uwezo pengine hata kuzidi wakina Mdee lakini Halima Mdee ni mmoja na nguvu iliyotumika kumtengeneza haiwezi kuachwa iende bure .Huhitaji kuwa mbobezi wa siasa kujua kuwa Mdee akienda kokote akasimama na mwanamama au mwanasiasa yoyote ataleta ushindani kwani “There is no bad publicity” .
CDM lazima ijifunze kutunza watu hii trend imeanzia kwakina Zitto na wengine ni udhaifu wao mkubwa na inawachelewesha kupata walau wabunge 100 .
Tofauti sio kwa CHADEMA NA CCM, wote wanatoa adhabu za kufukuza wanachama wao, tofauti ni kwamba wana- CCM wengi wakifukuzwa wanajua cha kufanya, (hutulia na kukiri makosa yao) baadaye chama huwasamehe!
Tofauti na walichofanya au wanachofanya akina Halima, yaani wanashirikiana na Magufuli+ Ndugai+ Tume ya uchaguzi, ku-surbotage maamuzi ya chama,wanaamua kuota mapembe kwa ujeuri unaolindwa na waliowapeleka, then bado hawaombi radhi, ila unataka chama kiwasamehe kwa sababu ni wanachama wazoefu?(seriously????)
Nionavyo, chadema wamefanya maamuzi sahihi kabisa, as long as hawakuona sababu ya kuomba radhi kwa waliyoyafanya basi ni haki yao kuadhibiwa!
Hakuna chama kinaweza kubeba wanachama wanaojiona kuwa wakubwa kuliko chama chao!