Halima Mdee: Mbowe alikuwa anatafuta huruma tu, hajawahi kuzungumza na Wazazi wangu

Halima Mdee: Mbowe alikuwa anatafuta huruma tu, hajawahi kuzungumza na Wazazi wangu

Katika kitu ambacho CCM inawapiga bao upinzani ni uwezo wa kutunza watu ! Si kwamba hawakwaruzani bali misingi ya chama inatambua kuwa chamacha siasa chochote msingi wake ni watu .

Leo hii unampiga chini mdee! Je unakumbuka sakata la Makamba na Kinana au lile la Nape au lile la Lowasa hawa wote hawakuwahi kufukuzwa CCM kwakuwa “Mtu si Mbwa”

Kuna wanachama wengi wenye uwezo pengine hata kuzidi wakina Mdee lakini Halima Mdee ni mmoja na nguvu iliyotumika kumtengeneza haiwezi kuachwa iende bure .Huhitaji kuwa mbobezi wa siasa kujua kuwa Mdee akienda kokote akasimama na mwanamama au mwanasiasa yoyote ataleta ushindani kwani “There is no bad publicity” .

CDM lazima ijifunze kutunza watu hii trend imeanzia kwakina Zitto na wengine ni udhaifu wao mkubwa na inawachelewesha kupata walau wabunge 100 .
Una maoni chanya lakini nakukumbusha pia kwamba, CCM imefanya mara nyingi tu kuwafukuza uanachama wanachama wake, alifukuzwa Sofia Simba, Jesca Msambatavangu, Benard Membe na wengine wengi tu katika historia!..
Tofauti sio kwa CHADEMA NA CCM, wote wanatoa adhabu za kufukuza wanachama wao, tofauti ni kwamba wana- CCM wengi wakifukuzwa wanajua cha kufanya, (hutulia na kukiri makosa yao) baadaye chama huwasamehe!

Tofauti na walichofanya au wanachofanya akina Halima, yaani wanashirikiana na Magufuli+ Ndugai+ Tume ya uchaguzi, ku-surbotage maamuzi ya chama,wanaamua kuota mapembe kwa ujeuri unaolindwa na waliowapeleka, then bado hawaombi radhi, ila unataka chama kiwasamehe kwa sababu ni wanachama wazoefu?(seriously????)
Nionavyo, chadema wamefanya maamuzi sahihi kabisa, as long as hawakuona sababu ya kuomba radhi kwa waliyoyafanya basi ni haki yao kuadhibiwa!
Hakuna chama kinaweza kubeba wanachama wanaojiona kuwa wakubwa kuliko chama chao!
 
kongole kwa hii hoja yako.

Halima alitakiwa aulizwe maswali yafuatayo.

1. Ni kikao gani cha Chadema kilipitisha majina yao kuwa wabunge wa viti maalum.

2. Ni kiongozi gani wa Chadema alijaza fomu za uteuzi za kina Halima na kuzipeleka Tume ya Uchaguzi.

Kama Halima angekuwa mkweli angeeleza mambo hayo mawili na suala hili lingefikia tamati.

Binafsi inanishangaza kwa VYOMBO VYA HABARI vya Tanzania vimeshindwa kudadisi mambo hayo mawili.

Cc Erythrocyte , Kalamu1, Nguruvi3
Halima alikuwa na nafasi nzuri kabisa ya kueleza mkasa wote huu ulivyotokea katika mkutano huo. Hii ndiyo ilikuwa nafasi yao nzuri ya kuhitimisha kila kitu, lakini hakufanya hivyo, kwa sababu zipi?
Alikula nadhiri kwamba asiseme kitu wakati walipokuwa wnapanga mipango ya kwenda Bungeni, kwamba hakuna kuzungumzia mambo hayo?

Kuna njia nzuri za kuzungumzia jambo bila hata ya kumsuta au kumshutumu kiongozi wako, kama alihusika na jambo hilo, bila ya kuonekana kuwa unavutana naye, na watu wakakuelewa.

Halima na uwezo wake aliokwishauonyesha huko nyuma, kabaki tu wa kusema "UHUNI"?

Kama ilikuwa ni mipango ya kuendeleza uhujumu wa chama chao, iliyotokea nje ya chama, kwani angeizungumzia mipango hiyo, wajumbe bado wasingeweza kuelewa na kupiga kura kutokana na uelewa huo?

Haya mambo kamwe hayawezi kujificha milele. Ni swala la muda tu, kila kitu kitajitokeza nje, na tutajua kilichotokea.

Mwisho, nami niulize swali: Hivi Halima ni mmoja kati ya wale waliowasilisha rufaa ya kufukuzwa ndani ya chama? Inafahamika kwamba baadhi yao walighaili kufanya hivyo, sasa sijui kama Halima ni mmoja wa hao. Kama ni kati ya hao ambao hawakujishughulisha, basi tutaanzia hapo kukisia mambo.
 
Kwenye hili sina upande, ila kwa hili la Wazazi kwani ni lazima Wazazi wamwambie Halima kuwa walikutana na Mbowe?. haswa kama hawakuafikiana?.

Huenda walimwambia sisi hatutaweza kuongea chochote na Halima.
 
Dj ni msanii sanii sana , tangu apange njama za kumuuwa Sabaya simwamini kabisa
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Yani we jamaa najaribugi kuimagine upoje, nakosa jibu. Wala hujishughurishagi kufikiri
 
Katika kitu ambacho CCM inawapiga bao upinzani ni uwezo wa kutunza watu ! Si kwamba hawakwaruzani bali misingi ya chama inatambua kuwa chamacha siasa chochote msingi wake ni watu .

Leo hii unampiga chini mdee! Je unakumbuka sakata la Makamba na Kinana au lile la Nape au lile la Lowasa hawa wote hawakuwahi kufukuzwa CCM kwakuwa “Mtu si Mbwa”

Kuna wanachama wengi wenye uwezo pengine hata kuzidi wakina Mdee lakini Halima Mdee ni mmoja na nguvu iliyotumika kumtengeneza haiwezi kuachwa iende bure .Huhitaji kuwa mbobezi wa siasa kujua kuwa Mdee akienda kokote akasimama na mwanamama au mwanasiasa yoyote ataleta ushindani kwani “There is no bad publicity” .

CDM lazima ijifunze kutunza watu hii trend imeanzia kwakina Zitto na wengine ni udhaifu wao mkubwa na inawachelewesha kupata walau wabunge 100 .
Akishachafuka inabidi kumfungia milango hata awe mzuri vipi. Kumbuka hata Yesu alipokuwa msalabani Mungu alimpa kisogo maana alikuwa amebeba dhambi za ulimwengu ndio maana Yesu akalia akisema Mungu wangu mbona unaniacha? Kama vipi niepushe na kikombe hiki. Mdee ameshachafuka hata awe mzuri vipi ni jambo la busara kumwacha aende.
 
"Freeman Mbowe aliamua kutafuta huruma tu kwa wajumbe wa Baraza Kuu kwa kunitajia wazazi wangu, hajawahi kuzungumza na wazazi wangu hata siku moja kuhusu sakata hili, Nilisikitika, na sikuwa na nafasi ya kujibu," kauli ya Halima Mdee mara baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kusema kuwa alizungumza na wazazi wake kuhusu kuuacha Ubunge alionao sasa.

Chanzo: Dar Mpya

Haya yanatoka wapi tena?

Maelezo haya kumhusu Halima Mdee, tumeambiwa yalitolewa mbele yake Halima Mdee, wajumbe wote wa Baraza kuu na mbele ya wenzake wote 18 Mdee na kuhitimishwa na M/Kiti kumtaka Halima Mdee naye asimame mbele ya Baraza Kuu aseme kwa kinywa chake kama hayo maelezo ni ya KWELI ama UONGO...

Halima Mdee hakusimama KUYAKANUSHA ama KUYAKUBALI...

Na mtu anaposomewa mashitaka yake mbele ya mahakama na kuulizwa kweli au siyo kweli halafu akanyamaza kimya tu, maana yake hiyo ni ishara ya KWELI...

Sasa leo baada ya kuhukumiwa iweje aanze kulalamika akiwa gerezani wakati alikuwa na muda wa kujitetea..???
 
Yaani Mdee yupo sahihi na ndiye anapendwa na watanzania kuliko makajanja yenu ya NGO iliyokufa. Kwa taarifa yako Mdee sasa ni maarufu kuzidi huyo mwenyekiti wenu gaidi wa hicho ki NGO chenu, na tena asubiri DPP atalifufua file afungwe
Watanzania wenyewe ndio wewe?
 
Katika kitu ambacho CCM inawapiga bao upinzani ni uwezo wa kutunza watu ! Si kwamba hawakwaruzani bali misingi ya chama inatambua kuwa chamacha siasa chochote msingi wake ni watu .

Leo hii unampiga chini mdee! Je unakumbuka sakata la Makamba na Kinana au lile la Nape au lile la Lowasa hawa wote hawakuwahi kufukuzwa CCM kwakuwa “Mtu si Mbwa”

Kuna wanachama wengi wenye uwezo pengine hata kuzidi wakina Mdee lakini Halima Mdee ni mmoja na nguvu iliyotumika kumtengeneza haiwezi kuachwa iende bure .Huhitaji kuwa mbobezi wa siasa kujua kuwa Mdee akienda kokote akasimama na mwanamama au mwanasiasa yoyote ataleta ushindani kwani “There is no bad publicity” .

CDM lazima ijifunze kutunza watu hii trend imeanzia kwakina Zitto na wengine ni udhaifu wao mkubwa na inawachelewesha kupata walau wabunge 100 .

Hakuna mtu muhimu duniani
 
"Freeman Mbowe aliamua kutafuta huruma tu kwa wajumbe wa Baraza Kuu kwa kunitajia wazazi wangu, hajawahi kuzungumza na wazazi wangu hata siku moja kuhusu sakata hili, Nilisikitika, na sikuwa na nafasi ya kujibu," kauli ya Halima Mdee mara baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kusema kuwa alizungumza na wazazi wake kuhusu kuuacha Ubunge alionao sasa.

Chanzo: Dar Mpya
Naona mna tafuta huruma kumpitia Halima. Kama mna mpenda kamuoe maana hana bwana
 
🔴 Maisha ndivyo yalivya

🔴 Unachukua katoto cha simba kalikotelekezwa kadogo, unakatunza , unakapa maziwa , kanakuwa urembo wa nyumba ,nnamaita petty kanakuwa fadhila yake kanakutafuna

🔴 Unamchukua ndugu yako choka mbaya kijijini, unamleta mjini unampa mradi wako anakuhujumu, anakufilisi na anaanza kujijenga na kukufanya uwe adui yake hadi nyumbani

🔴 Unamchukua demu wako choka mbaya, unaamua kumsomesha au kumfungulia biashara ili msaidiane kimaisha lakini baadaye anakutana na majitu mengine, anakugeuka na kuchukuliwa na majamaa mengine

🔴 Unamchukua mdogo wako unamfundisha maisha, unamsimamia , baada ya kuujua mji anaanza madharau, alikuwa anakusalimia brodher shikamoo sasa anakutaja kwa jina lako kitu ambacho zamani hakikuwepo

⛔ Anakuja mfanyakazi mpya kwenye taasisi, mburura kabisa hajui chochote na hala hela yoyote, wewe unampokea kama boss wake au mfanyakazi mwenzake, unamfundisha kazi, na kum suport financial mpaka anakaa sawa na kuelewa kazi. Huyohuyo anaanza kukupiga majungu na kukuhujumu ili ufukuzwe kazi au aipindue nafasi yako
 
Hapa ni story ya he said she said. Kwa speculations zangu, nina Conjectures au Lemmas au Postulates ambazo siwezi kuziandika kwa vile sina factsza kutosha.
 
[emoji837] Maisha ndivyo yalivya

[emoji837] Unachukua katoto cha simba kalikotelekezwa kadogo, unakatunza , unakapa maziwa , kanakuwa urembo wa nyumba ,nnamaita petty kanakuwa fadhila yake kanakutafuna

[emoji837] Unamchukua ndugu yako choka mbaya kijijini, unamleta mjini unampa mradi wako anakuhujumu, anakufilisi na anaanza kujijenga na kukufanya uwe adui yake hadi nyumbani

[emoji837] Unamchukua demu wako choka mbaya, unaamua kumsomesha au kumfungulia biashara ili msaidiane kimaisha lakini baadaye anakutana na majitu mengine, anakugeuka na kuchukuliwa na majamaa mengine

[emoji837] Unamchukua mdogo wako unamfundisha maisha, unamsimamia , baada ya kuujua mji anaanza madharau, alikuwa anakusalimia brodher shikamoo sasa anakutaja kwa jina lako kitu ambacho zamani hakikuwepo
Yeah, 100%..
 
Back
Top Bottom