Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Wapo Live ITV sasa hivi.

Halima anaongea
 
Hasira zenu mnaapomwona mtu akihusiana na CCM ama kusikia Tu ana mahusiano na mtu wa CCM mnamtimua, Chama kitabaki kimekonda Hadi watu mliomo ndani!!

Fuatilieni Kwa kuthibitisha Kwanza hayo mahusiano yalisababishwa na Nani?
Hata akibaki mmoja hakuna shida ikiwa tu ni mpiganaji wa kweli. Mbona suala la kufukuzwa lipo kwa kila chama. Labda nitajie chama maarufu hapa Tanzania ambacho hakijawahi kufukuza wanachama ndani ya chama
 
Ile saini ndio utata wenyewe hata kama si ya kweli, tunataka Democrasia iwe Pana zaidi mkuu, hata kwenye mambo ya uzushi, utafutwe ukweli Kwanza ndio hukumu ifuate
 
Madaraka ni matamu Jamani, lakini pesa ya ubunge ni tamu zaidi.
 
Hata akibaki mmoja Hakuna shida ikiwa tu Ni mpiganaji wa kweli. Mbona suala la kufukizwa lipo kwa kila chama. Labda nitajie chama maarufu hapa Tanzania ambacho hakijawahi kufukuza wanachama ndani ya chama
Swala la demokrasia ni la muhimu zaidi kuliko kurupu kakara zenu
 
Mbona Halima anaongea kama vile anajisemea yeye peke yake wakati anatakiwa kuwasemea wenzake wote?
 
Chadema walifanya makosa makubwa Sana kuwafukuza wabunge wao bila ya kubaini ukweli wa Jambo lenyewe
Si waliitwa, na wakakataa kwenda.. Acha wale jeuri yao
Hivi inawezekana kwa mtu mzima mwenye akili zake timamu mwanachama kindakindaki akashawishiwa kirahisirahisi hivyo.wewe unaweza kushawishiwa kwa namna hiyo
Kwahiyo na wewe unaamini kuwa majina yalipelekwa na CHADEMA? Nikuulize yule aliyekuwa gerezani kwa siku 133, akaachiwa usiku saa moja, asubuhi akaapishwa kuwa mbunge, Je, hao CHADEMA walijuaje kuwa atakuwa huru mpaka watume jina lake Tume?

Unashindwa kutumia akili yako kubwa kufikiri?
 
CHADEMA kindakindaki huku bado mmekumbatia ubunge, stop kidding me.

Option is simple, rudini CHADEMA muachie ubunge au bakini na ubunge muondoke Chadema.

Msituchezee akili.
 
Hakuna mkubwa zaid ya CHADEMA wanajisumbua tuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…