Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Kosa ni fairness in terms of Natural justice.

Ila anakubali kuwa walifutwa uanachama kihalali.
Kama fairness haikuwepo siyo kwamba hata maamuzi yalitolewa na hiyo unfair committee ni batili??

Tafadhali mtusaidie kufafanua enyi wajuvi wa sheria
 

..hakuna Baraza kuu la chama chochote linaloketi, au kufanya maamuzi, bila Mwenyekiti, na viongozi wakuu wa chama, kushiriki.

..Jaji alitakiwa kuangalia na kuzingatia kama rufaa ya kina Halima ilisikilizwa kwa kufuata vile Katiba ya Chadema inavyoelekeza.
 
Ni kweli, walichofanya kina Mdee baraka za Mbowe zinaonekana japo CDM hawawezi kukiri hilo, hivyo Mbowe ni sehemu ya hili tatizo.

Tindo zitto junior
Mbowe anahusika vipi wakati anayepeleka fomu ni Mnyika na kamati kuu ndio hupitisha majina?

Mfano Nusrat alijaza fomu akiwa gerezani na alitolewa na DPP usiku ule ule ili akaape kesho yake. Je mbowe ana uwezo gani wa kutoa mtu magereza?
 
Atawavua vipi wakati rufaa yao haijasikilizwa?
Wabunge wa Cuf walifukuzwa uanachama Spika akawavua Ubunge wakakata Rufaa wakiwa Sio wabunge.Katiba ya Nchi inasema Mbunge anapoteza ubunge kwa kufukuzwa uanachama wake wala haisemi atapoteza ubunge baada ya kukataa Rufaa ni Uhuni wa Spika na Serikali ukizingatia namna Walivyopata UBUNGE wao kwa msaada wa Serikali Tume ya Uchaguzi na Spika

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 

Ok mkuu
 

Na huu ndio ukweli. Jaji kafanya maamuzi ya kijinga Sana. Kwa hivyo baraza kuu component yake ni akina nani? Maana hata viongozi wa kamati kuu wasipo Kaa, akina Halima Mdee watadai baraza kuu halijatimia.
 
Hukumu ina maajabu ndani yake kwa sababu composition ya baraza la juu imeundwa kwa mujibu wa katiba ya chadema, sasa mahakama inaposema composition hiyo ni batili inamaanisha pia kuwa katiba ya chadema ni batili. Kwa mawazo yangu mimi
 
Huyo rufaa utasimama wewe kama jaji ilo utamke hayo!
 
Hii maana yake hata samia haruhusiwi kusimamia Mkutano Mkuu wa CCM kwenye suala kama hili , je jambo hilo linawezekana ?
 
Hukumu ina maajabu ndani yake kwa sababu composition ya baraza la juu imeundwa kwa mujibu wa katiba ya chadema, sasa mahakama inaposema composition hiyo ni batili inamaanisha pia kuwa katiba ya chadema ni batili. Kwa mawazo yangu mimi
Mwambieni chairman arudishe kipengele alichong'oa!
 
Ni kweli, walichofanya kina Mdee baraka za Mbowe zinaonekana japo CDM hawawezi kukiri hilo, hivyo Mbowe ni sehemu ya hili tatizo.

Tindo zitto junior
Lakini inasikitisha; kwani CHADEMA walikuwa wameanza kuwakaba vizuri sana CCM. Ile kesi ya ugaidi na manyanyaso yote waliyokuwa wameyapitia nyakati za Magufuli, yote watu walikuwa wameyaona na kuyaelewa vizuri.

Kazi ya chama ilitakiwa kuanzia hapo na kwenda mbele; hasa ukichukulia ukosefu wa ushawishi alio nao mwenyekiti mpya wa CCM na madudu yake mapya, kama yale ya IGA ya DP World na ufisadi mwingi kama ripoti za CAG zinavyoonyesha; ilikuwa ni kazi ya CHADEMA kushikilia ilipokuwa imefikia na kuzidisha nguvu kuwaondoa CCM.
Hata maswala ya Katiba Mpya, na kusimama na kujieleza kwa nini wasingeruhusu uchaguzi usio haki, mambo ambayo yanaeleweka vizuri kwa wananchi..., kwa sababu azijuazo Mbowe pekee, yote haya yakazimwa!

Mbowe badala ya kuwa "HERO", kageuka kuwa "VILLAIN". Haijulikani sababu zilizomfanya ageuke 'so drastically' katika muda mfupi namna ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…